NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva , Judith
Wambura Mbibo Jide ambaye hivi karibuni
ndoa yake iliripotiwa kuwa katika
sintofahamu na kuvunjika , anadaiwa kuhamia
katika hoteli moja yenye hadhi ya nyota tatu
iliyopo Oysterbay jijini Dar .
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jide amekuwa
akionekana akiingia na kutoka kwenye hoteli
hiyo huku nyumba yake iliyopo Kimara -
Temboni , Dar ikiwa haina mkazi wa kudumu .
Wiki iliyopita , kulienea taarifa katika
mitandao ya kijamii ikieleza kuvunjika kwa
ndoa ya Jide na mume wake, Gardner Gabriel
Fikirini Habash . Wawili hao walifunga ndoa
mwaka 2005 .
Taarifa zikadai kwamba Gardner naye
aliondoka nyumbani hapo na kwamba hivi
sasa anaishi kwa mmoja wa ndugu zake.
Hata hivyo
Ijumaa iliyopita Tulizungumza na Gardner
ambaye pia ni meneja wa msanii huyo, lakini
alikanusha vikali uvumi huo akisema si kweli .
Kufuatia madai hayo, mapaparazi wetu
walikwenda hadi nyumbani kwa nyota hao
ambapo hakukuonekana dalili za kuwepo kwa
mtu ndani .
Baadhi ya majirani walioulizwa, walisema
mara ya mwisho walimuona Gardner miezi
miwili iliyopita akiwa na basi la Bendi ya
Machozi lakini hawaelewi kwa sasa wanaishi
wapi na wakoje katika ndoa yao!
Juzi , mapaparazi wetu walipiga kambi
hotelini hapo ambapo mfanyakazi mmoja wa
hoteli hiyo alisema , Jide anaishi hotelini hapo
na kwamba kutokana na kuwa mteja wa
muda mrefu, hata kadi ya kufungulia mlango
wa chumba chake anaondoka nayo .
Mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Jide ( jina
tunalo) alithibitisha msanii huyo kuishi
hotelini hapo ingawa alikataa kuzungumza
lolote kuhusu ndoa hiyo , kwa kile alichodai
kuwa haieleweki .Ni kweli Anaconda ( Jide )
anaishi pale , wewe nenda tu mapokezi
kaulize utaelezwa kama hivi sasa yupo au
hayupo, alisema mtu huyo.
Juhudi za kutafuta ukweli wa sakata la nyota
hao zinaendelea huku ikielezwa kuwa ,
Gardner ndiye anayetakiwa kutoa tamko
kwani ndiye anayepatika kirahisi katika simu
yake ya mkononi .