mmmh yani huu uzi umenishangaza, na mawazo kama haya ndo yameleta wanaume marioo, wasiotaka kufanya kazi ndio mana wadada wengi dunia ya leo unakuta mtu anajitolea hadi mahari aolewe, mwingine anaishi na mwanume lakini mwanaume hela yake ni pombe na wanawake hajui kodi ya nyumba wala watoto wanakula nini, huwa najiuliza mtu anawezaje kuishi na mwanaume wa namna hii, ila sasa nimeanza kupata majibu. Tunasahau kwamba kiasili mwanaume ameumbwa kutafuta, mimi kazi yangu kuzaa na kutunza familia, kuchangia kwangu ni ziada tu so mimi kama mwanamke kuwa nacho au kutokuwa nacho haitakiwi kuwa sababu kabisa kwenye mahusiano, na kiukweli naishukuru hiyo mentality manake mimi mwanaume ambae hana kitu nilikuwa simtaki, na nimeolewa na aina ya mwanaume nilikuwa namtaka na kaka wa watu wala hajui hata mshahara wangu na huwa haulizi, sio kama sichangii chochote lakini nachangia kwa kupenda kwangu vile nnavyojisikia. Mama zetu waliolewa enzi hizo na wanaume wenye pesa au hata wenye maisha ya kawaida tu wao wakiwa hawajasoma wala hawana kazi, auunakuta ana kazi lakini akiolewa tu anaambiwa acha kazi na waliishi maisha mazuri sana, mana the purpose was clear kazi ya mwanaume na mwanamke ilikuwa very clear kwenye ndoa, lakini wanawake wa sasa mnayakaribisha matatizo wenyewe, eti mkatafute wote kheeeeeeeeeee