Latino na harakati za kuzamia ughaibuni mpaka kutoswa baharini

Duh
 
Stori nzuri na hongera kwa kuandika kwa urefu
 
Tumerejea nakazia Latino ndio mwenye mkasa sio Mimi kama umeshawai sikia popote kisa chake basi OK ndio mana nikasema Anasimulia wapo awajakiskia ndio wanasoma hapa nafikiri tumeeelewana then ilo LATINO sio jina lake halisi ilo jina kajipa kutokana na harakati zake za uzamiaji.... OK

Tuendelee......
Basi tulikwenda kule kwenye kile kisiwa jumla tulikua wanne kweli samaki walikua wanapatikana pale kisiwani na tulikua na boti kubwa kidogo na pia ilikua na barafu ya kutosha ya kuhifazia samaki wasiharibike kwa kipindi kirefu pamoja na masunduku makubwa ya kuhifazia samaki ivi vitu ni oda tulipewa na boss flani tunapopata mana ake tupeleke kwake pia tulibeba vitu vingne kama kisu iki kisu chenye boya ata kikitumbukia majini akizami kiberiti cha chuma pia na baruti zile za kupasulia miamba sasa tuliingia kwenye uvuvi haramu yes tukaweka kambi kwenye kile kisiwa tukatafuta eneo zuri tukaweka makazi safi kila tutakapo maliza shughuli zetu basi tutarudi pale kupumzika.

Kuhusu kisiwa inasemekana kwamba miaka ya nyuma palikua na watu wanaishi pale waliweka makazi kifamilia lakini watu wale ghafla tu walitoweka na aikujulikana walikwenda wapi na hata kutoka kwao awakuonekana kama wamevuka kwenda upande gani ila ilisemekana kile kisiwa ni lango kuu la viumbe vya ajabu ambavyo vinatoka angani na kuja eneo lile lakini upande wa pili inasemekana kulikua na jamii nyingne iliishi uko.
Lakini pia pembeni kulikua na kisiwa kingne ambacho kiliibuka tu apakua na historia ya kuwai kuwapo ilisemekana ni nyangumi kwaiyo kile atuku deal nacho sie tulibaki pale tulipofikia, basi shughuli iliyotupeleka pale ikaanza rasmi siku iyo kama kawaida tukaingia mzigoni kwenda kuvua samaki tulipofikia eneo la tukio kwenye kina kirefu tukatoa zile baruti tayari kwa kuzilipua ila kabla ya atujalipua tukaanza pata ishara mbaya ilikuaje mwenzetu mmoja akaingia chini alishuka kwenye maji kwenda kuangalia uwepo wa samaki maeneo yale na jamaa uwezo wake uliluhusu alikua ana pumzi ya kutisha lakini pia kuogelea alikua njema basi jamaa alizamia kwenda kucheki alicheki lakn kupitia maelezo yake baadae kule chini alimuona papa sasa kwa vile ye ni mtaaalamu aling'amua fasta kwamba hapa pana hatari na ukiwa kwenye maji papa kukona ni laisi kupitia viganja vya mikono au miguu vingang'aa kwaiyo laisi kukuona jamaa alivyogundua kwamba yupo kwenye hatari ikabidi aludi juu sasa kwa kupiga makasia akaibuka juu na kuita kwamba tusogeze boti alipoibukia alikua mbali kidogo nasi fasta tukaanza paleleka boti kule kwake nae akawa anakuja kwetu spidi alijiatidi kuyakata maji vilivyo wakati huo yule papa sasa ndio anakuja nae spidi kumfata mshkaji.
Sasa jamaa alipofikia boti na kukamata akitaka kudandia ndani yule papa alikuja ghafla akamralua jamaa kwenye kisigino cha mguu pia akagonga na ile boti nusu ipinduke jamaa akaingia ndani wakati huo tayari keshaumia mguuni damu zinatiririka kwa wingi.

Basi mshkaji tukafunga bandeji mguuni tulimpa huduma ya kwanza na hapo tuakageuza tukarudi atukufanya tena kazi tulirudi kule kisiwani kwetu kuandaa maakuli na vitu vingne.

