Ladies, let’s do the real talk...

Sasa kama hana akili ya kuendesha mali zake angewezaje kuzitafuta na kuzizalisha hadi zikawa nyingi?
 
N༙A༙K༙U༙K༙U༙M༙B༙U༙S༙H༙A༙!!!

H༙A༙K༙I༙K༙I༙S༙H༙A༙ T༙A༙R༙E༙H༙E༙ 28 O༙C༙T༙O༙B༙E༙R༙ U༙N༙A༙M༙P༙I༙G༙I༙A༙ K༙U༙R༙A༙ W༙A༙K༙I༙L༙I༙ M༙S༙O༙M༙I༙ M༙H༙E༙S༙H༙I༙M༙I༙W༙A༙ T༙U༙N༙D༙U༙ L༙I༙S༙S༙U༙.
#NIYEYE
 
Vya kuchangia vipo vingi sana. Ndio maana hata mke ambaye ni mama wa nyumbani atapata mgao pasu pasu mkiachana. Mwanaume wa kuanza from scratch labda muwe mmetoka wote shule. Otherwise lazima atakua kuna mambo atakua ameshayaanza wewe umeyakuta katikati.

Hivi mfano mwanaume kamkuta mwanamke ana kila kitu naye anaenda kuchangia nini?
 
Wapo wengi hawana muongozo mzuri. Akikukuta unaakili unampa wazo afanye ivi aongeze mradi upi n.k
Acha kujidanganya.

Huna uwezo wa kumwambia chochote cha ajabu.

Alichopata ni akili zake, wewe ni nani useme hana muongozo mzuri?

Zaidi ni kumtia presha afilisike?
 
Mchango wake kwangu ni ku spoil furaha yangu, hiki ndicho wanawake wengi wanachokijua na kukiweza.

Anakuja kwako na maneno mengi matamu, kumbe moyoni ana bwana wake mwingine kabisaaaa

Kaka, mbona kama umevurugwa ?? Shemeji yetu amekufanyaje ??
 
wewe utakuwa m
Point yangu haipingi kusaidiana kimaisha na wala sijakataa kwamba maisha yamebadilika hivyo tunahitaji kusaidiana, na ndio mana nikasema hata mimi kwenye ndoa yangu japo mume wangu si mtu wa kufatilia kipato changu lakini still mimi mwenyewe najiongeza mana najua kama nataka tufike mbali kimaisha tunahitaji kusaidiana. Tatizo lipo kwa mleta mada, yeye ni kama vile anapinga mwanamke kuolewa au kuwa na mahusiano na mwanaume ambae tayari amejijenga kimaisha mwenye mali zake za majumba na magari na mabiashara, anataka kwamba tuolewe na wanaume ambao hawana kitu ili tukasaidiane kuchuma, like really????

Na pia si dhambi kuwa na mwanaume ambae hana kipato ilhali wewe mwanamke unacho alimradi awe na akili ya maisha, kweli hana lakini juhudi unaziona anapambana hata ukimpa mtaji unajua kabisa hela haitaenda bure, shida inakuja mpaka kijana anaitwa marioo, anakuwa hataki kujishugulisha yani alimradi wewe mwanamke unacho kazi yake kukupiga mizinga tu mbaya zaidia hadi familia yake wanaanza kuomba hela, anataka umlee tu hata ukimpa mtaji wa biashara mara nyingi ataishia kutumia kwenye starehe then anabaki hana kitu uendelee kumlea, umpe hela ya kula, ya kwendea gym na kwenda kunywea, hao ndo marioo na ndo vijana wengi wa leo hawa walamba midomo walivyo. Au mwingine unampa umtaji anafanya biashara akitoka kimaisha anakuona wewe tena si wa hadhi yake anaenda kuoa mwingine, na hili pia limeshawakuta wanawake wengi sana, au mwingine unakubali kuolewa nae hana kazi unatunza familia huku ukijua iko siku atapata mtatoka kimaisha, siku akipata kazi tu unakuwa hufai na ndoa inaishia hapo.
 
Yaan awe na akili za kutafuta mali zake alafu akose akili ya kuendeleza mali zake? Damn.....https://jamii.app/JFUserGuide it off
 
Ni kweli sio lazima uolewe na mtu fukara au kapuku ila alichotaka kuwasilisha nadhani hakijaeleweka kirahisi kwa baadhi ya wachangiaji.

Kwa jinsi nimeelewa ni kuwa alimaanisha ile hadhi na heshima apewayo mwanamke ambaye mmeanza nae from scratch ni tofauti na ile apewayo ambae amekuta everything in place. Hivyo anaekuta mazingira mazuri basi lazima awe na sifa ya ziada ya kuongezea thamani maisha ya yule mwanaume ili apate hadhi sawa na ambaye alichuma nae.

On the other hand, mwanaume kubadilika akipata depends on how you both lived and treated him. Kama ulimdharau na kumsimanga kwamba si lolote si chochote maana hakusaidii kitu wewe ndio kila kitu. Ukimjengea mentality kwamba wewe kuwa nae unamfanyia favor na unajuta hata kuwa nae kimahusiano basi tegemea tu siku mrija wa pesa ukifunguka atakubwaga bila kujiuliza mara 2! Na hili ndio kosa wanawake wengi hufanya bila kujijua ila sie wanaume huwa hatuongei tunauguliaga moyoni tu tukisubiria njia za riziki zifunguke.

