Lady Jaydee, huu wimbo wako vipi?

Lady Jaydee, huu wimbo wako vipi?

mito

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2011
Posts
10,682
Reaction score
10,801
Nilikuwa nasikiliza hapa sasa hivi wimbo wa Lady Jaydee Bongo radio, nahisi ni wimbo wake mpya, unless niko nyuma ya wakati. Huu wimbo ni full vichambo kwa aliyekuwa mumewe Gadner, manake anavyoelezea jamaa alivyobize kujaza vimwana mimba huku yeye Lady Jaydee akidhani ni wake peke yake, kumbe anatunzia wengine loh!

Mwenye huu wimbo tafadhali naomba aniwekee hapa niusikilize tena kwa makini, manake nilishikwa na butwaa sana nilivyousikiliza kwa mara yangu ya kwanza bongo radio.

CC atoto, Heaven on Earth, Diva Beyonce, data, Mokoyo, Matola, Dinazarde na wengine plz
 
Wimbo unaitwaje? Hebu weka nyama kwenye mada yako maana najua jide ana wimbo na mdada wa kenya kama sijakosea na una video..
 
Huo ni wimbo gani wa Jide, ka bado anamuimba gadna basi ujue kamu miss ex_ wake huyo.
Huwa nashangaa wasanii wabongo wameachana still ana mwimba mwenzangu. Hawajui maana ya Ku move on.
 
Mkuu nimeusikiliza tu kwenye redio leo hii, hawakusema unaitwaje, ila obvious siyo huo wa mdada wa kenya, coz kwa mtu aliyefuatilia sakata la ndoa yao ukiusikia tu unajua moja kwa moja anamsema Gadner, hasa madai kwamba jamaa alikuwa anatusua vimwana balaa na kuwajaza mimba
 
Hakika sijawai kusikia wimbo kama huo!
 
Huo ni wimbo gani wa Jide, ka bado anamuimba gadna basi ujue kamu miss ex_ wake huyo.
Huwa nashangaa wasanii wabongo wameachana still ana mwimba mwenzangu. Hawajui maana ya Ku move on.
Jide ana shida kubwa sana tena sana!
 
Jide ana shida kubwa sana tena sana!

Ila sijapenda alivyomsema jamaa, kaonyesha utoto na kisasi. Kwangu mimi naona wimbo wenyewe ni dhahiri kautunga mahususi kumsema jamaa, manake hauna ule ubora wa nyimbo zake nilizozizoea, i don't see professionalism in this song zaidi ya vichambo
 
Natamani niusikilize kwanza ili nipate uwanja wa kumjadili vyema...ngoja niutafute...! Jide ana tatizo
...
 
Ndo ubabe wenyewe huo na kisasi mbona tangu wameachana Gadna ame mind bussness zangu.
Kumsema vibaya ex wako kwenye nyimbo ni utoto flani hivi watu walio share bed.
 
Gadna alikua ana msaidia sana kwenye mambo yake mengi, tu Jide anaonyesha ni mbabe flani hivi asiye shaurika. Atamkumba tu Gadna
Pamoja na madhaifu ya G lakini alikuwa ana mchango mkubwa sana kwenye muziki wa Jide!
Jide kaporomoka sana kimziki baada ya kuachana na G!
Yani sasa hivi utafikiri afanyi muziki kabisa na wala haeleweki kabisa!
 
Natamani niusikilize kwanza ili nipate uwanja wa kumjadili vyema...ngoja niutafute...! Jide ana tatizo
...

Mkuu ukiupata tafadhali tuwekee hapa kwa kutumention kabisa ili tuje fasta
 
Pamoja na madhaifu ya G lakini alikuwa ana mchango mkubwa sana kwenye muziki wa Jide!
Jide kaporomoka sana kimziki baada ya kuachana na G!
Yani sasa hivi utafikiri afanyi muziki kabisa na wala haeleweki kabisa!
Na sidhani ka Jide alikua that perfect ukute aliyokua anafanya Gadna na Jide naye alikua anafanya kisiri mana inaonyesha ni silent killer.
Hasa kipindi kile cha bifu na Ruge Gadna ilibidi am support kwa kila jambo. But licha ya madhaifu mama aligoma kujishusha for the sake of her Bussiness.
 
Nilikuwa nasikiliza hapa sasa hivi wimbo wa Lady Jaydee Bongo radio, nahisi ni wimbo wake mpya, unless niko nyuma ya wakati. Huu wimbo ni full vichambo kwa aliyekuwa mumewe Gadner, manake anavyoelezea jamaa alivyobize kujaza vimwana mimba huku yeye Lady Jaydee akidhani ni wake peke yake, kumbe anatunzia wengine loh!!

Mwenye huu wimbo tafadhali naomba aniwekee hapa niusikilize tena kwa makini, manake nilishikwa na butwaa sana nilivyousikiliza kwa mara yangu ya kwanza bongo radio.

CC atoto, Heaven on Earth, Diva Beyonce, data, Mokoyo, Matola, Dinazarde na wengine plz

wewe utakua unazungumzia wimbo wake na Avril ambao alioshatamka kwamba yeye ameandikiwa mashairi na Avril na kupewa tu aimbe haku husika na uandishi wa lyrics..kitendo cha kumuhusisha kila ngoma na madongo kwa G sidhani kama ni busara!
 
Mkuu, mbona umeandika mcharazo mana pamoja na kununua miwani mpya ili nisome ulichoandika nimeshindwa kabisa kusoma......
Wewe utakua "daktari" mtoto....
Uandisha huo huwa una kera sana..
 
Back
Top Bottom