Latino na harakati za kuzamia ughaibuni mpaka kutoswa baharini

Latino na harakati za kuzamia ughaibuni mpaka kutoswa baharini

Tumerejea Latino katika safari yake *********** inaendelea

Kama nilivyosema inapofika usiku muda huo nakosa amani kabisa kutokana na vutu vya ajabu ambavyo nilikua naviona pale kisiwani kwaiyo sikupenda kabisa usiku uingie.

Basi nikaendelea kuwepo katika kisiwa kile na maisha ni Yale yale na hata chakula msos ndio ulikua ule wa kaa gogo ila kuna siku nilimpata samaki chewa akiwa ameharibika kafa tayari.
Nikamtengeneza vizuri akawa msosi safi kwangu lakini pia katika kile kisiwa palikua na panya wakubwa wanaendana na ndezi pia walikua wanauma wana meno makali sasa yale mabaki ambayo Mimi nilikua nayaacha wao ndio walikua wanafata kula ivyo nao niliwafanya msosi wanapokuja nilikua nawachoma na ule mti nilio uchonga wakushikia kaa kisha nawachoma natafuna msosi.

Basi katika kuendelea kuwepo pale kama nilivyosema palikua na kelele za ajabu ambazo zilikua zinatoka kwenye msitu apo kisiwani sasa siku iyo mida kama ya saa kumi zile sauti nikazisikia tena sio usiku kama nilivyozoea safari hii ni mchana na jua lake ndio zinapiga,
Sasa nikaona sio kweli nikavaa ujasiri nikaona ngoja nizifatilie zile sauti zinakotoka nijue ni za nini zilitoka ndani kabisa ya msitu.

Basi nika elekea uko nijue kuna nini nikaenda msitu umefunga kwaiyo nilikua nafanya kutanua miti ivi kisha napita taratibu taratibu nikifata zile sauti zinakosikika nilikwenda mpaka nilipokaribia zinakotoka zile sauti nikatulia kwa umakini nikapata nafasi nzuri kisha nikachungulia laivu kabisa nikaona sehemu ya tukio.

Palikua na viumbe na hao viumbe ni nyani wakubwa sio sokwe ni kama walikua wanafanya sherehe kabisa mana walizunguka ki mduara na katkati palikua na wengne kama ndio wahusika na palikua na ngoma izi za miti sio ngozi zile za mfano wa marimba ambazo unapiga na miti waliweka miti ndio wakawa awa nyani wanapiga na wengne wakiwa na shangwe kabisa bila shaka historia aikukosea kusema binadamu tulianzia uko pale palikua na shughuli ambayo wao walikua wanaifanya kama sherehe

Nakazia walikua nyani sababu pale unaweza hisi ni majini lakini kama ni majini Basi ata pale nisinge wafikia na nyani tuna shahabiana na binadamu ata kiakili mengne wanafanya kama binadamu ndio walikua wakifanya shughuli ile pale msituni lakini pia ni ngumu mno kuona yani bahati sana binadamu wa kawaida kuweza kuwaona.

Basi nikiwa natazama kile kinacho endelea pale lakini pia kuna kua na shida endapo ikitokea wale wakajua
nami ndio ikanikuta sababu kumbe pale pana ulinzi yupo ambae anakaa sawaia kuhakikisha akuna kiumbe cha tofauti kinakuja pale kama akiona anaenda haraka kutoa taarifa kabla ujawafikia ina maana mpaka mimi nakwenda pale yule mlinzi wao akuniona bado.

Sasa nikiwa natazama ghafla kuna nyani mmoja alitokea maeneo yale nilipo Mimi uyu sasa ndio alikua mlinzi alikua spidi akaelekaea kule kwa wenzake kutoa taarifa alafu alikua anatoa mlio flani ivi lakini nae alivofika akapigwa makofi na wenzake inavyo ashiria alichelewa alafu baadae akaonesha uku nilipo Mimi hapa sasa nikajiona nipo kwenye hatari ili ni janga akuna kingine zaidi ya kuondoka eneo lile.
Wazo la haraka kupanda kwenye mti uongo kwaiyo nika amua nikimbie na wale nyani wakaunga pale pale kuja kwangu nao spidi aya yalikua madume maana yalikua makubwa sana.

