Lakini Je, wangapi waliwahi kushitakiwa Mahakamani au hata kufungwa Jela kutokana na Ripoti ya CAG?

Lakini Je, wangapi waliwahi kushitakiwa Mahakamani au hata kufungwa Jela kutokana na Ripoti ya CAG?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hili ni Swali ambalo Watanzania tunapaswa kujiuliza , kwamba kwa miaka mingi ofisi ya CAG imejitahidi sana kuanisha mapungufu , Wizi , upotevu na Uchafu wote unaofanywa kwenye mashirika na idara za serikali , wako walioonyeshewa vidole moja kwa moja ( Wengi wao majina yao yanafahamika )

Lakini kwa miaka yote hiyo hakuna hatua zozote za kisheria zimechukuliwa dhidi ya Watuhumiwa hao wanaofahamika ( niko tayari kusahihishwa ) .

Sisi Wananchi tumeanza kuitilia mashaka Serikali yetu kwamba ripoti ya CAG yaweza kuwa mbinu ya kizamani ya serikali ya ccm ya Kupumbaza wananchi ili waone kwamba serikali yao iko makini , CAG yuko Makini , Takukuru iko Makini , Rais anafokea wezi na mchwa wa Taifa , au Rais Kanuna nk . wakati kwenye ukweli Serikali haina umakini wowote ule , na ndio maana wezi wa Taifa wako kila mwaka na wengi wao baada ya kuharibu mahali pale wanahamishiwa pengine , ama wanapandishwa vyeo .

Sasa kwa kufupisha , Swali langu ni dogo tu , Ni akina nani waliotajwa kwenye ripoti ya CAG ambao waliwahi kushitakiwa Mahakamani au kuhukumiwa kwa Haki ?

FB_IMG_1679994958834.jpg
 
Shida ukaguzi unafanyika kiuhasibu ila report inakuwa presented kisiasa.kumbuka CAG akikukuta huna supporting document ya matumizi yoyote hata kama yamefanyika kihalali utaambiwa umekula hizo pesa.Ndo maana kuchukuliwa hatua sio rahisi.
 
Back
Top Bottom