Laila, jini aliyenifundisha mapenzi nikiwa shule

Kuna siku tumeenda matembezi, tukaona tufike soko la kilombero kununu matunda, kama kawaida mke wangu kavaa baibui na mtandio juu. Kwenye daladala konda alikuwa amelewa, akawa anatukana hovyo. Nikiwa natoa nauli nimpe akafoka we jombaa acha kulala, toa nauli fasta, au kwa kuwa uko na rangi ya mtume .

Basi Laila akanizuia nisitoe hela, kwa macho yangu nikamuona ananyosha mkona na kumsukuma akajipiga kwenye chuma (wengine wote waliona ni gari imeyumba ndio maana kajigonga.) kisha nikamuona anamsachi na kuchukua hela zote bila kondakta kujua lolote, tukashuka. Cha ajabu gari haikuwaka tena pale kituoni, watu wakashuka ilikuwa mianzini kituo cha kwanza.

Laila akaanza kunionyesha uwezo wake, anachukua kitu chochote dukani akitaka na hakuna mtu anamuona. Nikaanza kuona maumbo yake tofauti tofauti, ila sio ya kutisha.

Nikiwa nimechoka kukaa tu home bila kazi, nikapata wazo niende manyara, kuna baba mdogo ni mkuu wa CID mkoa nikaongee nae nione kama nitapata kazi (nina cheti cha darasa la 7 tu). Nikaagana na Laila, safari ikaanza. Nakumbuka nilipanda Mtei mpaka manyara. Kufika pale nikatafuta kituo cha polisi nikaonyeshwa, fika polisi nikaomba kuionana na mkuu wa CID, nikaulizwa mimi ni nani, nikawajibu huyo ni baba mdogo.

Nilipelekwa kwa heshima sana mpaka ofisini kwake, baada ya salamu, nikaulizwa shida nilaeleza. Mzee akanitolea uvivu, rudi dar ukasome hakuna kazi utapata, kibaya zaidi kabla sijaongea lolote akamuita Pc na kumwagiza anipeleke kwa polisi walioko pale stand wanitafutie usafiri nirudi Arusha. Huo ukawa mwisho wa kuwaza kazi kupitia huyo mzee, hata hela ya maji hakutoa.

****
Nikiwa Arusha nikaanza kutafuta namna ya kumkimbia Laila, sababu hasa ni kuniwekea visheria vingi sana, halafu yeye ana uhuru wa kutoka hata bila kuaga ila mimi ni mpaka nimpe taarifa. Laila aliendelea kutembea na jamaa mmoja anaitwa Samson alikuwa dereva wa leopard tour. Ilifika kipindi akawa anamfata hapo home ila anaishia kwenye gari tu.

Penzi lao likakolea sana, jamaa akamwambia anataka amuoe. Na mimi kipindi hicho nikawa napata msukumo moyoni wa kumtoroka. Nikapata wazo nimwambie naenda nyumbani kusalimia mama na kuandaa mazingira ya kumpeleke, akaniruhusu bila shida. Nikaondoka Arusha kwenda kijijini kwetu (huo ni mwezi wa 9 paper la form 4 limeiva na mimi niliacha shule). Nikawaza ili ndugu wanipokee na kunisaidia, natakiwa nitafute mbinu ya kufanya.

Kufika home mama alifurahi sana maana tangu nitoroke Dar hakuna mtu alikuwa anajua niko wapi na nina hali gani. Ikabidi nitumie mwanya huo huo kutafuta sympathy, nikamwambia nimerogwa na pia nilichukuliwa toka kwa kaka kimiujiza mpaka Arusha. Kumbe kaka alimshirikisha mfanyakazi mwenzake swala langu, akashauliwa waende kwa mganga. Kufika kwa mtaalamu pale manzese wakaambiwa nimetupiwa jini ndilo limenitorosha. Kaka akakumbuka na maneno aliyoambiwa na Laila siku ile, wakaamini nilichukuliwa na majini.

Basi mama akawasiliana na kaka, kaka akaambiwa na yule mfanyakazi mwenzake kuwa kuna mtaalamu anapatikana Isbania Kenya, huyo ni mwisho wa matatizo (alikuwa ni mwenyeji wa sehemu moja inaaitwa Sirari) . Safari ya kuelekea Isbania ikaanza, tukafika jioni tukiwa na mama. Mama anaonana na mtaalamu, tukaambiwa nimependwa na majini, ndiyo yameniondoa shule, kwa hiyo yeye ana uwezo wa kuyafukuza.