Nilitoka mbio mpaka pale kwenye kibanda nilichofanya sikukaa pale nilikimbilia kwenye maji pale kibandan nilichukua lile dumu kama itatokea wakaingia kwenye maji niende mbali japo sikua na hakika kama wanaweza ingia majini nikaenda nalo dumu mpaka kwenye maji kule nao hao mi nikaingia kwenye maji wao wakaishia ukingoni pale mwa maji ufukweni.

Nilikaa ndani ya maji mule karibu saa nzima wao wapo pale nje wana nisubiri mi nawatizama tu pale baadae wakati Giza linaingia wale nikawaona wanaondoka wakapotea nami nikarudi pale kibandani japo nilikua na hofu lakini mara nyinngi nyani inapofika usiku huwa ana ujanja wa kiasi hicho kwaiyo nilirudi pale bandani.
Siku ya pili asubuhi baada ya kuamka tu ile nikaanza kusaka msosi kuwinda wale wadudu mule pembezoni mwa fuke aisee nikakutana na mshikaji mmoja kati ya wale ambao tuligongwa na meli ambao tulifika kuweka makazi pale kisiwani nilimkuta akiwa katika hali mbaya.

Kachoka na alafu ana vidonda vya kung'atwa na wale panya ambao nilikua nawatafuna nikiwapata pale kibandani wanapokuja kusaka masalio, jamaa kumbe nae pale katika kusambaratishwa aliogelea na kipanda cha ubao cha boti na pale alifika Ila sasa alivunjika mguu mfupa ulikua nje unaonekana
Sasa pale alivyofika mwanzo alikua anatafuta chakula kwa kujivuta kutokana na kuhumia mguu Ila mbeleni alishindwa ndio mana akazoofika nami nilimkuta kwenye hali iyo.
Akaniambia pale yeye angeshakufa isipokua kuna usiku mmoja wakati kama amelala kuna wadada wawili walimtokea yani ndotoni akiwa kwenye usingizi walifika wakiwa na marash yani wananukia kisha wakampa mpole na wakamuuliza hapa mmekuja kufata nini?
Kisha wakatoa kinywaji flani kama maziwa wakampatia anywe akanywa baadae alishtuka na aliweza kukaa kama takriban siku tatu au nne pasipo kusikia njaa.
Jamaa alikua kwenye kauli ya mwisho na ile kuonana na Mimi ndio Mara ya mwisho kwani akuchukua mda alifariki pale pale mbele yangu mwana alikufa nikimuona kumbuka mtu wa pili namshuhudia akifariki.

Nikachimba shimo kumsitiri mshkaji na nikamuhifazi nikampigia dua njema aendako ki ukweli sikua na raha siku iyo maana sasa hisia mbaya zikawa zinanijia kwamba hapa nami nitakufa tu japo nilikua Nina nguvu zangu bila shida yoyote mana sikuumia popote.

Pia pale kisiwani niliiishiwa maji nikawa natumia yale maji yanayopatikana kwenye miti flani unaikata kisha inamwaga maji ya kutosha ndio nikawa sasa natumia ayo.

Siku zilikatika, siku moja sasa nikiwa pale ufukweni kwa mbali nikaona kimeli kidogo ivi kipo na jahazi nyuma wamelifunga wanavuta na walikua wanakuja upande niliopo Mimi pale ufukweni apo nilijificha kwanza nikiwatazama walifika mpaka pale wakashuka walikua ni wasomali walishuka na mirungi na bunduki alafu wale kumbe walikua ni mahalamia wa kuteka meli baharini.

