Lagos, Nigeria yakabiliwa na wimbi kubwa la ombaomba wa mabavu.

Lagos, Nigeria yakabiliwa na wimbi kubwa la ombaomba wa mabavu.

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Wakazi wa Lagos wana malalamiko makubwa baada ya jiji hilo kukabiiliwa na wimbi kubwa la kundi ombaomba wa pesa wanaolazimisha watu kuwapa pesa.

Raia mmoja wa Lagos ameandika ushuhuda wake akisema;

Lagos siku hizi kunakera sana, maana niambieni kwa nini...

Nilikuwa kwenye safari yangu ya kawaida ya jioni. Nikasimamisha gari pembeni ya duka ili kuagiza kitu. Nilipokuwa narudi kuelekea kwenye gari langu, huyu jamaa akaniona nikielekea kuingia garini.

Akanisogelea na kusema, "Abeg, nipe kitu nile. Nina jeraha kwenye mguu."

Nikajifanya kama sijamsikia. Kisha akarudia tena, lakini safari hii kwa sauti ya ukali zaidi:

"Nipe kitu basi. Unaona jinsi ninavyotembea? Nina jeraha kwenye mguu na nataka kula."

Mawazo yangu ya kwanza yalikuwa, "Hii ni wazimu au nini? Huyu ana ujasiri wa aina gani?"

Alikuwa ameshika fimbo. Niliona jinsi alivyokuwa akiihamisha kutoka mkono mmoja kwenda mwingine, nami nikainama taratibu ili pia nijitayarishe kushika "kifaa changu cha amani."

Nafikiri aliona nilichofanya, akasogea nyuma kidogo kabla ya kuanza kuondoka.

Jilindeni mnapokuwa mkizunguka Lagos siku hizi.

Watu hawa sasa wana ujasiri mkubwa sana, na hawaonekani kujali madhara wanayoweza kusababisha.
 
Nigeria niwasaka hela wao hawachagui njia ya kupiga pesa
 
Hao sio omba omba, ni Matapeli walio changamka. Lol
 
Hao bado sana kwa panya road &co. Vyombo vyao vya usalama wakajifunze Bongo - siku mbili tu jiji litakuwa shwari hilo.
 
Back
Top Bottom