Lakini Je, wangapi waliwahi kushitakiwa Mahakamani au hata kufungwa Jela kutokana na Ripoti ya CAG?

Lakini Je, wangapi waliwahi kushitakiwa Mahakamani au hata kufungwa Jela kutokana na Ripoti ya CAG?

Shida ukaguzi unafanyika kiuhasibu ila report inakuwa presented kisiasa.kumbuka CAG akikukuta huna supporting document ya matumizi yoyote hata kama yamefanyika kihalali utaambiwa umekula hizo pesa.Ndo maana kuchukuliwa hatua sio rahisi.
Unakosaje supporting document kwenye malipo makubwa kama hayo na wakati kuna softcopy and hardcopy?
 
Shida ukaguzi unafanyika kiuhasibu ila report inakuwa presented kisiasa.kumbuka CAG akikukuta huna supporting document ya matumizi yoyote hata kama yamefanyika kihalali utaambiwa umekula hizo pesa.Ndo maana kuchukuliwa hatua sio rahisi.
Sasa kuna haja gani ya kufoka ?
 
Tatizo kubwa naloliona wengi wanayofanya hayo wanajuana. Unawezaje kumuwajibisha mtu unayemjua?mfano rahisi tu, je mtu kama mwigulu, ummy au nape wanaweza kuwajibishwa? Chukuliaa huo mfano alafu uone jinsi ilivyo ngumu
 
FB_IMG_1665831491154.jpg
 
Ilimkata mzabun wa bil600
Na kuumpa wa tillion1.1
Bila sababu za msingi..daah
Hili samia anahusika nalo maana alisema mchakato wa tende ukishaakamilika watu wasipate shida kukataa rufaa kwa kuwa inachelewesha mradi
 
Swali lako mleta mada ni gumu sana.
Mm nijibu japo kwa juu juu.

Jibu langu ni kwamba CAG anatapanya tu fedha za walipa kodi kwa kulipwa miposho mikubwa na kutumia gharama kubwa ktk uandishi wa mavitabu makubwa na mengi ya ripoti.

Lkn mwisho wa siku hapajawahi kutokea hata mmoja wa hawa mafisadi wakubwa wanaotajwa na ripoti ya CAG akafungwa.
 
Hili ni Swali ambalo Watanzania tunapaswa kujiuliza , kwamba kwa miaka mingi ofisi ya CAG imejitahidi sana kuanisha mapungufu , Wizi , upotevu na Uchafu wote unaofanywa kwenye mashirika na idara za serikali , wako walioonyeshewa vidole moja kwa moja ( Wengi wao majina yao yanafahamika )

Lakini kwa miaka yote hiyo hakuna hatua zozote za kisheria zimechukuliwa dhidi ya Watuhumiwa hao wanaofahamika ( niko tayari kusahihishwa ) .

Sisi Wananchi tumeanza kuitilia mashaka Serikali yetu kwamba ripoti ya CAG yaweza kuwa mbinu ya kizamani ya serikali ya ccm ya Kupumbaza wananchi ili waone kwamba serikali yao iko makini , CAG yuko Makini , Takukuru iko Makini , Rais anafokea wezi na mchwa wa Taifa , au Rais Kanuna nk . wakati kwenye ukweli Serikali haina umakini wowote ule , na ndio maana wezi wa Taifa wako kila mwaka na wengi wao baada ya kuharibu mahali pale wanahamishiwa pengine , ama wanapandishwa vyeo .

Sasa kwa kufupisha , Swali langu ni dogo tu , Ni akina nani waliotajwa kwenye ripoti ya CAG ambao waliwahi kushitakiwa Mahakamani au kuhukumiwa kwa Haki ?

Sjawah mm kuskia aiseeee, hio report sometime inakuwaga kama imekaa kimbea mbea
 
Ile stupid kuwalaghai tu wananchi, muone kachukia wakikutana huko wanagonga cheer's.
Angekuwa amekasirishwa kweli, angewataja pale, kuwatengua na hatua nyingine za kushtakiwa zingefuata.
Ila ni kama miaka yote life goes On...
 
Ilimkata mzabun wa bil600
Na kuumpa wa tillion1.1
Bila sababu za msingi..daah
Tumekwisha washtaki kwa "mungu". hapana, niseme "TUMEWATISHIA" na "mungu".

Tena mshtaki ni mkuu wa nchi, wewe unadhani hiyo ni kazi ndogo?

Sasa tunasubiri waliotishiwa 'mungu' watafanya nini.
 
Shida ukaguzi unafanyika kiuhasibu ila report inakuwa presented kisiasa.kumbuka CAG akikukuta huna supporting document ya matumizi yoyote hata kama yamefanyika kihalali utaambiwa umekula hizo pesa.Ndo maana kuchukuliwa hatua sio rahisi.
Eee,Bhwanah!

Hebu tueleze wewe mtaalam kuhusu ile hela ya ndege, au hizi tenda za gharama ya chini kukataliwa na kuchuliwa ile ya aghali zaidi.
Hebu tueleze hilo nalo linakuwaje. Tupo tayari kujifunza toka kwako mkuu!
 
Nachoshangaa CAG anaendeleaje na kazi wakati maoni yake ayatekelezwi?

Kama kuajibika si ajiuzuru
 
Hakuna consequences zozote.

Rais kasema mkimkamata mwizi na mkakuta taratibu zenu za utumishi haziruhusu kumchukulia hatua basi mhamishieni kwenye kitengo ambacho hakina hela. Sasa kwa nini mkuu wa nchi asihoji, asizipinge na kuzibadilisha kanuni za utumishi zinazomlinda mwizi ?

Yeye huyo huyo jana hiyo hiyo katukana watu walioshindwa kuhoji vitu vya dhahiri visivyoingia akilini vinavyoliumiza Taifa kwamba ni watu stupid! Akarudia tena kusema hii mijitu pumbaav. Halafu yeye huyo huyo kashindwa kuyahoji haya ya kanuni za utumishi zinazosema mwajiriwa wa umma ana kinga ya kudumu.
 
Back
Top Bottom