Kwa Mimi kama ni gaming kitu cha Kwanza cha msingi ni GPU.
GPU ni Graphics Processing Units KAZI yake ni ku-render images(kitu kama kuchora au kuonyesha picha) za gemu
FPS kirefu chake ni Frames Per Second, unavyoona video ni mkusanyiko WA images nyingi Tu, jicho la binadamu huona picha zikiwa kwenye motion iwapo image 24(kama sijakosea) zikiwa zinapita Kwa sekunde moja yaani 24fps.
Hivyo GPu inayorender frames(images) nyingi inafanya gemu kuwa nzuri Ila VRAM itabidi iwe kubwa na CPU iwe na core nyingi huku ikiwa na performance kubwa kwenye thread moja( core moja tuseme)
Maana gemu za siku hizi Kama Far Cry 6 inatafuna karibu GB 10 ya VRAM na 15GB ya RAM
Fremu zikiwa nyingi gemu ndio inakuwa smooth kucheza na kama refresh rate na yenyewe ikiwa kubwa (zaidi ya 60Hz), na ikiwa unaweza kupata zaidi ya 60fps kwenye ultra graphics settings kwenye resolution ya 1440p au 1080p hata 4k
Na kama unapenda kucheza online games basi GPU yenye NVENC encoder inasaidia kupata fremu nyingi, 1060 haina hii
DLSS kirefu chake ni Deep Learning Super Sampling hii ni teknolojia ya artificial intelligence iliyoundwa na NVIDIA Kwa ajili ya uboreshaji WA muonekano WA graphics.
Kikawaida ukicheza gemu kwenye low settings graphics utapata fremu nyingi zinazoweza fika hata 80fps Kwa low end na mid range GPU kama 1060, 1660, 2060 lakini ubora WA images inakuwa ni WA chini. DLSS inakuza ule muonekano WA graphics na kufanya graphics kuonekana kuwa kama high settings kumbe ni low
Idadi ya core pia ni ya kuzingatia gemu kubwa kubwa huwa zinaweza kukamua mpaka core 8, kikubwa ni uwezo CPU kwenye single thread.
GTX na RTX ni brand name za NVIDIA
GTX ni matoleo ya geforce 10th series yaliyokuwa yanatumia paschal architecture
RTX nadhani inamaanisha GPU inasapoti ray tracing, mambo ni mengi.
Kwa kifupi gaming PC zingatia GPU kama ndio msingi binafsi Naona kuanzia rtx 2060 kwenda mbele au gtx 1080 Ti, CPU yenye core zaidi ya 6, faster ram GB 16 (ddr4 2500Mhz) nk