Lady Jaydee: Mashabiki wa mikoani hamuoneshi ushirikiano ndiyo maana mikoa mingine siji kufanya show

Decree Holder

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2015
Posts
2,559
Reaction score
3,745
Watu wa mikoani malalamiko yenu nimeyasikia ila na mimi nina ya kwangu pia naomba myasikilize kwa umakini ili tuweze kwenda Sawa .
——————————————————————————————————————————————————————
Ukitoa Mwanza, Dodoma , Arusha , Geita na Mtwara kidogo muitikio wenu huwa unakuwa mdogo sana kwenye shows hii inakatisha tamaa kuwatembelea ——————————————————————————————————————————————————————
Pili mna kasumba ya kusema hamuamini kama msanii amefika hadi apitishwe kwenye PA awapungie mkono kama mbunge anaomba kura jimboni |
Radio zipo, TV zipo na simu mnazo za mkononi hiyo ni njia nzuri ya kutumia pamoja na vipeperushi|
Binafsi mambo ya kupita na kupunga mkono siyapendi hata kidogo na nikiitwa na promoter kitu cha kwanza namwambia hakikisha umefanya matangazo watu wameelewa otherwise sitaki mambo ya PA ——————————————————————————————————————————————————————
Hizi ni Zama za PA kweli jama ??
Na kisingizio huwa flani alitangazwa anakuja hakuja
Binadamu wote si Sawa, na tusihukumiwe kwa makosa ya watu wengine ambayo hayatuhusu
——————————————————————————————————————————————————————
Tatu , wengi wakifika mlangoni wanaomba kupunguziwa bei ya kiingilio [emoji134][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
Mtu anapoandaa shughuli ya kuwaburudisha mjue ameshapiga mahesabu kajua amegharamia kiasi gani na anataka gharama zake zirudi na apate faida pia , na nyie pia hapo hapo awape burudani |
Tujitahidi kuwa waelewa na kwenda na wakati ili kuepusha kero ndogo ndogo pamoja na malalamishi |
Ndio mwisho wa siku unajikuta mtu unarudi mikoa ile ile ambayo watu wanajitokeza na kuelewa |
Asanteni kwa mapenzi mema |
Ila Dodoma nitarudi very soon , sijui mmeniloga ‍♀️‍♀️ Ila pia huwa nafata Nyomi [emoji3][emoji3][emoji3]
——————————————————————————————————————————————————————
Halafu katika wasanii ambao hawabagui crowd ni mimi, maana JayDee ni wa watu wote wale Classy wa Serena na hata masela wangu vilevile.
Kwahiyo hajatengwa mtu wala nini |
Sehemu nilizowahi kupita nyie ni mashahidi kuwa nishafika hadi vijijini mwenu na kulala sehemu yoyote ile bila kujitia u star |
Mimi ni mtu humble sana , ila tu nina misimamo yangu pia .
 
Kaanzisha bifu na watu wa mikoani. Akifa msimzike.
 
Naona amewatenga wa kanda ya Ziwa wenzie. Sisi wa pwani tuacheni na wakina mwana FA wetu
 
Dalili za kuvimbiwa huwa ni kutoa Pungent smell from the shithole..,
Nadhani Jide hakunyimwa Kunde!!!
 
Mhenga naona anaanza kupoteza kumbukumbu sasa! We sie ndie komando bint machozi ulokuwa hupokei simu za mapromota enzi zile una mbeleko ya Mr Kusaga? Mikoani wanataka we wakuone kwenye PA ili waone tu ni nn kilimvutia G habbash afu wasije hata kwenye show husika!! Nenda tu Dodoma wanakoambiwa wao ndo mji mkuu huku hawapo hata kwenye big four
 
I like jay dee so much, I wish I could have her number just I can hear her voice directly talking to me...... I have her message.
 
Kabisa halafu kajishtukia maana huwa wanaona wa mikoani washamba,juzi juzi tu hapa iliandaliwa show sijui mara au geita msanii aslay hakutokea kwa muda muafaka wakati watu walilipa kiingilio na matangazo juu kuwa atakuwepo. Jamaa kuja kachelewa anajitetea ndege ilichelewa kuondoka. Yaan kwa ulafi alichukua pesa za show mbili za siku moja akitegemea akimaliza ile moja atapanda ndege kuja kupiga nyingine mkoa mwingine.

Jide alikua na uongozi mzuri chini ya mkojozaji
Amekosea sana kuanzisha bifu na wa mikoani, badala ya kuja na strategies za nini afanye ili kuwavutia wapenzi wa mikoani kwenye show zake kaamua kumwaga sumu!!!
 
huu pia ni ujumbe kwake...sisi wa mikoani hatuendi kumuangalia mtu asiye na mvuto jukwaani...kucheza hujui unaimbaimba tu...tuje tukuone wa nini......bora tusikilize redio...so far hata audio zako hatusikilizi tunakujaje kwenye show yako.......pambana tu na hali yako
 
Uzee mbaya sana ndugu zangu .. jaydee ndio hivyo tena keshagota anakimbiwa na wanaume hadi mashabiki hajui afanye nini na aseme na muda gani..ama kweli wakati ukuta
 
huyu bibi watu bado mnalipa kiingilio kwenda kumuona , mikoani anaitwa mfupa na ngozi.
 
Pole yake, kama ni maharage yameshachacha tayari, keshafulia, asitafute umaarufu mpya kwa kuwaponda mashabiki wake, ameshachelewa, na sisi hatuna haja nae, akae huko huko aliko.
 
Duh!Naona yule jamaa aliyemuanzishia uzi wa majibu ya hovyo alikuwa sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…