Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Muda wa kula kimasihara sasaTumerejea Latino katika safari yake *********** inaendelea
Kama nilivyosema inapofika usiku muda huo nakosa amani kabisa kutokana na vutu vya ajabu ambavyo nilikua naviona pale kisiwani kwaiyo sikupenda kabisa usiku uingie.
Basi nikaendelea kuwepo katika kisiwa kile na maisha ni Yale yale na hata chakula msos ndio ulikua ule wa kaa gogo ila kuna siku nilimpata samaki chewa akiwa ameharibika kafa tayari.
Nikamtengeneza vizuri akawa msosi safi kwangu lakini pia katika kile kisiwa palikua na panya wakubwa wanaendana na ndezi pia walikua wanauma wana meno makali sasa yale mabaki ambayo Mimi nilikua nayaacha wao ndio walikua wanafata kula ivyo nao niliwafanya msosi wanapokuja nilikua nawachoma na ule mti nilio uchonga wakushikia kaa kisha nawachoma natafuna msosi.
Basi katika kuendelea kuwepo pale kama nilivyosema palikua na kelele za ajabu ambazo zilikua zinatoka kwenye msitu apo kisiwani sasa siku iyo mida kama ya saa kumi zile sauti nikazisikia tena sio usiku kama nilivyozoea safari hii ni mchana na jua lake ndio zinapiga,
Sasa nikaona sio kweli nikavaa ujasiri nikaona ngoja nizifatilie zile sauti zinakotoka nijue ni za nini zilitoka ndani kabisa ya msitu.
Basi nika elekea uko nijue kuna nini nikaenda msitu umefunga kwaiyo nilikua nafanya kutanua miti ivi kisha napita taratibu taratibu nikifata zile sauti zinakosikika nilikwenda mpaka nilipokaribia zinakotoka zile sauti nikatulia kwa umakini nikapata nafasi nzuri kisha nikachungulia laivu kabisa nikaona sehemu ya tukio.
Palikua na viumbe na hao viumbe ni nyani wakubwa sio sokwe ni kama walikua wanafanya sherehe kabisa mana walizunguka ki mduara na katkati palikua na wengne kama ndio wahusika na palikua na ngoma izi za miti sio ngozi zile za mfano wa marimba ambazo unapiga na miti waliweka miti ndio wakawa awa nyani wanapiga na wengne wakiwa na shangwe kabisa bila shaka historia aikukosea kusema binadamu tulianzia uko pale palikua na shughuli ambayo wao walikua wanaifanya kama sherehe
Nakazia walikua nyani sababu pale unaweza hisi ni majini lakini kama ni majini Basi ata pale nisinge wafikia na nyani tuna shahabiana na binadamu ata kiakili mengne wanafanya kama binadamu ndio walikua wakifanya shughuli ile pale msituni lakini pia ni ngumu mno kuona yani bahati sana binadamu wa kawaida kuweza kuwaona.
Basi nikiwa natazama kile kinacho endelea pale lakini pia kuna kua na shida endapo ikitokea wale wakajua
nami ndio ikanikuta sababu kumbe pale pana ulinzi yupo ambae anakaa sawaia kuhakikisha akuna kiumbe cha tofauti kinakuja pale kama akiona anaenda haraka kutoa taarifa kabla ujawafikia ina maana mpaka mimi nakwenda pale yule mlinzi wao akuniona bado.
Sasa nikiwa natazama ghafla kuna nyani mmoja alitokea maeneo yale nilipo Mimi uyu sasa ndio alikua mlinzi alikua spidi akaelekaea kule kwa wenzake kutoa taarifa alafu alikua anatoa mlio flani ivi lakini nae alivofika akapigwa makofi na wenzake inavyo ashiria alichelewa alafu baadae akaonesha uku nilipo Mimi hapa sasa nikajiona nipo kwenye hatari ili ni janga akuna kingine zaidi ya kuondoka eneo lile.
Wazo la haraka kupanda kwenye mti uongo kwaiyo nika amua nikimbie na wale nyani wakaunga pale pale kuja kwangu nao spidi aya yalikua madume maana yalikua makubwa sana.
Nilitoka mbio mpaka pale kwenye kibanda nilichofanya sikukaa pale nilikimbilia kwenye maji pale kibandan nilichukua lile dumu kama itatokea wakaingia kwenye maji niende mbali japo sikua na hakika kama wanaweza ingia majini nikaenda nalo dumu mpaka kwenye maji kule nao hao mi nikaingia kwenye maji wao wakaishia ukingoni pale mwa maji ufukweni.
Nilikaa ndani ya maji mule karibu saa nzima wao wapo pale nje wana nisubiri mi nawatizama tu pale baadae wakati Giza linaingia wale nikawaona wanaondoka wakapotea nami nikarudi pale kibandani japo nilikua na hofu lakini mara nyinngi nyani inapofika usiku huwa ana ujanja wa kiasi hicho kwaiyo nilirudi pale bandani.
Siku ya pili asubuhi baada ya kuamka tu ile nikaanza kusaka msosi kuwinda wale wadudu mule pembezoni mwa fuke aisee nikakutana na mshikaji mmoja kati ya wale ambao tuligongwa na meli ambao tulifika kuweka makazi pale kisiwani nilimkuta akiwa katika hali mbaya.
