Land cruiser ipi mjapani alitulia kati ya hizi

Yeah mkuu bila shaka unazungumzia 78 series hardtop, siku hizi ndio gari za polisi na ambulance kwa baadhi ya hospitali. Nadhaani maafande wameukubali mziki wake defender sizioni siku hizi.
Injini ya Defender inachoka haraka. Niliwahi kuendesha hiyo Mkonga nje, gari ina Km Laki mbili kwenye dash board lakini ukitekenya stata gari inawaka utazani umetoka kubandua manailoni mda mfupi uliopita... Ile gari ukipewa mpya by the time you are Thirty mbona unazeeka nayo!
 
Tatizo ni kwamba unashindwa kunielewa au labda umeamua kutokunielewa au pia nimeshindwa kujieleza na kueleweka kwako kwa maana kujieleza na kueleweka wkt mwingine nayo siyo kazi rahisi!..

Mkuu me nafikiri unapoint nzuri tu kwamba gari inayokuja Africa inakua haina vitu vingi kama ambazo zinazoenda USA/Europe zinakua navyo,na hio kimsingi inaeffect mpaka kwenye price.

Lakini naomba nikuhakikishie gari iliyotengenezwa kwa ajili ya Africa ni tofauti sana na inayotengenezwa kwa ajili ya wenzetu. Kwa mfano Toyota Harrier na Lexus RX ni gari mbili tofauti kuanzia uzito wa gari,safety, handling , speed na vitu vingine.

Wenzetu safety na handling ya gari ni first priority kabisa.kwenye safety ndio unaongelea uzito wa gari airbags,immobilizer na vingine.Gari za wenzetu zimejaa airbags lkn za Africa airbags zipo mbele tu.

Kama unaangaliaga vipindi vya magari vya wenzetu utaona wanatest gari zao kwenye hill au konakona wakiangalia jinsi handling yake ilivyo na hicho kwa wenzetu ni kitu cha msingi sana, nilishawahi kumiliki Lexus Is200 ya mwaka 2001 na toyota mark x ya mwaka 2006, mkuu handling ya ile lexus huwezi compare kabisa na mark x ingawa mark x ni gari ya kisasa zaidi.ile lexus ilikua ukipita kwenye utelezi inakuwashia taa ya lock diff iligari isiteleze sana yote kwa ajili ya security.

So mkuu nafikiri kama umemiliki au ku test gari hizi zinazotengenezwa kwa ajili ya wenzetu na hizi za kwetu zinakua tofauti sana!
Natumaini nimekuelewesha kitu.
 
Hilo ni kweli kuna ambayo ilinunuliwa mwaka 1990 mzee akiwa kitengo ikawa ndio gari anayotumia akitaka tusafiri kwenda kijiji, alikuja kuuziwa kwa mnada 2000. Mpaka sahizi ninavyo type gari ipo active inapigwa rangi tu na kuwa refreshed na accessories. 78 series is a living legend.
 
naongezea huo u luxury kweny lexus ni mpaka transmision nkimaanisha amna lexus manual zote auto
 
naongezea huo u luxury kweny lexus ni mpaka transmision nkimaanisha amna lexus manual zote auto
Zipo za manual kuna lexus is ndugu yake altezza ni 6 gears manual transmission
 
kuna post cjazielewa huku mnataka sema lexus na toyota are two diffrent things?
 
sammz umegoogle alteza ukasoma wikipedia ndo mana umesema ipo ambayo ni manual ata ukigoogle landcruiser utakuta transmision ni manual na auto ila ukichek lexus yake haina manual same to lexus rx 300 nk
 
Narudia tena unaandika mambo meengi lkn unarudia kile kile ambacho nimekwisha kueleza wewe sijui form ulipata daraja gani kwa maana duh!..

Stop embarrassing yourself. Use google, itakusaidia sana.
 
sammz umegoogle alteza ukasoma wikipedia ndo mana umesema ipo ambayo ni manual ata ukigoogle landcruiser utakuta transmision ni manual na auto ila ukichek lexus yake haina manual same to lexus rx 300 nk
Sio nmegoogle nshaona live kabisa iyo lexus is manual gear sita
 
sammz umegoogle alteza ukasoma wikipedia ndo mana umesema ipo ambayo ni manual ata ukigoogle landcruiser utakuta transmision ni manual na auto ila ukichek lexus yake haina manual same to lexus rx 300 nk

Ur right kaka kuikuta manual ni mpaka mtu mwenyewe kaamua kubadili gearbox system, lakini factory made zote ni Auto
 
kuna post cjazielewa huku mnataka sema lexus na toyota are two diffrent things?

Not really Kampuni ni moja ila matoleo yake ya mwaka mmoja uki compare yana vionjo tofauti na kimoja ulishakitaja which is Transmition.
 
Huu uzi mtamu sana. Naufatilia kwa kila hatua.
 
Not really Kampuni ni moja ila matoleo yake ya mwaka mmoja uki compare yana vionjo tofauti na kimoja ulishakitaja which is Transmition.
Niongezee kidogo tu, Lexus was meant to be a luxury brand ili ipambane na gari za mabara ya ulaya na marekani.
 
Mkuu umekuja na series ila naomba uje na model maana series zinaweza kuwa na engine ya aina moja mfano 1hdt au 1HKZ au 1HKJ sasa hizi model ndizo zinaweza kujua gari ni ipi nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…