Latino na harakati za kuzamia ughaibuni mpaka kutoswa baharini

Big up sana mwamba [emoji2936][emoji2935]
 
Nilikwambia hizi kitu zenu zikifikaga maeneo hayo hata kama umekooi huko huwa zinaanza kuota kutu!.
ila niseme kitu Mimi na Sofia tuliingia kwenye mahusiano lakini aikua mahusiano ya kujiachia ni mwendo wa mpela mpela kibabe na Mara nyingi mi sikua muanzaji mpaka aanze yeye kisha mim ndio nijibu mashambulizi kwake
 
Tuendelee
Latino....... Mpaka kufika uko msituni ilikua ni mwendo wa kukatiza porini akukua na bara bara za gari ni pori kwa pori pia mule msituni kulikua na kambi za majangiri ambazo nazo zilikua na viongozi mule porini kwaiyo sasa yanafanyika mandalizi ayo ya unga pia vidumu vya maji,
lakini kwangu nilikua mgeni ndio nakwenda uko kuanza iyo kazi pia wale wazee walikua na vijana wao kama Mimi ambao tulikwenda uko pamoja
kabla ya hii wakati nipo mdogo nilishawai kwendaga kuwinda na babu uko mwanzo sasa hapa ilikua kwa muda mwingne ukubwani sasa nikiwa na dingi.

siku ya safari tena ndio ilikua tunafanya matambiko ya tuendako pia kujua sheria za uko yani namaanisha mfano sheria hii ilikua kwamba kule msituni ndio kuna itwa nyumbani na nyumbani kunaitwa viameni yani sehem uliyo iacha kuitelekeza kisha unaenda nyumbani msituni kuanzisha makazi, pia kulikua na halama uko msituni sie wageni vijana ndio tunafundishwa kazi.

Lakini katika lile kundi tulikua tunafika mpaka idadi ya watu 10 na zaidi tunakua wengi ivyo kunahitajika umakini maana unavyo kwenda uko kunakua na mawili kurudi au kutokurudi sababu kule unakutana na walinzi wa wanyama pori wale magemu ivyo unaweza kutana na mpambano wa awa jamaa ikawa hatari ufe au ubaki mzima ni vita. Yaani atakae muwai mwenzio ndio kashinda ukichelewa umekwenda na maji basi hizi tambiko panakua na kiongozi mkuu wa safari akiongozwa na mtaalamu kufanya tambiko kwa kuangalia safari itakuaje na ata uko tunako kwenda kwamba wapi panafaa na wapi apafai na ata akisema tuvunje kambi tuondoke akuna kusuburi ni kuondoka.
Uyo kiongozi pia anakua na hirizi moja kubwa inapumua na inatoa mlio wa dondora uyu mnyama yupo na kiunoni yupo ka nyingu uyo mzee anaivaa ile hirizi kiunoni linakua na mkanda.
sasa kama sehemu kuna tukio lilenataka kutikea lile irizi linatoa taarifa linakaza pale kiunoni ivyo tunajua hapa kuna lolote inakaza na kutoa ule mlio kuhashiria pana hatari.
Pia mama mmoja wa mkuu wa msafara nae anafanya tambiko mnakaa mstari yeye yupo na kinu na mwichi anatwanga nafaka flani kisha ule unga ndio anatumwagia mmoja baada ya mmoja kama kutupa baraka tuendako kisha yeye akimaliza kutwanga zina pigwa risasi juu hewani tatu kuashiria sasa safari imebarikiwa kule msituni kwenda bila kufanya ivyo kunakua na mengi mfano mnaweza enda sehemu ambayo ina mnyama lakini nyinyi msimuone mnaweza kaa ata wiki amjapata kitu ivyo pale mnalaisishiwa kazi.

Niseme kidogo kulikua na waarabu flani ivi wao walikua wanakata kibali cha kuwinda na walikua wana mkodi muwindaji moja ya wawindaji ambao waliwai wakodi alikua ndani ya lile kundi letu awa awakufanya tambiko lolote sasa yule mwindaji kwenye safar siku iyo aliwaambia safari hii tusiende ila wale walifosi kwamba wacha twende wanajiamini ivyo yule muwindaji wakamuacha wakaenda wao kama wao kuwinda.
Ila walimchkua jamaa mmoja wa pale kijijin ambae anaya fahamu maeneo ambayo wanyama upatikana kwa wingi walivyokwenda walikaa karibu siku tano pasipo kumuona mnyama yeyote mpaka vyakula waliishiwa, katika kuendelea kuwepo jamaa wa kijini yule. akaja akamuotea fungo mnyama ambae yupo ka mbwa ila ana mabaka mabaka ana arufu kali sana ata akigusa mti anaacha harufu na utajua hapa alipita mnyama gani sasa yule jamaa e katika kuzunguka peke ake akamkuta akampiga risasi.