Kachoka na alafu ana vidonda vya kung'atwa na wale panya ambao nilikua nawatafuna nikiwapata pale kibandani wanapokuja kusaka masalio, jamaa kumbe nae pale katika kusambaratishwa aliogelea na kipanda cha ubao cha boti na pale alifika Ila sasa alivunjika mguu mfupa ulikua nje unaonekana
Sasa pale alivyofika mwanzo alikua anatafuta chakula kwa kujivuta kutokana na kuhumia mguu Ila mbeleni alishindwa ndio mana akazoofika nami nilimkuta kwenye hali iyo.
Akaniambia pale yeye angeshakufa isipokua kuna usiku mmoja wakati kama amelala kuna wadada wawili walimtokea yani ndotoni akiwa kwenye usingizi walifika wakiwa na marash yani wananukia kisha wakampa mpole na wakamuuliza hapa mmekuja kufata nini?
Kisha wakatoa kinywaji flani kama maziwa wakampatia anywe akanywa baadae alishtuka na aliweza kukaa kama takriban siku tatu au nne pasipo kusikia njaa.
Jamaa alikua kwenye kauli ya mwisho na ile kuonana na Mimi ndio Mara ya mwisho kwani akuchukua mda alifariki pale pale mbele yangu mwana alikufa nikimuona kumbuka mtu wa pili namshuhudia akifariki.
Nikachimba shimo kumsitiri mshkaji na nikamuhifazi nikampigia dua njema aendako ki ukweli sikua na raha siku iyo maana sasa hisia mbaya zikawa zinanijia kwamba hapa nami nitakufa tu japo nilikua Nina nguvu zangu bila shida yoyote mana sikuumia popote.
Pia pale kisiwani niliiishiwa maji nikawa natumia yale maji yanayopatikana kwenye miti flani unaikata kisha inamwaga maji ya kutosha ndio nikawa sasa natumia ayo.
Siku zilikatika, siku moja sasa nikiwa pale ufukweni kwa mbali nikaona kimeli kidogo ivi kipo na jahazi nyuma wamelifunga wanavuta na walikua wanakuja upande niliopo Mimi pale ufukweni apo nilijificha kwanza nikiwatazama walifika mpaka pale wakashuka walikua ni wasomali walishuka na mirungi na bunduki alafu wale kumbe walikua ni mahalamia wa kuteka meli baharini.
Baadae Mi nikajitokeza, fasta sana wakanipigisha magoti na kuniweka chini ya ulinzi mitutu yote kwangu wakaniuliza jina langu pia dini yangu kiswahili wanakielewa nikawatajia mi ni muislamu wale jamaa nao pia ni ivyo ivyo nivyotaja jina wakasema kuna nabii mwenye jina lako alipata matatizo na akaja kuokolewa na wapita njia una mfahamu?
Nikamtaja basi wakasema nawe pia umeokolewa na sisi pia wakaniambia nisome sura flani ivi ya kufungua ibada waislamu wana elewa ili ufanye ibada unaanza na sura iyo inaitwa surat infaata nikawasomea vilivyo mpaka mwisho uzuri nilikua nafahamu wakaelewa kwa kuitikia msahalaah na kunikaribisha .
Katika wale kwenye lile kundi pia kulikua na mtoto wa kike na pia alikua na kaka yake uyu wa kike aliitwa Sofia na kaka mtu aliitwa Masud yule sofia nilimuona na silaha
sub machine gun (SMG) double magazine zilizo jaa risasi na wale wengne walikua na bunduki za AK47 fourty seven sasa nilijiunga na wale jamaa kwenye ile kambi tukawa pamoja yule Sofia alikua akikaa sana na Mimi akiniulizia sana story jinsi nilivyoweza Ku survive
pale nilipo
basi alikua anapenda sana zile story wale wasomali kufika kwao pale chombo chao kilikua na matatizo ..................................
Tupumzike tutarejea Latino is on....
HAPO☝🏾 NDIPO STORY HUWA ZINAANZA KUHARIBIKA.kulikua na mtoto wa kike na pia alikua na kaka yake uyu wa kike
Unampangia wee nani? Aachane nazo wakati.ndio maisha?Ninafuatilia story yako
Kulingana na experience ya humu na kama unataka kweli kutushirikisha story yako
Ishu zako na Sofia achana nazo
Simulia ulivyoendelea na hao wasomali ishu za malavidavi achana nazo mzee
Sent from my SM-J730GM using JamiiForums mobile app
Akileta story za Aofia hamna uzi hapoUnamp
Unampangia wee nani? Aachane nazo wakati.ndio maisha?
atakula kona maana record inaonesha toka kwa khumbu, kanyaAkileta story za Aofia hamna uzi hapo
Mtaanza kumuita aje aendelee na hatokuja
Sent from my SM-J730GM using JamiiForums mobile app
Hawa hawajifunzi tu wanamwambia alete hicho kipandeatakula kona maana record inaonesha toka kwa khumbu, kanya