Yani huu muda wa msoto ndio huwa una reveal true colors za wanawake tulio nao by 100% kama wako real na sisi au wanajilazimisha tu kwa kutuonea huruma tu iliojaa masimango. Mwanamke mshenzi atakudhalilisha mbele za watu, atakufedhehesha na atlast atakupora kauli yako kama kidume sababu anakupa tuff. Hizi tabia mie lazima nikuache at the end!

Mwanamke wa ukweli ndio anachukuaga point 3 katika kipindi hiki. Yani kuna wanawake wanajua kuziba ma gap ile mbaya. Huwa na heshima full, hawezi kuacha udhalilike na pia hawezi kukunyima sauti kama mwanaume.
 
Kikubwa kupendana tu haijalishi ana mali au hana mali. Unasema naenda kucontribute nini? Yeye hadi anakuja kunitaka atakuwa anahitaji nini? Mpaka akataka mahusiano basi kuna kitu ameona kinapungua katika maisha yake, hicho ndio nitakachocontribute
Tatizo huja pale wmbapo watu wataanza kusema "huyu binti ni good digger"
 
mwanamke unapaswa kumuheshimu mumeo....thats all.....mali kitu gani......sbb kuna ambao wameanza pamoja...mme mhangaikaji,,,,,uke ni mama kumunyumba.....sawa....but wana fujo balaaa.......hapo zikikubali unategemea nini....na ndio wanaoshinda kwenye masinagogi kuwaombea wenzao mabaya.......heshima na upendo......mali ni mbwembwe tuu....
 
Kiubinadamu: kila mtu anakuwa free na proud na ana uchungu na kitu ambacho amekitolea jasho. Ni nzuri zaidi kuanza na mtu kutoka chini; lakini pia sio lazima, na pia sio guarantee kwamba huko mbele atakuheshimu na kukutreat vizuri baada ya mambo kutiki. Sasa mtu kama alianza na mwingine chini wakafanikiwa ila wakashindwana; ndiyo kusema asioe au?

Mtu sahihi; regardless ana mali au hana mali ni mtu mwenye UTU. kuna wanaume hela hana na utu hana vile vile; leo utateseka na akizipata ndiyo utateseka zaidi. Tena mwanaume mwenye hela hadi akufuate ni kwamba wewe ndiye anayekuhitaji. Upendo wa maskini hauaminiki kwa kweli (hata mimi mwanamke maskini naweza kumkubalia mtu kisa tu hela). Inawezekama kabisa yupo na wewe kwa sababu ndiyo mtu ambaye he can afford at that time; ila dream woman wake ni mwingine kabisa. Akishapata hela ndiyo yale, sikutaki wewe sio type yangu. Au mwingine ndiyo ile tu nafsi inamsuta mmetoka mbali; basi utaendelea kuwa mke mtazamaji ila mkewe halisi atakuwa naye huko nje akizitumbua.

Na tusiwaseme tu mabinti kwamba wanapenda ready made; na wanaume wengi wa kiafrika wanazingua. Mtu unaanza naye chini huko mnapigika wee; siku nuru inaanza kuonekana unasema angalau sasa na mie ntaanza kuvaa na kanguo ka elfu 15; mwenzako ameshatafuta wa kuzitumia naye. Wewe ndani maisha yanabaki almost vile vile afu huko nje mwenzako anaspend tu. Ndiyo malipo yako hayo.

Kuna mdada humu alikuwa analalamika mumewe wameanzia huko chini, wakapambana wakaanzisha kampuni yao, sasa hivi imesimama maisha yamewanyookea. Lakini mume magari anapanda mwenyewe, mke anaenda ofisini na daladala. Yaani magari ya kwao lakini yeye anaishia kuyapigia picha kwa nje, kila kitu ni manyanyaso. Na usiseme mkewe alimnyanyasa zamani coz she did'nt. Na mtu akunyanyase afu akuvumilie miaka yote hiyo hadi mje mfanikiwe; obviously angeshamuacha au basi mshukuru tu alikupa mori ya kupambana. Ndiyo hayo wanawake wengi wanaishi kwa uchungu, anasubiri mume afilisike au agonjeke ndiyo anapata chance ya kulipiza. Na wanaume wakorofi uzeeni wanaisoma namba

Binti akikutana na mwanaume ana mali, akampenda na ana utu na anamuheshimu; kwa kweli aolewe tu. Usimkatae mtu kisa eti ana mali atakunyanyasa wakati mtu hajawahi hata kukudharau. Umaskini sio sifa wala sio kigezo cha kuja kuwa mume bora. So tusiwachukulie wanaume wote wenye mali kana kwamba hawafai na maskini wote ndiyo wanafaa. Kuna watu wana dharau zao za asili hata kama hana hela. Yaani hata muanze naye barabarani; kwake hutokuwa na hadhi wala heshima.

Kama mtu ana mali aombe tu apate mtu mwenye kujitambua; atakayekuwa na uchungu na mali za mumewe kwa sababu anajua ndiyo zitawasaidia watoto wao na wapendwa wao. Sio mtu ana akili ya ku-slay tu.
 
Ahsante mama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…