PostGE2025 Larry Madowo: Sijalipwa na mtu yoyote kuchafua taswira ya nchi yoyote

PostGE2025 Larry Madowo: Sijalipwa na mtu yoyote kuchafua taswira ya nchi yoyote

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mtangazaji wa CNN na mwandishi wa makala kuhusu matukio ya Oktoba 29 yaliyotokea Tanzania amesema kuwa hajalipwa na mtu yeyote kwa lengo la kuichafua nchi yoyote. Ameeleza kuwa badala ya hoja na ushahidi uliomo kwenye makala kujibiwa au kukanushwa, amekuwa akishambuliwa binafsi.

Aidha, ameweka wazi kuwa baadhi ya video zinazotengenezwa dhidi yake ni za uongo, na amedai kuwa zinatengenezwa kwa kutumia teknolojia ya AI.
 
Wanasema ni ubwawa aka mchele mchele aka mchicha mwiba

USSR
 
Wauaji wanatapatapa sana kupitia uzushi, Propaganda, uongo
 
Mtangazaji wa CNN na mwandishi wa makala kuhusu matukio ya Oktoba 29 yaliyotokea Tanzania amesema kuwa hajalipwa na mtu yeyote kwa lengo la kuichafua nchi yoyote. Ameeleza kuwa badala ya hoja na ushahidi uliomo kwenye makala kujibiwa au kukanushwa, amekuwa akishambuliwa binafsi.

Aidha, ameweka wazi kuwa baadhi ya video zinazotengenezwa dhidi yake ni za uongo, na amedai kuwa zinatengenezwa kwa kutumia teknolojia ya AI.
Hata akilipwa.

Jadili hoja usijadili mtoa hoja.

Ukijadili mtoa hoja badala ya hoja, hiyo ni ad hominem logical fallacy. Ni dalili ya kushindwa kujibu hoja.

Kwani akilipwa kufichua ukweli kuhusu mauaji ya serikali Tanzania, wakati mauaji hayo ni ya kweli na yanatakiwa kufichuliwa, mauaji hayo yatakuwa ya uongo?

Kwa nini tunataka kuhamisha goli kutoka habari ya mauaji kwenda kwa mtoa habari?

Watu hawajauawa Tanzania?

Larry kasema uongo wapi?
 
Ukweli utabaki kua ukweli tu, Larry endelea kusema ukweli
“Heri wale wanaodhulumiwa kwa ajili ya haki… furahini na shangilieni, kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni.”
 
Back
Top Bottom