Akataka laki 3 ya Tanzania akalipwa nusu, nikaambiwa nikae pale siku 7 anifanyie dawa. Basi mama akaondoka kesho yake ila akatakiwa kurudi baada ya siku 2 ili wakati nafanyiwa dawa awepo na ilitakiwa aje na pesa zote zilizobaki, nikabaki kwa mtaalamu. Siku ya kufanyiwa dawa, nikashuhudia usanii mkubwa unafanyika pale, ila kila nilipojaribu kuongea na mama kuwa tunaibiwa tu hapa, akanijibu ni hayo majini yananidanganya ili niondoke pale[emoji22]

Usanii wa mtaalamu

Akapandisha mizimu yake ya uongo na kweli, kilichonifanya nisimuamini 100% ni kuona anatumia vitabu vya dini. Akipandisha majini anatumia qur'an na akipandisha mizimu anatumua biblia.

Mtaalamu: Baba daudi, baba ibrahim, baba isaka, baba yakobo……. anaeleza shida zake huku amefungua biblia upande wa zaburi.

Matibabu

Mtaalamu akachukua beseni, akajaza maji na kuweka sabunu ya unga, akavaa kanzu yeye nikono mirefu na mipana. Akaanza kuvuruga sabuni kwenye maji huku anaimba kwa lugha isiyoeleweka. Baada ya muda nikamuona anafanya kama anajikuna lakini mikono iko ndani ya maji, hatimae akatoa ka chupa ka plastic kamechoka, ndani yake kuna vitu. Kuangalia vizuri naona nywele, vitamba, udongo nk, akasema akili zangu ziliwekwa kwenye ile chupa na huyo alienitumia hayo majini. Imebidi aifate hiyo chupa kule ilikokuwa umefukiwa (sehemu moja inaitwa msomela Bagamoyo)

Nilichogundua ile chupa aliibana na kitu kama rubber band mkononi, alipokua anajikuna ndio aliifungu na kuangukia kwenye disha la povu.

Basi tukaambiwa kazi imeisha, natakiwa niogee dawa alizonipa kwa siku 7, ila hirizi nikagoma, wakalazimisha nikaichukua kufika njiani nikaitupa kichakani. Tukaodoka mpaka sehemu moja inaitwa Tarime tukalala hapo, kesho yake tukaanza safari ya kurudi nyumbani.

Usiku wake Laila akaja ndotoni akiwa amekasirika sana, akaniambia hatanisamehe, nitajuta kwa kuvunja ahadi. Nikamwambia mama, yule jini kanifata usiku, akaogopa sana. Ikabidi awasiliane na kaka, kaka akasema ameambiwa kuna mtaalamu wa majini anapatika manzese, niende tutapata ufumbuzi.

Safari ya kwenda Dar ikaanza, nakumbuka tulipanda gari inaitwa 'takrimu' kama sijakosea, zilikuwa zinazungukia Nairobi then Arusha to Dar. Kufia Dar tukaenda kwa huyo mtaalamu, he was very smart kidogo, sikugundua uongo wa wazi, ali- generalise tu using common sense.

Akachinja kuku, baada tu ya kumkata shingo, akamwachia, kisha kuku akawa anatapa tapa halafu akageukia upande wa mashariki akatulia, mtaalamu akasema tayari amepindua meza[emoji3]. Nikapewa dawa za kuogea, tukaondoka.

Safari zote za kwenda kwa wa mtaalamu ni kutafuta sympathy tu kwa kaka ili anipe third chance nimalize shule. Kila nilipokuwa nawaambia tunadanganywa naonekana ni yule jini ananituma. Lakini ukweli ni kwamba Laila hakuwa tatizo kwangu, nilipoondoka Arusha nilitafuta bangi na mfupa wa nguruwe nikawa natembea navyo mfukoni. (katika kutafuta msaada wa kimawazo kuna mzee aliniambia nikifanya yale ambayo majni hawayapendi atanichukia na kuondoka). Hivyo vitu vilimfanya aache kuja live, ila anakuja ndotoni.

Nakumbuka Laila aliniambia nisinywe pombe, nikaanza kunywa japo homu walijua ni stress ila mimi nilijitahidi ninuke pombe muda wote, nikawa mlaji mzuri wa kitimoto nakambare, nikawa mhuni wa kutupwa, silali bila apple kuliwa.