Kile kisiwa kumbe ilikua ikifika usiku kuna sauti zinasikika toka porini na azieleweki za nni kama sokwe au mbwa ni sauti za ajabu tulikua tunaskia lakini habari za sauti atukuskia kabisa ndio tulizipata pale sasa.
Kwaiyo pale tuliendelea kuwepo kwa siku kazaa tukiendelea kuvua samaki kama kawaida kuna siku tuliingia kuvua usiku wakati tupo katikati, bahari ikabadilika ikachafuka pakawa na zile pepo za kusi za nguvu maji yakabadirika rangi yanakua kama matope ivi alafu mawimbi makubwa makubwa usawa wa nyumba kile chombo chetu kikaanza kuyumba hasa na pia tulikua na taa yetu moja karabai lakini sio ya kujaza upepo ilikua ya utambi ok ambayo tunatumia kuvutia samaki ile taa ilikua na utambi flani ivi sasa ule utambi uliisha ila sisi atukujua icho kitu kabla ya kuja nayo.

Ile zoruba ya bahari na upepo ile taa ikazima tulipojarbu kupandisha utambi kisha upepo ule mkali kwenye kuangaika uku na uku ile taa ikaenda na upepo hapa sasa tukawa kiza atuna hata harama ya kuashiria tupo pale kwajili ya kuonekana kama itatokea meli kubwa zisitugonge ilikua ni mida ya usiku mkubwa iyo kama saa 8 au Tisa ivi ndio tupo kwenye icho kizaa zaa.

Aikuchukua muda sana wakati tupo hapo atuna ili wala lile ghafla meli hii hapa na ipo usawa wetu ila sio sana apo atuja jianda mana imetushtukiza tu akuna la zaidi ile meli ikaja ikatupalaza ilitupita pembeni lakin iliturusha na kile chombo chetu kilipasuka na kila mtu alilushwa upande wake ni vurugu tupu.

Uzuri atukua kati kati kabisa pale tungekufa ilitupitia pembeni apo sasa kila mtu aokoe uhai wake binafsi niliwai dumu la maji lilikua na maji kidogo pia na kamba nikajifunga tumboni liwe boya langu sasa nisije kuzama kama ntaishiwa upepo.

Wale wenzangu sasa sikujua walirushwa wapi mi nikaanza kupiga makasia kwa kuhsi tu maana sina uelekeo wowote nikayakata maji nikayakata maji ikafika muda pumz imekata sina upepo nikakata moto nikazimia kabisa fahamu zikapotea
Sikuelewa kilicho endelea saa kumi na moja alfajiri kwa makadirio nikashtuka nipo ufukweni ina maana muda nazima nilikua karibu na ufukwe kule kisiwani.
Ina maana lile dumu lilinivuta vuta mpaka pale kwenye ufukwe wa bahari nikabaki hapo..
Basi nikajivutavuta mpaka pale kisiwani angoche Niko mwenyewe tu wale wenzangu siku waona kwa haraka nikajua wazi sasa wamekufa. Nikasubiri kukuche mana mvua ilikua inanyesha na lile banda letu liliku Lina vuja ivyo kulivyokucha nikafanya utaratibu wa kurekebsha nikiwa mwenyewe na pale nilipo hapana uhakika wa kupita mtu mana pale kisiwani watu huwa awendi kutokana na imani zile za kishirikina .

Pale palikua na kibiriti pia kisu pamoja na bangi kwajili ya kufukuzia mambo ya majini na vibwengo awapendi ile harufu ya mjani ila sina hakika basi nikaingia msituni mule kwenye kisiwa nikatafuta Magogo ya maana makubwa ili nikiwasha moto usizme mana isije mbele kiberiti kikaisha ikawa tabu na pale na kihitaji muda wote.
Nilianza kuishi pale mwenyewe nikiwa nakula kaa gogo mikaa flani ivi mikubwa ile ambayo ina mikasi mikubwa kama ianakamata kidole inakata nilichonga mti vizuri ndio nikawa nawindia wale walikuapo pale pembezoni mwa ufukwe kwenye vimiti miti nikiwakuta nilikua nawachoma nakuja kuchoma pale kwenye moto na kua msosi palikua na miti ya minazi nilikua naangua Yale madafu kwajili ya maji ya kunywa yalikua yananisaidia pale.
Sasa kile kisiwa ilikua sasa iifika usiku ni hatari mzee zile kelele kama za wanyama ndio zina sikika sasa alafu sometimes unaona kam mtu kavaa ushungi ka mwarabu anakuja Mara ghafla anapotaea Mara unasikia marashi yapo karibu yako kabisa ki ukweli lile eneo ilikua ikikfika usiku basi amani inanitoka akuna usalama zaidi ya hofu tu kwangu ..............
Wakuu
Latino ata endelea si muda

Maphoto yapi tena Mirlz B Matthew
 
Aisee inahitaji ujasiri kuyaishi maisha hayo
 
Dah kuna popoma moja itakuja kusema eti ilizamia geita

Naua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…