Tatizo ni kwamba unashindwa kunielewa au labda umeamua kutokunielewa au pia nimeshindwa kujieleza na kueleweka kwako kwa maana kujieleza na kueleweka wkt mwingine nayo siyo kazi rahisi!..
Mkuu me nafikiri unapoint nzuri tu kwamba gari inayokuja Africa inakua haina vitu vingi kama ambazo zinazoenda USA/Europe zinakua navyo,na hio kimsingi inaeffect mpaka kwenye price.
Lakini naomba nikuhakikishie gari iliyotengenezwa kwa ajili ya Africa ni tofauti sana na inayotengenezwa kwa ajili ya wenzetu. Kwa mfano Toyota Harrier na Lexus RX ni gari mbili tofauti kuanzia uzito wa gari,safety, handling , speed na vitu vingine.
Wenzetu safety na handling ya gari ni first priority kabisa.kwenye safety ndio unaongelea uzito wa gari airbags,immobilizer na vingine.Gari za wenzetu zimejaa airbags lkn za Africa airbags zipo mbele tu.
Kama unaangaliaga vipindi vya magari vya wenzetu utaona wanatest gari zao kwenye hill au konakona wakiangalia jinsi handling yake ilivyo na hicho kwa wenzetu ni kitu cha msingi sana, nilishawahi kumiliki Lexus Is200 ya mwaka 2001 na toyota mark x ya mwaka 2006, mkuu handling ya ile lexus huwezi compare kabisa na mark x ingawa mark x ni gari ya kisasa zaidi.ile lexus ilikua ukipita kwenye utelezi inakuwashia taa ya lock diff iligari isiteleze sana yote kwa ajili ya security.
So mkuu nafikiri kama umemiliki au ku test gari hizi zinazotengenezwa kwa ajili ya wenzetu na hizi za kwetu zinakua tofauti sana!
Natumaini nimekuelewesha kitu.