Fugwe
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 1,676
- 663
Ni jana ndoa ya bro wangu ilikufa kabisa.Chanzo cha kifo cha ndoa hiyo ni baada ya bro kumfungulia mkewe biashara na kumkabidhi ili ajipatie mahitaji yake sio mpaka mumewe ampe.Lakini cha ajabu mkewe ameendelea kutoa shida zake kwa bro,bro akimuuliza mwanamke anajibu hela za dukani ni zake mke na yeye kama mume anatakiwa amhudumie tu!!!!Swala hili lilizusha ugomvi ulopelekea ndoa kuvunjika au kufa . . . . . . . . . . . . . . . .. . . . . . Kesi za namna hii ni nyingi sana,mwanamke anahitaji haki sawa,sijui hizo haki sawa anazitafsiri namna gani.Unakuta mwanamke ni mwajiriwa au ni mjasiriamali,mshahara au hela ya biashara haionekani nyumbani,akitakiwa wagawane matumizi ya nyumbani anang'aka,anasema hayo ni majukumu ya mume!Kwa nini?Wengine inafikia mpaka gharama za vocha,saloon,nguo wanadai kwa mume wakati wana kipato,ukiwauliza wanasema mi mke wa mtu bana,biashara au kazi yangu ni yangu haihusiani na ndoa/mahusiano yangu!Sasa najiuliza hicho kipato ni cha nini?. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .Wanawake wengine wanasaka vidume wenye hela wakati wao wanajimudu sijui ili iweje!Kuna mzee mmoja,mkewe ni mwajiriwa serikalini na yule mzee ni mfanyabiashara,imebidi kutumia ubabe,mkewe akipata mshahara lazima aulete nyumbani na utanunulia mahitaji ya nyumbani mpaka uishe wote siku hiyo!Namkubali sana huyu mzee.Wakati mwingine ni bora wanawake wasiwe na kazi au kipato kwa usalama wa familia.Labda mnaweza kuniambia hizo hela mnatafuta za nini?
Eiyer,
Hapa nasema kutoka chini ya sakafu ya moyo wangu. The same snario, yamenitokea, na hapa nitampa mwenza wangu naye asome thread hii ingawa italeta maneno tena. Mimi ni mfanyakaz wa Serikali, nina cheo kikubwa tu na pato langu si hapa kulinganisha na maisha ya mtanzania wa kawaida. Mwenzangu ni mjasiria mali, mtaji na plan ya biashara yake ni nguvu zangu, yeye katika mtaji hakutoa hata senti moja. Namshukuru, ni mzuri katika kusimamia biashara na anaingiza kipato kikubwa kwa mwezi. TATIZO LILIPO; hela yake ni sawa na ukoma, hakuna anayejua inakwenda wapi, hanunui chochote kile pale nyumbani kuanzia chakula, kulipa bili ya umeme, DSTV, maji,ada za watoto,gharama za matengenezo madogo kwa mafundi na mbaya zaidi miradi yangu hayuko tayari kuisimamia hata kama ana nafasi yuko radhi kuona nawatuma mafundi kununua vifaa vya ujenzi bila kuwasimami na mafundi kama unavyojua ni wachakachuaji wakubwa. Kwa mambo mengine ni mzuri, anajua wajibu wake kama mama, anajua wageni na n.k. Sikuona kugombana naye ni njia sahihi, ila nilimwambia ukweli kwamba kila mwisho wa mwezi alete pato lake na la kwangu tuchanganye then tupange matumizi, hiyo haikuwa rahisi mpaka wazee wa dini waliingilia. kwa sasa tunakwenda vizuri. Wana Jf, msishangae mbona haya ni ya kila siku kwenye maisha ya ndoa?? ila suala la divorce liwe ni hatua ya mwisho baada ya mengine kushindikana.
