Hizo mashine hazina mfano mkuu, halafu sahivi kuna zile exclusively kwa ajili ya watalii kuna kampuni moja iko Arusha walianza kuziundia body kinyemela na kuzifanya warbus kwa ajili ya kubebea watalii kabla mjapani hajawashtukia ikabidi awape leseni ya kuziunda for Africa. Ziko njema sana hizo cruiser ni gari ya maisha ukiwa nayo.Land cruiser 78s ni gari ya karne.
Hata Mimi mkuu hio 100 ninaihusudu n kuitamani sana ntaitia mkononi one dayila naona design kali ilikuwa ya 80 series na 100 series wadau, ni vile sijapata hizo penenge ila lazma ntakamata moja hasa 100 series respect
sema land cruiser 200 zinaboa hazina ile feel ya off road 4x4 halafu engine hata haina muito mzuri kama za 100 ama 80 series, pia mkunjo wa body umekaa kinyanya sana, at least hii facelift ya 2016 ipo na mvuto zaidi
mi nazikubali sana especially engine inavyoitika, hebu iskilizie apo
Duh! wewe mshikaji halafu unavyoandika kwa harufi kubwa kumbe haujui unapotosha hapa!
Toyota haijawahi kununua Lexus kama unavyotaka kuaminisha watu hapa bali Lexus ni brand iliyoanzishwa na Toyota ili kutengeneza luxurious version ya Toyota ambayo itashindana na likes za BMW's Audis &Co. na hazijawahi kuwa Kampuni (Toyota na Lexus) mbili tofauti bali Lexus imeanzishwa na Toyota!
Unatataka kununua gari ya aina gani huwo ni uamuzi wako kwa maana pesa ni yako pia lkn mimi nimekupa sababu ya kwanini zinaitwa hivyo yaani for African/EU/US/Japanese market!
Tatizo ni kwamba unaandika tu juu juu lkn hauendi ndani, unaposema ina mapungufu kwenye quality control unamaanisha nini?
Inaelekea unalishwa sana maneno ya vijiweni na wewe unakubali, ngoja nikuulize swali dogo sana unafahamu magari ambayo UN TZ wanatumia? Je unafikiri ni Toyota for European market au Toyota for African market?
Nakujibia swali, UN wote walioko Afrika pmj na Tanzania wanatumia magari ya Toyota yaliyotengenezwa for African market (tropical version), unafahamu ni kwa nini? kama kulingana na msemo wako ni kwamba hayana ubora?
Au unataka kuniambia wewe unaufahamu klk organization kubwa kama UN ambayo ina wataalamu wa kila fani?
Hata Serikali yetu yenyewe hainunui Toyota for EU au US market bali wananunua Toyota for African market (tropical version) sasa unajua ni kwa nini?
Hata ofisi za Kibalozi zote hapa TZ zinazotumia Toyota pmj na Ubalozi wa Ujapani wenyewe hawanunui Toyota zilizotengenezwa for EU au Austarlia market bali wananunua Toyota for African market sasa unajua ni kwa nini?
Ni kwa sababu zimetengenezwa ili ziendane na mazingira ya TZ/Afrika ambapo ni kawaida kwa mfano gari kuingia kwenye maji yanayofunika mpaka boneti hivyo kuna vitu maalumu wanavyoongezea/kupunguza ambavyo hauvihitaji ukiwa Ulaya au Ujapani lkn ukichukuwa BMW X5 ukaenda nayo Tunduru au Serengeti unaweza ukairudisha na umeibeba kwenye tela hiyo ndiyo sababu!
I regret to let u know kwamba Procurement System za nchini kama utawatumia Toyota au CFAO motors wanakuagizia toka nchi wanayojua wao. Ukitaka specific car mfano made for UK au US basi unawaambia na wanakuagizia pia na bei inakua tofauti.
It doesnt mean UN ndo hawatumii haya magari tunayotumia, wazungu ni wanafiki wakubwa sana na wako tayari kutembea na ndala pia wakiwa huku lakini ni bilioneas. I dont see any correlation na mawazo yako kwa kuwasema embassies na UN departments wanatumia magari hayo huku.
Pia unatakiwa kujua Mobilization cost ya miradi huku Africa ipo chini na cost ya wazungu huko kwao so hata magari watanunua ya kimaskini tu
Mfano: Landcruiser 70series wanaleta toka South Africa, Hilux D4D wanatoa South pia.
Na Toyota Japan hawapokei order direct from TZ by kipping Toyota TZ Agent hata kidogo, Pia huwezi kuagiza gari kupitia Toyota Kenya labda utumie 3rd Party kutoka Kenya au nchi yoyote upendayo.
So as long as ukitaka kuagizia gari Toyota unaomba current list ya magari waliyonayo na wanakuagizia wao, hivyo hivyo UN, US Embasy, TZ Gvt na private institution ndo wanafanya.
Halafu hao UN na Embassy wanakua na Amored Cars usitake kusema wataagiza Toyota acha chai wewe.
Lexus ni Toyota hao hao mkuu. Walifanya hivyo ili kupata soko Marekani maana wadhungu toyota hawazimind ni gari ya bei chee. Ilibidi kubadili jina ili auzepo kabei ka kuridhisha. Ila ni wale wale ndugu yanguLC 80 haichuji ina engine 1HZ na nyingine zimefungwa 1HDT cc 4200,fuel consumption nzuri... In short ndio gari ninayo ikubali hapo. Afu kwanini matoleo haya yanarandana na Lexus SUVs!?!?
Ndiyo wanazo bossHii series nao Wana V8?
Mbona unakuwa mbishi na mgumu kuelewa hivyo? Hivi tatizo lako hasa ni nini? Au hapa kigumu kuelewa ni kipi? Ngoja nikuulize swali, ni kwa nini kuna Toyopta land cruiser ya tropical version? Unafahamu ni kwa nini inaitwa hivyo? Usiandike maandishi meengi twende hatua kwa hatua tutakutana tu mahali tuanzie hapo kwanza!