Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Ni wazi matatizo yanayoikumbuka Tanzania kwa sasa ni matokeo ya Hayati Magufuli kuufifisha upinzani huku aliamini ni salama kwake hadi hapo angemaliza Utawala wake pasiwepo wa kumsumbua. ALIJIDANGANYA!
Hayati Magufuli pamoja na mazuri yote aliyopata kuyafanya lakini hilo la kuufifisha upinzani na kuunyima fursa ya kuwamo Bungeni hakika kwalo ndilo pungufu na udhaifuye mkubwa na ambao lazima aujutie hata huko alipo.
Leo hii kwa mfano laiti Bungeni wangekuwapo wabunge mfano wa Joseph Mbilinyi hakika hicho kiburi cha wanaojiita CCM yenyewe akina Makamba na Nape hakika kisingekuwepo.
Tabu za umeme na gharama za mabando kupanda holela na asiwepo japo Mbunge wa kuhoji seriously ni kwa sababu waliomo wanahofia 2025 kwenye kura za maoni kutemwa na wamebaki kujipendekeza tu.
Haya yote yanatusibu kwa sababu Hayati Magufuli aliamini mfumo wake huku alisahau kuna kufa. Ona sasa tabu tunazozipitia!
Magufuli kwa hilo ulitukosea sana!
R.I.P.