Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 16,908
- 19,123
Dodoma. Serikali ya Tanzania imefungia laini za simu 18,622 baada ya kubainika kufanya matukio ya uhalifu nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndungulile leo Jumatano Julai 28 2021 wakati akifungua mkutano wa mapato na matumizi wa wizara na taasisi zake.
Amesema kuwa laini hizo ziligundulika katika kipindi cha kati ya Aprili hadi Juni mwaka huu na kuwataka Watanzania kuhakiki usajili wa laini zao.
“Tumevizuia vitambulisho vilivyotumika kusajilia laini 14,768, ndio maana niwaombe sana Watanzania tuendelee kufanya uhakiki wa laini zetu ili hayo yasije yakajitokeza,”amesema.
Amesema watu wamekuwa wakisajiliana laini za simu kwa kutumia vitambusho vya wengine.
Chanzo: Mwanainchi