wewe utakuwa m
Point yangu haipingi kusaidiana kimaisha na wala sijakataa kwamba maisha yamebadilika hivyo tunahitaji kusaidiana, na ndio mana nikasema hata mimi kwenye ndoa yangu japo mume wangu si mtu wa kufatilia kipato changu lakini still mimi mwenyewe najiongeza mana najua kama nataka tufike mbali kimaisha tunahitaji kusaidiana. Tatizo lipo kwa mleta mada, yeye ni kama vile anapinga mwanamke kuolewa au kuwa na mahusiano na mwanaume ambae tayari amejijenga kimaisha mwenye mali zake za majumba na magari na mabiashara, anataka kwamba tuolewe na wanaume ambao hawana kitu ili tukasaidiane kuchuma, like really????
Na pia si dhambi kuwa na mwanaume ambae hana kipato ilhali wewe mwanamke unacho alimradi awe na akili ya maisha, kweli hana lakini juhudi unaziona anapambana hata ukimpa mtaji unajua kabisa hela haitaenda bure, shida inakuja mpaka kijana anaitwa marioo, anakuwa hataki kujishugulisha yani alimradi wewe mwanamke unacho kazi yake kukupiga mizinga tu mbaya zaidia hadi familia yake wanaanza kuomba hela, anataka umlee tu hata ukimpa mtaji wa biashara mara nyingi ataishia kutumia kwenye starehe then anabaki hana kitu uendelee kumlea, umpe hela ya kula, ya kwendea gym na kwenda kunywea, hao ndo marioo na ndo vijana wengi wa leo hawa walamba midomo walivyo. Au mwingine unampa umtaji anafanya biashara akitoka kimaisha anakuona wewe tena si wa hadhi yake anaenda kuoa mwingine, na hili pia limeshawakuta wanawake wengi sana, au mwingine unakubali kuolewa nae hana kazi unatunza familia huku ukijua iko siku atapata mtatoka kimaisha, siku akipata kazi tu unakuwa hufai na ndoa inaishia hapo.