Lady Jaydee: Nilikuwa mwizi wa simu, sio hela..

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Msanii Lady Jaydee ameamua kufunguka jinsi alivyoanza harakati zake za kuingia kwenye muziki enzi hizo.

Akiandika mtiririko wa matukio kwa kadri ya kumbukumbu zake, amejikuta akikumbuka tukio la kuiba simu ya baba yake mdogo ili kupiga Radio One kwenye kipindi cha 'DJ Show' ambako kulikuwa na mashindano ya kusaka vipaji vya kuimba alikoibuka mshindi hapo baadae.


"Nilipata offer ya kurekodi wimbo wa kwanza baada ya kushinda shindano la Vipaji Halisi. Unapiga simu Radio One Stereo unaimba au ku rap kipindi “DJ Show” na Mike Mhagama. Na hapo ndio niliposikika rasmi. Sikuwa na pesa ya Studio ya kumlipa Master Jay", anaanza kusimulia Jide kupitia mtandao wa Twitter.

"Na nyimbo zilizonipa ushindi ni Keep On wa Mc Lyte, Stranded wa Lutricia McNeal na Gotta get you home wa Foxy Brown. Kulikuwa na awamu mbalimbali. Nikafanikiwa kuingia Top 3 na baada ya hapo kuibuka kidedea mshindi wa kwanza. Shukrani sana kwa Mike Mhagama" anaendelea kufunguka msanii huyo bora wa kike kwa nyakati zote katika tasnia ya muziki nchini.

"Kipindi hicho nilikuwa nafanya muziki just for fun tu, nothing serious. Nilikuwa naiba simu nyumbani kwa baba yangu mdogo ambapo nilikuwa naishi kipindi hicho ilipogundulika kuwa naiba simu kupiga radio eti naimba nilikula kibano pia. Ila sijutii wala nini".

"..Atleast sikuwa naiba pesa, nilikuwa naiba simu" anachombeza Komando kwa utani na kicheko juu.

"Kwa leo tuishie hapa. Story itaendelea siku nyingine kwa maombi maalum au kwa mapenzi yangu binafsi. Shukrani" amemalizia hivyo Lady Jaydee.

My take: Sikuwa nafahamu kwamba Jide alipata nafasi ya kwanza pale Radio One kutoka kwa kaka mkubwa Mike Mhagama (jamaa alikuwa peace sana huyu kwa wakongwe wenzangu mnaomkumbuka). Siku zote najua alianzia Clouds Media moja kwa moja.

NB: Akiendelea nitakuja kuweka hapa.
 
Binafsi nilivyo elewa kwamba Mike mhagama aligundua kipaji chake
Lakin clouds waliendeleza nakumkuza zaidi mpaka akawa jide huyu tunaye mjua

NB:"kipindi jide anatoka nilikuwa mdogo sana nimemjua ukubwani tuu!.
 
Binafsi nilivyo elewa kwamba Mike mhagama aligundua kipaji chake
Lakin clouds waliendeleza nakumkuza zaidi mpaka akawa jide huyu tunaye mjua

NB:"kipindi jide anatoka nilikuwa mdogo sana nimemjua ukubwani tuu!.
Nami naona ni hivyo pia mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…