Ladies, why?...!


Eiyer,
Hapa nasema kutoka chini ya sakafu ya moyo wangu. The same snario, yamenitokea, na hapa nitampa mwenza wangu naye asome thread hii ingawa italeta maneno tena. Mimi ni mfanyakaz wa Serikali, nina cheo kikubwa tu na pato langu si hapa kulinganisha na maisha ya mtanzania wa kawaida. Mwenzangu ni mjasiria mali, mtaji na plan ya biashara yake ni nguvu zangu, yeye katika mtaji hakutoa hata senti moja. Namshukuru, ni mzuri katika kusimamia biashara na anaingiza kipato kikubwa kwa mwezi. TATIZO LILIPO; hela yake ni sawa na ukoma, hakuna anayejua inakwenda wapi, hanunui chochote kile pale nyumbani kuanzia chakula, kulipa bili ya umeme, DSTV, maji,ada za watoto,gharama za matengenezo madogo kwa mafundi na mbaya zaidi miradi yangu hayuko tayari kuisimamia hata kama ana nafasi yuko radhi kuona nawatuma mafundi kununua vifaa vya ujenzi bila kuwasimami na mafundi kama unavyojua ni wachakachuaji wakubwa. Kwa mambo mengine ni mzuri, anajua wajibu wake kama mama, anajua wageni na n.k. Sikuona kugombana naye ni njia sahihi, ila nilimwambia ukweli kwamba kila mwisho wa mwezi alete pato lake na la kwangu tuchanganye then tupange matumizi, hiyo haikuwa rahisi mpaka wazee wa dini waliingilia. kwa sasa tunakwenda vizuri. Wana Jf, msishangae mbona haya ni ya kila siku kwenye maisha ya ndoa?? ila suala la divorce liwe ni hatua ya mwisho baada ya mengine kushindikana.
 
nikweli hiyo hua inatokea ila sio kwawanawake wote. wapo nawawake wao ndo baba ndomama katika familia zao nawaume zao wapo tuu hawanampango nafamilia zao. wao wakipata pesa zao wanalewea pombe nawengine wanahonga wavimada. hili swala lipo kwawote.
 
jamani wanaume acheni kukwepa majukumu kuhudumia mke na watoto ni wajibu wenu mimi siulizwi mshahara wangu na vocha nanunuliwa na saloon napewa hela na gari nawekewa mafuta. but pesa yangu natumia pale ninapojisikia wakati mwingine simuombi ila mwenyewe anajua majukumu yote ni yake. sasa ukiutolea macho mshahara wa wife utakuwa mvivu wa kutafuta, mwanaume hasifiwi sura bali utafutaji!
 
mimi naamini ni tabia ya mtu,lakini inapendeza ndani mahitaji mkisaidiana.kuna dada mmoja,kila kitu ndani alikuwa anatoa mume,imagine akienda kumnunulia nguo mtoto wake,risiti anampelekea mume,na mume analipa.na yeye huyo dada hela anazo.walikuja kuachana,alipata shida,analalamika tu sasa.kiufupi ni vizuri mpangiane majukumu,mimi nitafanya hiki na wewe utafanya kile,mnajikuta maisha yanaenda vizuri tu.mambo ya kumfanya mume ATM wako haipendezi.mume kum treat mke sio vibaya,lakini usi take advantage
 
Kaka shkamoo. Umetoweka siku hizi
Ngoja kijana ajifunze siasa za marriage game asije akaingia kichwa kichwa akachemsha. Muelimishe banaa, sifa ya mwanaume kuchunwa ( na mke na small house pia)

Ngoja odm aje amalizie.

King'asti my dear ndo majukumu nisijeshindwa bure kumhonga kipenzi changu!

Hivi huwa upo wapi si nimekukataza siasa, afu ukinionea Michelle tafadhali sana
 
Last edited by a moderator:
ebwana n'dai like,...;.;;;huyo bro wako ni mtu ws aina yangu kabsaaa/tyipical me
 
Kumbe ndoa hua zinavunjika kwa mambo madogo madogo namna hii??kha! Sasa hua watu wanaoana ili iweje?mwanaume hutaki kutimiza majukumu yako kwenye familia halafu uitwe kichwa cha nyumba inahuuuu???wanaume wa siku hizi wanapenda miteremko sana yaani unataka mkeo akichangia laki na wewe uweke laki?aibu gani hiyo!?
 

kisukari unakaa wapi nina maongezi na wewe
 
Last edited by a moderator:

Purple wewe ulitaka uweke ngapi au usiweke kabisa? Umemsoma cacico?
 
Last edited by a moderator:
Wenyewe wanasema maandiko matakatifu yalisema kwa 'ADAM ATAKULA KWA JASHO NA EVA ATAZAA KWA UCHUNGU' Mwanaume utahudumia familia yako tu, upende usipende na mwanamke akikugomea kukusaidia kama ana kazi huna la kufanya. Duu, kweli wanaume tumeumbwa matesooo!
 
Hapa umenena mrembo...


Mara nyingi kisukari unampata kwenye lile jukwaa lilee

kisukari unakaa wapi nina maongezi na wewe
 
ni kweli wababa mnaweza kuvunja ndoa sababu tu mke hachangii matumizi ya ndani? sidhani kama hili lina ukweli. huyo kaka yako hajasema ukweli kilichovunja ndoa yake, chunguzeni vizuri
 
Na kuna wanawake wangapi huwa wanawapa wakwe zao misaada ya kifedha? me nadhani hapa alichokosea yule mke mtu ni kutomshirikisha mume wake matumizi ya mradi aliopewa. Angeonesha ushirikiano pengine wasingefikia hatua ya kudevorcena inaonesha wazi kuwa mume alimpenda sana mkewe ila mke alitaka kuchuma mali. Jiulize hapa kuna ushirikiano kiasi cha kujenga nyumba kwa pamoja au kufanyiana michezo michafu tu.
 

I think thats too general.mm naona ni busara kumsaidia mume wangu katika kupanga mikakati mbalimbali ya maisha ikiwemo masuala yanayohusu finance.Nadhani na wanawake wengi siku hizi wapo hivi.Kuna ushahidi mwingi kutoka kwa watu wengi wamesomeshwa na mama zao sio tu kwa vile hao wamama ni single,bali ni kuwasaidia waume zao....
Mie nadhani huyo"kaka" yako nae hakutumia hekima...alipaswa kumuelimisha mkewe taratibu na kuwa na uvumilivu...
 
ni kweli wababa mnaweza kuvunja ndoa sababu tu mke hachangii matumizi ya ndani? sidhani kama hili lina ukweli. huyo kaka yako hajasema ukweli kilichovunja ndoa yake, chunguzeni vizuri
We unaamini anayezungumziwa ni kaka yake? Chezeya Eiyer wewe? Hebu fuatilia thread zake vizuri mkwe..... afu kumbe una sauti tamu kama ya kasuku eh?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…