Husninyo
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 23,851
- 9,472
Thread hii ni maalum kwa wadada hasa waliopo kwenye mahusiano ila bado hawajaolewa na wana mpango endelevu na wenza wao
Wadada wengi wanashindwa kutambua wapi wanapendwa na wapi wanadanganywa. Vigezo vifuatavyo vitakusaidia kutofautisha mwanaume anayekupenda na mwenye mpango wa kukuoa na Yule anaekutumia tu ila hana mpango na wewe.
Mawasiliano:
Mwanaume anaekupenda hawezi kumaliza siku bila kuwasiliana na wewes (kama hakuna external factors zinazosababisha mawasiliano yawe mabovu). Kama wewe ni mtu wa kupiga simu kila siku, kutuma emails lakini mwenzio haoneshi ushirikiano ujue hapo kuna utata.
Ushirikishwaji:
Anaekupenda ni lazima atakushirikisha mambo yake mengi yawe makubwa au madogo. Unaweza shirikishwa kwa namna ya kuombwa ushauri au kupewa taarifa. Kama upo kwenye uhusiano ila unashangaa mambo yanafanyika tu bila kuelewa ujue haupo myoni mwake, haoni kama waweza mshauri la maana na haoni kuna umuhimu wa wewe kujua.
Utambulisho.
Jiangalie kama unatambulika kwa ndugu, rafiki na jamaa zake wa karibu. Kama muda wa kutambulishana rasmi kwa wazazi haujafika, vipi kwa marafiki, wafanyakazi wenzie au makaka na madada!!. Unawafamu marafiki zake wawili wakati anao 30? Utambulisho huwa ni swala gumu kama mwanaume hakupendi na hajivunii kuwa na wewe. mwanaume ambae tayari ana mpenzi mwingine na anatambulika kwa watu wake wa karibu ni mzito kukutambulisha na wewe. inabidi ustuke hapo.
Mazingira.
Unapafahamu anapoishi? Anapofanya kazi? Maeneo anayopenda kutembelea? Kama jibu ni hapana, unahisi ni kwa nini? Kuna sababu nje ya uwezo wenu zinazosababisha usifahamu hayo ulishamwomba ufahamu ila alikataa? Hapa nakuachia utafakari mwenyewe.
Anakufahamu kiasi gani?
Kama upo na mpenzi lakini haoneshi interests za kutaka kukufahamu zaidi inabidi ujiulize mara mbili mbili. Kwa mfano, mpenzi wako anajua jina lako na mahali unapoishi tu. Hajui mazingira unayoishi, kazi unayofanya, hajui ndugu zako hata kwa kuwasikia ujue huyo mwanaume hakupendi. Anaekupenda ataandika kitabu kizima kukudescribe lakini asiyekupenda hata page 1 haitojaa.
Ubahili/ubinafsi
Hapa ni kwa wenye wapenzi wenye uwezo mzuri kifedha. Angalia kama anasikiliza shida zako na kujaribu kuzitatua. Inawezekana hakujali na hakuhudumii kipesa kwa sababu ana mpenzi mwingine ambae ameelekeza huko matumizi yake. Pengine hakuamini, anahisi hata akikuhudumia utamtosa; ila kama anashindwa kukuamini anawezaje kukupenda? Mtu wa hivyo hata upendo wake ni wa mashaka. Kama hana uwezo kifedha je anakuwa na wewe bega kwa bega unapokuwa na shida? Anayekupenda atakujali wakati wa shida na raha.
Ameoa.
Kama Unahitaji life partner halafu una date mume wa mtu ujue umepotea. Cha mtu ni cha mtu na mwanaume haoi kwa bahati mbaya. Probability ya kuolewa na huyo mwanaume ni 0.000000000000001. hapa huitaji kuambiwa jua linawaka au mvua inanyesha. Akili kichwani mwako.
NB: kigezo kimoja hakitoshi kuconclude kuwa hupendwi. Usisubiri mpaka mwanaume akutamkie kuwa hakupendi. Katika vigezo vyote hivyo nina mifano ya ukweli ambayo imewahi kunikuta mimi, ndugu zangu na marafiki.
KWA WALIOOLEWA:
KWA WANAUME:
Nakaribisha maoni, nyongeza, masahihisho etc. karibuni, jisikieni kama mmeuanza mwaka mpya wa2012, anaetaka vinywaji achukue kwenye jokofu.