Baadae Mi nikajitokeza, fasta sana wakanipigisha magoti na kuniweka chini ya ulinzi mitutu yote kwangu wakaniuliza jina langu pia dini yangu kiswahili wanakielewa nikawatajia mi ni muislamu wale jamaa nao pia ni ivyo ivyo nivyotaja jina wakasema kuna nabii mwenye jina lako alipata matatizo na akaja kuokolewa na wapita njia una mfahamu?
Nikamtaja basi wakasema nawe pia umeokolewa na sisi pia wakaniambia nisome sura flani ivi ya kufungua ibada waislamu wana elewa ili ufanye ibada unaanza na sura iyo inaitwa surat infaata nikawasomea vilivyo mpaka mwisho uzuri nilikua nafahamu wakaelewa kwa kuitikia msahalaah na kunikaribisha .

Katika wale kwenye lile kundi pia kulikua na mtoto wa kike na pia alikua na kaka yake uyu wa kike aliitwa Sofia na kaka mtu aliitwa Masud yule sofia nilimuona na silaha
sub machine gun (SMG) double magazine zilizo jaa risasi na wale wengne walikua na bunduki za AK47 fourty seven sasa nilijiunga na wale jamaa kwenye ile kambi tukawa pamoja yule Sofia alikua akikaa sana na Mimi akiniulizia sana story jinsi nilivyoweza Ku survive
pale nilipo
basi alikua anapenda sana zile story wale wasomali kufika kwao pale chombo chao kilikua na matatizo ..................................

Tupumzike tutarejea Latino is on....
Huu uongo sijui mwisho wake ni nini
 
Naaaamu Turejee sasa
Jamii forum na Hati chafu, za mapenzi ni kweli zinaharibu nyuzi???? Mkaguzi mkuu wa nyuzi JF fdizzle na msaidizi wake TODAYS wata jibu Embu tuone

Inaendea
kile chombo chao au meli walyokuja nayo ilikua na mushkeri kidogo sasa kufika kwao pale ni kwajili ya marekebisho alafu ile meli kumbe waliiteka na watu waliopo mule sikujua waliwaacha wapi nahisi yawezekana waliwatosa majini lakini pia mule mlikua na vitu walivyoteka Mchele, unga, sukari, samaki na vingne vingi kwaiyo kwa ishu ya misosi aikua tabu tena kwangu apo ni mtelezo tu.

Kwaiyo apo sasa yule Sofia ndio alikua mpishi na Mimi mda mwingi ndio nilikua nae kumsaidia kutengeneza samaki na mboga mboga kisha msosi fresh.

Wale jamaa walendelea kuwepo pale mpaka maji yalipo pungua kwwnye kile kisiwa kunakua na siku maalumu ya kutoka yale maji sasa ile meli ndio ilikua na tatizo chini kwaiyo maji Yale yalipo pungua ndipo ikawa nafasi ya wao kuweza kurekebisha ile meli.
Walifanya mawasiliano na wenzao wakaja pale wakfanya marekebisho ile meli ikapata afazali sasa hapo ndio wakaniambia twende mbele yani niondoke nao kuelekea uko kwenye uharamia wa kuteka meli baharini humo .

Walitoa begi moja la silaa kisha wakaniambia nichague ipi itakayo nifaa nikachagua silaa moja inaitwa Raifo sina hakika kama nimeandika sahihi wakaniuliza kwann umechagua hii niliipenda tu zile ni Silaa ambazo zilitumiwa na ma sniper kwa juu ilikua na lenzi binafsi nieleze nilishawai kufundshwa kutumia silaa na babu yangu alikua muwindaji wa wanyama pori alikua anatumia izi silaa lakini sio kama ile.
Hii iliboreshwa zaidi na baba yangu nae alikua mtaalamu wa kutumia silaa.
Basi nilichukua ile silaa ili kuwaonesha kwamba na Mimi naweza itumia nikafanya jambo moja wale wabaya wangu nyani ndio nikaona ngoja niende uko Leo nika wanyooshe nikamchukua Sofia tuka elekea kule msituni uzuri nikakutana nao tukiwa na Sofia nikamtandika nyani mmoja na tukarudi kule na Sofia na yule nyani.

