Laki nne inatosha kufungua duka la vipodozi?

All the best mkuu!
 
Ni rahisi sana kwenye makaratasi na jitahidi iwe rahisi kwenye utendaji na ulete mrejesho
 
Itatosha kwa kuanzia kama
Tayari una fremu na umeshalipia kodi walau miezi mitatu
Tayari una vibali
Tayari fremu ina makabati na miundombinu mingine imayoendana na hiyo biashara
Matumizi binafsi hayatatoka hapo
Mzigo wa kuanzia haupo mbali
bila kusahau asitegemee hiyo biashara kumlisha ,kumvisha walau kwa miezi sita ikuwe kwanza
 
Au kanunue perfume za kupima anza na aina nne na usimalize 400k yote nunua hata za 200k tu weka kipimo cha 5k 7k 10k na 25k naandika hivi kwakua kwanza ujazo hazipishani sana na ukapata harufu nzuri nne nahakika unaweza uza muda mfupi ikarudisha hela. Maeneo ya kutembelea ni maofisini vaa vizuri nukia alafu usiongee sana fika eleza mzigo ulionao pita kwenye maofisi binafsi ya serikali na mashuleni Japo kuna shule waalimu hawaruhusiwi kupaka manukato makali ila bado riziki ipo.

Ukimaliza huko sajili whatsapp business kwenye profile weka kama hio biashara ushaifanya sana piga picha nzuri post kwenye profile yako, alafu kila siku usiku post bidhaa zako na chukua hata picha za wadada warembo post andika asante mteja wangu kwa kuniamini na kunukia vizuri lazima utoboe .

usikae kizembe ukiona ukweli hauendi weka na uongo ukisikia kuna event vaa vizuri nenda na mzigo kwenye pochi uza humo humo alafu piga picha sana uwapostie whatsapp na caption za kibiashara lazima utoboe.

Zingatia: hii njia ikakutoa uje uninunulie kitimoto kilo ndizi mbili na coke baridiii kama barafu.😎
 
Mbinu Za kivita hizi siwezi weka hapa

Ilaaa ni very cheap, Kazi yake ni kupamba jina na kutengeneza wateja

Anaweza amua kuanziasha brand yake au akatembelea upepo wa mtu ambae ameshalishika soko
Mfano Wix
Naomba nije PM kwako mkuu
 
Kukopeshaa ni risk,

Nakumbukaa nikiwa 1st yr nilikua nakopeshaa tshet, sendols khaaah mbna nilikua hasaraa,

Nkaahirisha, nkaingia kukopesha vitenge, na madila ila home woiiio kila siku ni story tyuuh.

Kukopeshaa ni hasaraa.
Ndio maana nimemuuliza kama ana roho ngumu, kukopesha na kuchekeana na vitu viwili tofauti.. nimefanya ishu ya kukopesha kwa riba, sio bidhaa ni fedha, hivyo pia nina uzoefu kidogo, biashara ya kukopesha ni uso wa mbuzi hakuna aibu.

Ukicheka na kima, utavuna mabua.
 
Hapo kweli uko sahihi.
 
Hii naenda kuiprint
 
Kukopeshaa ni risk,

Nakumbukaa nikiwa 1st yr nilikua nakopeshaa tshet, sendols khaaah mbna nilikua hasaraa,

Nkaahirisha, nkaingia kukopesha vitenge, na madila ila home woiiio kila siku ni story tyuuh.

Kukopeshaa ni hasaraa.
Waha mbona hawapati hasara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…