Lady JayDee: Hii ni "TUZO" yangu ya 30...

Lady JayDee: Hii ni "TUZO" yangu ya 30...

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Msanii bora wa kike africa mashariki, Judith wambura mbibo aka lady jaydee ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook idadi ya tuzo anazomiliki mpaka sasa, ambapo amesema hii ni tuzo yake ya 30 kupata toka aanze muziki mwaka 2000.

Ni juzi tu shabiki wake warumi alipost jumla ya idadi ya tuzo anazomiliki msanii huyo ambapo alitaja tuzo ishirini na tatu tu (23) , hivyo msanii huyo kaibuka na idadi kamili ya tuzo anazozishikilia mpaka sasa ambazo ni 30.

"Boss wangu (Lady jaydee) nikuombe radhi na mashabiki wote kwa kupunguza idadi ya tuzo kutoka 30 hadi 23, unajua dada jide tuzo zilikuwa nyingi sana hadi nikachanganyikiwa kuzi orodhesha zote, maana nilikuwa naona mawenge kweli maana tuzo ni nyingi balaa."

"Tuzo yangu ya 30. Ahsanteni kwa ushirikiano, nimeipokea na ninarudi nayo nyumbani. Shhhhhh!! Kimya kimya"
Alipost lady jaydee kwenye ukurasa wake wa facebook
 
Last edited by a moderator:
hapo kwenye ''zilikuwa nyingi sana hadi nikachanganyikiwa'' pameniacha hoi!!
 
Kumbe huwa anajishaua bure kumbe anazipenda, huyu si ndiye aliuliza kwa dharau kama tuzo za KILI zimefanyika!!! kumbe nazo anazihesabu!!! aaha 'Sizitaki mbichi hizi'.
 
Nimebaki tu nacheka. Warumi umeshindikana kiama hahaha

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nimebaki tu nacheka. Warumi umeshindikana kiama hahaha

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Ahahah binamu sijakuona leo au na wewe ulikuwa airport kumpokea baba ubaya?
 
Kumbe huwa anajishaua bure kumbe anazipenda, huyu si ndiye aliuliza kwa dharau kama tuzo za KILI zimefanyika!!! kumbe nazo anazihesabu!!! aaha 'Sizitaki mbichi hizi'.

Anazihesabu kwa kuwa zinamuhusu, duh tuzo 30? Kweli jide katishaa
 
mfano mzuri na hauna majigambo dada wengine wangezipata cjui kelele za wao na vyombo ya habari kuwapaisha .ukijishusha mungu atakupandisha! hongera cc*
 
Ahahah binamu sijakuona leo au na wewe ulikuwa airport kumpokea baba ubaya?

Haahahaaha nilitaka niende kumuona baba ubaya live, sema nilikosa nauli binamu. Roho imeniuma kweli kutokumpokea domo, najua nimekikosa kigodoro cha airport

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kumbe huwa anajishaua bure kumbe anazipenda, huyu si ndiye aliuliza kwa dharau kama tuzo za KILI zimefanyika!!! kumbe nazo anazihesabu!!! aaha 'Sizitaki mbichi hizi'.

Kwa hiyo wewe umekasirika kwa alivyozihesabu Tuzo za Kili?
Ova.
 
Back
Top Bottom