Yote haya nilifanya kama tiba ya kumuepuka Laila, ila kuna jambo moja nilichelewa kulijua, connection ya mimi na Laila ilikuwa kupitia marashi flani aliyokuwa ananiletea kila mara. Pia kulikuwa na chupa ndogo ndani kuna maji kama mercury hivi, hicho kichupa kilikuwa sealed ila ukikishika unayasikia marashi ya ndani.

Hii ilikuwa kama key holder kwa hiyo nikawa nayo muda wote kumbe ni airport ya Laila. Mpaka kipindi hiki Laila hakunitokea live, bali ndotoni akiwa na maumbo ya kutisha sana. Wanawake niliokuwa natembea nao walikuwa wanapata changamoto ya kuharibu mizunguko yao ya mwezi, wengine maumivu ya tumbo nk lakini sikuthubutu kuwaambia chanzo ni mimi.

*******
Nikamuomba kaka anilipie nikafanye mtihani kama PC, baada ya maandalizi hatiamae nikafanya mtihani kama PC pale Biafra high school. Matoke yalipotoka nikapata Division 3 ya mwisho, kaka akataka niende chuo. Binafsi niliona nimechezea sana muda, kwanza nimerudia darasa, pili sikufanya paper na wenzangu. By that time wao wanaingia form six, nikamwambia kaka hapa natafuta kazi kisha nitajisomesha, japo aligoma ila nikakaza akaniruhusu.

Nilipopata cheti, nikaanza michakato ya ualimu au jeshi (utaratibu wa kwa mujibu wa sheria ulikuwa bado haujarudishwa). Katika mizunguko nikakutana na mwalimu wangu wa shule ya jeshi ya mwanzo, nilimuacha akiwa luten. Baada ya mipango mingi na rushwa,kukimbizwa kuzunguka kiwanja, hatiamae nikatoboa usahili wa mkoa, nikapangiwa Jkt mlale- Ruvuma.

NB: Kuna siri nyingi sana nimeacha nilizoambiwa na kufundishwa na Laila, halikuwa lengo la thread, maybe wakati mwingine.

Ilinichukua miaka miwili kufanikiwa kumfukuza kabisa Laila. Huenda siku moja nikaeleza mapabano yaliyotokea na vituko alivyonifanyia nikiwa mlale, mpaka siku nakuwa huru.
*****

Baada ya ku report tu kambini, nikaanza maisha mapya yenye furaha na amani, leo hii nikijitathimini nimepiga hatua kuwazidi baadhi ya wale classmates. Nina heshima kwa jamii yangu.

Moral of the story.

Kwenye maisha, hakuna kuchelewa wala kuwahi, hapa kuna hatua unazoweza kuchukua:

Badili mtazamo: Badala ya kujikazania mawazo ya kuchelewa, jaribu kubadili mtazamo na kuona fursa zilizopo mbele yako. Jifunze kutazama kuchelewa kama nafasi ya kujifunza na kuboresha mbinu zako. Kumbuka kuwa mafanikio ni safari ya muda mrefu na hakuna wakati uliochelewa sana kuanza.

Weka malengo mapya: Jipange upya na kuweka malengo mapya. Fikiria ni malengo gani unayotaka kufikia na jifunze kutoka kwenye muda uliopita uliochukuliwa kufikia malengo hayo. Weka malengo yanayopimika, yenye muda uliowekwa na hatua za kufikia malengo hayo.

Jifunze kutoka kwa wengine: Tafuta watu ambao wamefanikiwa katika eneo lako na uombe ushauri na mwongozo. Jiunge na jumuiya za watu wenye malengo kama yako na ufanye mazungumzo na watu wenye uzoefu. Unaweza kujifunza kutoka kwa mafanikio na changamoto zao na kutumia maarifa hayo kuendelea mbele.

Kubali mchakato: Kumbuka kuwa mafanikio mara nyingi yanachukua muda na juhudi. Kubali kuwa mchakato wa kufanikiwa unaweza kuwa na vikwazo na changamoto, na ni sehemu ya safari yako ya kibinafsi. Kuwa na subira na uzingatie maendeleo kidogo unayopata kila siku.
****
[emoji3578]cotterpin.
Jini malaya sio? [emoji23][emoji23]
 
Afande cotterpin salute kwako mike

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom