Land Rover ya Sugal Mohamed iliyomtorosha Nyerere asikamatwe

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MZEE SUGAL MOHAMED ALIVYOMTOROSHA MWALIMU NYERERE ASIKAMATWE NA MAKACHERO
na Guled Issa

Mzee Sugal Mohamed ni moja ya majina ya mashujaa yanayopaswa kuingia katika historia ya mashujaa waliojitolea katika kuwakinga viongozi wa harakati za uhuru wasidhalilishwe na wakoloni wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mfano wa Mzee Sugal ni moja ya mifano mingi ambayo hii leo haifahamiki na wala hakuna juhudi ya kuhifadhi kumbukumbu hizi.

Labda kama ingelikuwa si kisa kilichomkuta yeye na wenzake baada ya uhuru historia hii ya huyu mzee isingelifahamika kamwe.

Kijografia Mzee Sugal Mohamed alikuwa anaishi Arusha kwa sasa ni Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara.

Mzee Sugal alikuwa Mtanganyika mwenye asili ya Kisomali.

Baada ya Tanganyika kujipatia uhuru wake mwaka 1961, Meja Jenerali Muhidini Mfaume Kimario akishika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Ndani kuanzia mwaka 1983 mpaka 1989 katika kipindi chake kama waziri mwenye dhamana alipata kuwanyima amani wazee wa Kiislamu Watanzania wenye asili ya Kisomali katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mtwara na sehemu mbalimbali nchini kwa kuwakamata kila mara.

Jambo la kukamatwa mara kwa mara kwa wazee hawa liliwanyima amani ya kuishi katika makazi yao na baada ya kuchoshwa na kadhia hii ndipo wazee hawa wakakata shauri la kumuendea Mwl Julius Nyerere ili kumfikishia malalamiko yao.

Wazee hawa walipoonana na Nyerere wakamwambia kuwa katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika sote tulikuwa pamoja tukishirikiana kudai uhuru sasa iweje leo baada ya Tanganyika kuwa huru thamani yetu ipotee.

Mzee mmoja katika wazee hao Mzee Sugal Mohamed akamkumbusha Mwalimu mkasa wa yeye kutaka kukamatwa na serikali ya Waingereza wakati wa vuguvugu la kupigania uhuru.

Mzee Sugal akamweleza Nyerere kisa kizima cha kutaka kushikwa na serikali ya Kiingereza mjini Arusha.

Ilikuwa hivi:

''Katika harakati za Tanganyika kupigania uhuru Mwl. Julius Kambarage Nyerere akiwa mjini Arusha, akihamasisha watu kuunga mkono Tanu, kulipatikana taarifa za kutaka kukamatwa Nyerere na serikali ya kikoloni ya Muiingereza.

Mohamed Sugal akamchukua Nyerere kwa gari yake aina ya Land Rover na kutokomea nae mpaka msituni umbali mrefu kutoka mjini ili kuwakwepa makachero wa serikali ya Muingereza.

Inasemekana kulikuwapo na watu wenye magari yao na wangeweza kumsaidia lakini hawakuonesha nia ya kutoa msaada wowote kwa Mwl. Nyerere.

Baada ya kufika msituni Mwl Nyerere alitaka kumlipa Mzee Sugal malipo kama shukrani ya kumuokoa na balaa hilo lakini kitu cha kushangaza kama sio kustaajabisha kwa moyo aliokuwa nao Mzee Sugal akamwambia Nyerere kuwa amefanya msaada ule kama moja ya mchango wake katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Baada ya Nyerere kukumbushwa mkasa huu alisikitika sana kisha akaomba aitwe Waziri wa Mambo ya Ndani Meja Jenerali Muhidini Mfaume Kimario na kuulizwa kuhusu kadhia ya wazee wale.

Mwl. Nyerere alimwambia Meja Jenerali Kimario kuwa kwa kitendo cha kuwasumbua wazee wale si jambo jema, akaongezea kusema kuwa wakati Tanganyika inafanya harakati za kudai uhuru pale Moshi alipokulia Muhidin Kimario walikuwapo majasusi wa wakoloni wakiitumikia serikali ya Kiingereza wakipinga harakati za Tanganyika kuwa huru, hawa wazee wakati huo walichangia mchango wao hadi ikawa sababu ya kupatikana uhuru.

Mwl. Nyerere alitoa amri kusipatikane mtu wa kuwasumbua wale wazee na wapatiwe haki sawa na Watanganyika wengine bila kubaguliwa kwa namna yoyote ile.

Nyerere alimuuliza Mzee Sugal Mohamed kama ile Land Rover yake iliyomuokoa bado ipo, Mzee Sugal akamjibu ipo.

Bila kusita Nyerere alimuomba Mzee Sugal ailete Land Rover yake hiyo ili iwekwe kama kumbukumbu, naye mzee Suagl bila khiyana aliipeleka Land Rover yake hiyo Makao Makuu ya nchi Dodoma na ikahifadhiwa kama kumbukumbu ya uhuru.

Hii ilikuwa ni miaka ya 1988 mpaka 1989.

Mzee Sugal Mohamed alifariki mwaka 1995.

PICHA: Guled Issa akiwa Maktaba na picha ya mwisho ni Meja Jenerali Muhidin Kimario.

Screenshot_20240627-145429_WhatsApp.jpg
Screenshot_20240627-145738_WhatsApp.jpg
 
Kichwa cha huyu Mzee Mohamed Said kimehifahi kumbukumbu nyingi, Serikali ikiweza ione namna ya kumuwezesha atuandikie vitabu vingi vya historia ili Vizazi vijavyo waweze kujifunza
Tatizo serikali inataka Nyerere ndiyo awe the cornerstone of our history. Na hapo ndipo mzee wetu anaposhindwana na serikali

Kuna watu wameplay part kubwa sana kwenye historia ya Tanganyika/Tanzania lakini hawazungumzwi ila mzee Said amekuwa akiwataja sana
 
Ni kweli usemacho Mkuu

Japo nahisi hatuko tayari kuandika

Huyu Mzee pamoja na akina Mzee Butiku wanajua sana matukio ya hii Nchi ila hawapata sapoti ya kuwaruhusu waiandike

Likizo moja nilienda Kijijini, Kuna Wazee wapo Kwenye late 90 wanasimulia matukio mengi sana ya nyuma
 
Nadhani ni muda wa kuachana na kusoma Mfekane war pamoja na Ngoni migration ili tusome historia halisi ya Tanzania yetu 🙌
Ni kweli History ya Tanzania ifumuliwe iandikwe upya "Historia halisi" without bias

Mfano mdogo tu kuna watu kama Bibi Titi Mohammed, Oscar Kambona n.k wanatajwa vibaya katika Historia eti kisa tu walitofautiana ideologies na Mwalimu

Lakini mengi mazuri waliyofanya yenye tija hayazungumzwi au yamezungumziwa kwa kifupi sana lakini ni miongoni mwa mashujaa wa hili taifa
 
Ni kweli History ya Tanzania ifumuliwe iandikwe upya "Historia halisi" without bias

Mfano mdogo tu kuna watu kama Bibi Titi Mohammed, Kambona n.k wanatajwa vibaya katika Historia eti kisa tu walitofautiana ideologies na Mwalimu

Lakini kile walichokifanya chenye tija hakizungumzwi au kinazungumzwa kwa kifupi sana lakini ni miongoni mwa mashujaa wa hili taifa
Naunga mkono hoja, kuanza upya sio Ujinga
 
MZEE SUGAL MOHAMED ALIVYOMTOROSHA MWALIMU NYERERE ASIKAMATWE NA MAKACHERO
na Guled Issa

Mzee Sugal Mohamed ni moja ya majina ya mashujaa yanayopaswa kuingia katika historia ya mashujaa waliojitolea katika kuwakinga viongozi wa harakati za uhuru wasidhalilishwe na wakoloni wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mfano wa Mzee Sugal ni moja ya mifano mingi ambayo hii leo haifahamiki na wala hakuna juhudi ya kuhifadhi kumbukumbu hizi.

Labda kama ingelikuwa si kisa kilichomkuta yeye na wenzake baada ya uhuru historia hii ya huyu mzee isingelifahamika kamwe.

Kijografia Mzee Sugal Mohamed alikuwa anaishi Arusha kwa sasa ni Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara.

Mzee Sugal alikuwa Mtanganyika mwenye asili ya Kisomali.

Baada ya Tanganyika kujipatia uhuru wake mwaka 1961, Meja Jenerali Muhidini Mfaume Kimario akishika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Ndani kuanzia mwaka 1983 mpaka 1989 katika kipindi chake kama waziri mwenye dhamana alipata kuwanyima amani wazee wa Kiislamu Watanzania wenye asili ya Kisomali katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mtwara na sehemu mbalimbali nchini kwa kuwakamata kila mara.

Jambo la kukamatwa mara kwa mara kwa wazee hawa liliwanyima amani ya kuishi katika makazi yao na baada ya kuchoshwa na kadhia hii ndipo wazee hawa wakakata shauri la kumuendea Mwl Julius Nyerere ili kumfikishia malalamiko yao.

Wazee hawa walipoonana na Nyerere wakamwambia kuwa katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika sote tulikuwa pamoja tukishirikiana kudai uhuru sasa iweje leo baada ya Tanganyika kuwa huru thamani yetu ipotee.

Mzee mmoja katika wazee hao Mzee Sugal Mohamed akamkumbusha Mwalimu mkasa wa yeye kutaka kukamatwa na serikali ya Waingereza wakati wa vuguvugu la kupigania uhuru.

Mzee Sugal akamweleza Nyerere kisa kizima cha kutaka kushikwa na serikali ya Kiingereza mjini Arusha.

Ilikuwa hivi:

''Katika harakati za Tanganyika kupigania uhuru Mwl. Julius Kambarage Nyerere akiwa mjini Arusha, akihamasisha watu kuunga mkono Tanu, kulipatikana taarifa za kutaka kukamatwa Nyerere na serikali ya kikoloni ya Muiingereza.

Mohamed Sugal akamchukua Nyerere kwa gari yake aina ya Land Rover na kutokomea nae mpaka msituni umbali mrefu kutoka mjini ili kuwakwepa makachero wa serikali ya Muingereza.

Inasemekana kulikuwapo na watu wenye magari yao na wangeweza kumsaidia lakini hawakuonesha nia ya kutoa msaada wowote kwa Mwl. Nyerere.

Baada ya kufika msituni Mwl Nyerere alitaka kumlipa Mzee Sugal malipo kama shukrani ya kumuokoa na balaa hilo lakini kitu cha kushangaza kama sio kustaajabisha kwa moyo aliokuwa nao Mzee Sugal akamwambia Nyerere kuwa amefanya msaada ule kama moja ya mchango wake katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Baada ya Nyerere kukumbushwa mkasa huu alisikitika sana kisha akaomba aitwe Waziri wa Mambo ya Ndani Meja Jenerali Muhidini Mfaume Kimario na kuulizwa kuhusu kadhia ya wazee wale.

Mwl. Nyerere alimwambia Meja Jenerali Kimario kuwa kwa kitendo cha kuwasumbua wazee wale si jambo jema, akaongezea kusema kuwa wakati Tanganyika inafanya harakati za kudai uhuru pale Moshi alipokulia Muhidin Kimario walikuwapo majasusi wa wakoloni wakiitumikia serikali ya Kiingereza wakipinga harakati za Tanganyika kuwa huru, hawa wazee wakati huo walichangia mchango wao hadi ikawa sababu ya kupatikana uhuru.

Mwl. Nyerere alitoa amri kusipatikane mtu wa kuwasumbua wale wazee na wapatiwe haki sawa na Watanganyika wengine bila kubaguliwa kwa namna yoyote ile.

Nyerere alimuuliza Mzee Sugal Mohamed kama ile Land Rover yake iliyomuokoa bado ipo, Mzee Sugal akamjibu ipo.

Bila kusita Nyerere alimuomba Mzee Sugal ailete Land Rover yake hiyo ili iwekwe kama kumbukumbu, naye mzee Suagl bila khiyana aliipeleka Land Rover yake hiyo Makao Makuu ya nchi Dodoma na ikahifadhiwa kama kumbukumbu ya uhuru.

Hii ilikuwa ni miaka ya 1988 mpaka 1989.

Mzee Sugal Mohamed alifariki mwaka 1995.

PICHA: Guled Issa akiwa Maktaba na picha ya mwisho ni Meja Jenerali Muhidin Kimario.
Hao majasusi wa wakoloni waliokuwa Moshi wakipinga Tanganyika kuwa huru walikuwa wanaona mbali sana. Tungebaki na wakoloni sasa hivi tungekuwa ni moja ya mataifa yenye maendeleo makubwa kabisa na siyo nchi inayogawiwa vipande kwa waarabu kama ilivyo sasa!
 
Atajitokeza na aliyemsaidia maji ya kunywa nae adainkuwmekwa kwenye historia
Ivan...
Utapita kichochoro kipi umfikie Nyerere na kata yako ya maji?
Nyerere alikuwa kazungukwa na watu madhubuti.

Sahani yake ya chakula ilikuwa inazungushwa utadhani kitabu cha maulidi hadi iwekwe kwake ale.

Haya si ya kufanyia kejeli ulizeni muambiwe.
 
Naam, Historiaaridhawa kabisa, shukran sana.
The Republican,
Watu wengi wanaokuja Maktaba kunihoji huwa hawafanyi kejeli katika historia hii.

Huniweka kitako kabisa wakaniuliza maswali ya maana sana wakitaka kuijua historia hii kwa undani zaidi.

Kitabu cha Abdul Sykes kinakwenda chapa ya tano sasa.

Kitabu kimewavutia wasomaji wengi sana.
 
MZEE SUGAL MOHAMED ALIVYOMTOROSHA MWALIMU NYERERE ASIKAMATWE NA MAKACHERO
na Guled Issa

Mzee Sugal Mohamed ni moja ya majina ya mashujaa yanayopaswa kuingia katika historia ya mashujaa waliojitolea katika kuwakinga viongozi wa harakati za uhuru wasidhalilishwe na wakoloni wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mfano wa Mzee Sugal ni moja ya mifano mingi ambayo hii leo haifahamiki na wala hakuna juhudi ya kuhifadhi kumbukumbu hizi.

Labda kama ingelikuwa si kisa kilichomkuta yeye na wenzake baada ya uhuru historia hii ya huyu mzee isingelifahamika kamwe.

Kijografia Mzee Sugal Mohamed alikuwa anaishi Arusha kwa sasa ni Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara.

Mzee Sugal alikuwa Mtanganyika mwenye asili ya Kisomali.

Baada ya Tanganyika kujipatia uhuru wake mwaka 1961, Meja Jenerali Muhidini Mfaume Kimario akishika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Ndani kuanzia mwaka 1983 mpaka 1989 katika kipindi chake kama waziri mwenye dhamana alipata kuwanyima amani wazee wa Kiislamu Watanzania wenye asili ya Kisomali katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mtwara na sehemu mbalimbali nchini kwa kuwakamata kila mara.

Jambo la kukamatwa mara kwa mara kwa wazee hawa liliwanyima amani ya kuishi katika makazi yao na baada ya kuchoshwa na kadhia hii ndipo wazee hawa wakakata shauri la kumuendea Mwl Julius Nyerere ili kumfikishia malalamiko yao.

Wazee hawa walipoonana na Nyerere wakamwambia kuwa katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika sote tulikuwa pamoja tukishirikiana kudai uhuru sasa iweje leo baada ya Tanganyika kuwa huru thamani yetu ipotee.

Mzee mmoja katika wazee hao Mzee Sugal Mohamed akamkumbusha Mwalimu mkasa wa yeye kutaka kukamatwa na serikali ya Waingereza wakati wa vuguvugu la kupigania uhuru.

Mzee Sugal akamweleza Nyerere kisa kizima cha kutaka kushikwa na serikali ya Kiingereza mjini Arusha.

Ilikuwa hivi:

''Katika harakati za Tanganyika kupigania uhuru Mwl. Julius Kambarage Nyerere akiwa mjini Arusha, akihamasisha watu kuunga mkono Tanu, kulipatikana taarifa za kutaka kukamatwa Nyerere na serikali ya kikoloni ya Muiingereza.

Mohamed Sugal akamchukua Nyerere kwa gari yake aina ya Land Rover na kutokomea nae mpaka msituni umbali mrefu kutoka mjini ili kuwakwepa makachero wa serikali ya Muingereza.

Inasemekana kulikuwapo na watu wenye magari yao na wangeweza kumsaidia lakini hawakuonesha nia ya kutoa msaada wowote kwa Mwl. Nyerere.

Baada ya kufika msituni Mwl Nyerere alitaka kumlipa Mzee Sugal malipo kama shukrani ya kumuokoa na balaa hilo lakini kitu cha kushangaza kama sio kustaajabisha kwa moyo aliokuwa nao Mzee Sugal akamwambia Nyerere kuwa amefanya msaada ule kama moja ya mchango wake katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Baada ya Nyerere kukumbushwa mkasa huu alisikitika sana kisha akaomba aitwe Waziri wa Mambo ya Ndani Meja Jenerali Muhidini Mfaume Kimario na kuulizwa kuhusu kadhia ya wazee wale.

Mwl. Nyerere alimwambia Meja Jenerali Kimario kuwa kwa kitendo cha kuwasumbua wazee wale si jambo jema, akaongezea kusema kuwa wakati Tanganyika inafanya harakati za kudai uhuru pale Moshi alipokulia Muhidin Kimario walikuwapo majasusi wa wakoloni wakiitumikia serikali ya Kiingereza wakipinga harakati za Tanganyika kuwa huru, hawa wazee wakati huo walichangia mchango wao hadi ikawa sababu ya kupatikana uhuru.

Mwl. Nyerere alitoa amri kusipatikane mtu wa kuwasumbua wale wazee na wapatiwe haki sawa na Watanganyika wengine bila kubaguliwa kwa namna yoyote ile.

Nyerere alimuuliza Mzee Sugal Mohamed kama ile Land Rover yake iliyomuokoa bado ipo, Mzee Sugal akamjibu ipo.

Bila kusita Nyerere alimuomba Mzee Sugal ailete Land Rover yake hiyo ili iwekwe kama kumbukumbu, naye mzee Suagl bila khiyana aliipeleka Land Rover yake hiyo Makao Makuu ya nchi Dodoma na ikahifadhiwa kama kumbukumbu ya uhuru.

Hii ilikuwa ni miaka ya 1988 mpaka 1989.

Mzee Sugal Mohamed alifariki mwaka 1995.

PICHA: Guled Issa akiwa Maktaba na picha ya mwisho ni Meja Jenerali Muhidin Kimario.

View attachment 3027618View attachment 3027619
Umri hauna maana kabisa. kumbe Muhidin Kimario alikuwa blazamen namna hii?

Nilimfahamu akiwa mdingi na mkitambi wake...
 
Back
Top Bottom