Yule nyani pale wale wajamaa walimtafuna vizuri mi ndio nilimtengeneza sasa hapa nikajua jamaa hawa magumashi akuna cha dini wala nini hawa ni maaalamia tu dini wanayao lakini awa izingatii wnabaki tu na kivuli cha dini awana lolote tulikula nyani yule vizuri .
Sasa tukaingia kwenye utekaji katika ishu hii ya utekaji tulishateka teka sana Ila kuna tukio moja lilikua kubwa ambalo tulikutan nalo uko baharin, tulikutana na meli ya wafanya biashara ambayo ilikua na mizigo tuliwateka wale jamaa na tukachukua mzigo wao,

wao tukawaacha na hata meli atukuizamisha sasa kumbe wale jamaa wakafanya mawasiliano na askari wa patrol kutokana na ule uaharamia tuliofanya sisi atuna habari ghafla wakaja wale patrol na boti zao walitumia spika vipaza sauti vile kwamba tunatakiwa tujisalimishe alafu ile meli yetu pale palipotengenezwa palileta itilafu tena kwaiyo ikawa aina spidi sasa mi ndio nilikua na ile silaa ya kulenga mbali nilikua juuu
kwaiyo pale ikabidi nianze akuna kungoja walikua na boti zao mbili nilipiga moja kwenye tenki za mafuta nikapasua wale jamaa fasta wakahamia nyingne nzima ile niliyopiga ikalipuka hapa nafikiri wali elewa kua kuna mdunguaji.

Awakuchukua mda waliondoka pale sie tukaendelea na safari yetu taratibu alafu katika kupora vitu kuna jamaa nilimpora begi ndogo ivi ye nahisi alikua mtu wa kanisa nilivyo fungua nilikuta kuna vitu vya kanisa na pia kulikua na msaba wa dhahabu niliuchukua nikauficha ikitokea uko mbeleni unisaidie kama nikiuza.

kumbe walivyo ondoka wale patrol walienda kujipanga,
sisi atuna habari
Ghafla walifika wale jamaa na boti tatu tena sasa walipofika awakuchelewa wakaanza kurusha risasi kwetu yule masuz na mwingne ally pamoja na mwingne tena kasimu wao wakaanxa kujibu mashambulizi mi nilkua kwa juu kabisa wao wapo chini katika kurushiana zile silaha yule masuz dada ake na Sofia akapigwa risasi kifuani kwenye moyo nyingne begani akazima pale pale.

Sasa kule juu Mimi nikaendelea kulusha zile risasi ila walikua wanatuzunguka awatulii sehem moja baadae Mimi niliipigwa risasi ya kiuno lakini ilinipalaza au kunikwangua aikuingia moja kwa moja nilikua navunjika kiuno hapa lakini sikupata athari kubwa basi nilidondoka toka kule juu mpaka chini kwenye meli nikapoteza fahamu pale pale.
Nilipokuja kuzinduka tuilikua kisiwani yule Sofia alikua akinisaidia kunitibu lile jeraha la kuchunwa na risasi alitumia kisu cha moto kuchoma lile jeraha kuondoa kama kuna unga ule wa silaha ili kuua sumu maana zikibaki huwa zinaleta mazara ata kansa pia akachukua majani flani ivi porini akaniwekea ya dawa.

Jamaa yule kaka ake na Sofia masuz tayari alishafariki ivyo tulifanya namna pale tuakamsitiri jamaa, Dada ake alikua na majonzi sana siku ile ndio ishatokea sasa,
Tulikaa pale kwa siku kazaa baadae tukaondoka pale kisiwani tuka elekea kwao walikotokea wao uko somalia namimi kama jamaa yao tulishaungana pale basi tulienda waote mpaka somalia.
Tulipofika kule baada ya kuwasili Mogadishu niliambatana na Sofia mpaka kwenye makazi yake nilikutana na ndugu zake akanitambulisha fresh na pia akafanya mpango kwenye shughuli za uvuvi kuniunganisha na jamaa flani ivi ambao wao walikua wana vua papa kwa kutumia ndoana flani ivi za shaba ndio zilikua imara kwa kuwanasa wale papa.

Niljiunga na jamaa kufanya ile kazi ila Mimi nilikua upande wa kuchochea makaa ya mawe tulikua kwenye zile meli zinazotumia makaa ya mawe sio mafuta ndio nilikua na chochea ila baadae nilisogea mbele nikaacha kuchochea makaa nikawa kwenye upande wa kuvua.

Kule sasa kwenye kuvua ndio nikajua jamaa wanavua papa kwa kutumia chambo za mahiti ya watoto wachanga wa binadamu jinsi wanavyopata vichanga ni vile labda kama mtu mimba yake imeharibika au mtoto kafia tumboni zile mimba kubwa au kazaliwa kafa au wale wanao toa ujauzito mimba kubwa sasa katika kutupa ndio watu wanatumia iyo fursa ule uchafu unachukuliwa na inawekwa oda kabisa kwenye ma hospital tena ina pesa nzuri tu ambayo ma dokta huwa wanapata kupitia hii ishu mpaka leo.

Lakini ni kwa usiri inafanyika hii biashara sio waz wazi so kupitia chambo hiki papa huwa wanakamatika kilahisi na hata ukimpasua ishu ya kukuta labda sikio la binadamu au kidole nywele viungo vya binadamu kwa ujumla ni kawaida sana
Ni ishu ya kikatili ki binadamu lakini ndio watu na kazi zao ..................... Latino is on

Sio kweli slip way
 
Mi kusema za kweli nilikuw naenda vizuri tu ila pale kwenye manyani wanafanya jando na unyago na pale upo kwa juu na bunduki yako yenye lensi ukalenga tanki la petrol la boti ya adui ikalipuka puuuuuuu, ngoma ka muvi nikaanza kuikonsida kivingine hii stori, samahani lakini.
 
Sasa kile kisiwa ilikua sasa iifika usiku ni hatari mzee zile kelele kama za wanyama ndio zina sikika sasa alafu sometimes unaona kam mtu kavaa ushungi ka mwarabu anakuja Mara ghafla anapotaea Mara unasikia marashi yapo karibu yako kabisa ki ukweli lile eneo ilikua ikikfika usiku basi amani inanitoka akuna usalama zaidi ya hofu tu kwangu ..............

.......................................
Why majini na vibwengo huwa na sura za kiarabu?
 
Sasa kile kisiwa ilikua sasa iifika usiku ni hatari mzee zile kelele kama za wanyama ndio zina sikika sasa alafu sometimes unaona kam mtu kavaa ushungi ka mwarabu anakuja Mara ghafla anapotaea Mara unasikia marashi yapo karibu yako kabisa ki ukweli lile eneo ilikua ikikfika usiku basi amani inanitoka akuna usalama zaidi ya hofu tu kwangu ..............

.......................................
Why majini na vibwengo huwa na sura za kiarabu?
Akikujibu unite niko shamba napalilia kidogo!
 
Sasa kile kisiwa ilikua sasa iifika usiku ni hatari mzee zile kelele kama za wanyama ndio zina sikika sasa alafu sometimes unaona kam mtu kavaa ushungi ka mwarabu anakuja Mara ghafla anapotaea Mara unasikia marashi yapo karibu yako kabisa ki ukweli lile eneo ilikua ikikfika usiku basi amani inanitoka akuna usalama zaidi ya hofu tu kwangu ..............

.......................................
Why majini na vibwengo huwa na sura za kiarabu?
Futati
Daku
Daku
Daku
Futari
Chai😂😂
 
Back
Top Bottom