Ila kichwa akamkata na kumtoa manyoya akamuondoa miguu mkia na kubaki mwili tu kule akawadanganya uyu ni swala jamii mpya na wale awajui pia wana njaa wakambanika safi kitoweo. Walipokuja kula ile nyama jamaa wali fungulia koki wali arisha vibaya sana na safari ikaishia hapo wakarudi nyumbani wako hoi bin taaabani walikosa matambiko pia kukurupuka ikawa bahat mbaya kwao.

Ivyo safari ikaandaliwa vixuri na kisha kuingia mzigoni na safari ilikua ya usiku sababu ni safari ya siri. Basi tukaingia msituni na kwenda kutafuta eneo ambalo tutaweka kambi letu na kuanzia mawindo hapo.
Niongee kitu apo nimeongea maandalizi na mwanzo nilipoanza safari hizi za mawindo ivyo safari zilikua nyingi tulishafanya isipokua sasa nagusa moja ya safari ambayo tulipata kisanga.


Siku iyo bana tulipiga nyati mmoja na kongoni awa wana pembe ndefu wapo ka nyumbu ivi,
sasa kuna jamaa zetu wawili mmoja anaitwa gogo jina la utani alikua mbavu hasa giants ana nguvu sana sasa wakati wanaleta nyama kwenye kambi zile nyama zipo kichwan zimewafunika awaoni mbele vixuri wakasimamishwa njiani kucheki vizuri ni wale askar wa wanyama pori game leserve sasa mmoja wetu sisi aliona tukio ivyo na pale kambini tukatoweka haraka sana wao walipokuja awakutukuta.

Awa jamaa sasa niwaeleze mkasa wao ambao uliwakuta walipokuja kutusimulia baada ya kutoka miez mitatu mbele walitokaje na ile ilikua kesi kubwa.
Jamaa walichukuliwa wakiwa na nyama zao zile wamebebeshwa kama ushahidi kuelekea morogoro walitembea pori kwa pori mguu kwa mguu wakifika mahali wamechoka. wanapumzika safari inaanza ivyo ivyo.

Sasa walifika sehemu flani usiku mkubwa wakapumzika wakaweka mahema kisha wakatulia pale jamaa wamefungwa kamba kwenye vigogo kwa nyuma ya mikono wakawasha moto na kulala hapo wakati huo ile mizigo ya nyama ipo pale wakaja fisi maeneo Yale bila shaka walipata harufu wale magemu askari wamelala fofo usingizi mzito kutokana na kuchoka na safari wale fisi wakabeba nyama yote ile na ule ndio ulikua ushahidi wao
wale jamaa sijui ndio zile tambiko wale askari awakushtuka na fisi walikua wengi waktembea na nyama yote .
Asubhi wale askari wana amka wanakuta jamaa wapo ila nyama akuna ikabidi waingie kazini kuanza kusaka zile nyama jamaa waliska saka mpaka....
akuna kitu akuna walicho ambulia fisi walitokomea nazo mbali sasa ushahidi umepotea wakawa wanabishana tuwaache wengne twende nao itajulikana mbeleni mwingne akasema mbona mmoja ana kisu utakua ushahidi tosha huu japo wanajilaumu mno.

Jamaa waliondoka nao mpaka sehemu husika uongozini kwamba jamaa tumewakamata kwenye hifadhi majangiri ushahidi kisu hiki hapa yule jamaa gogo akamwambia mwenzake hii kesi tunagoma na tunasema sisi tulikua wapita njia tu katika mto ruvu hiki kisu tulibeba kama msaada kwetu unaweza pata shida kika tusaidia atuna bunduki wala nyama iweje waseme sisi majangiri ???!
................ Tutarudi kabla ya mtanange ili

Tukashudie nani atapigwa na kitu kizito kichwani
Soon tukutane tena
 
Latino stori yake si ndo anasimulia kule YouTube? Namfatilia sana huyo jamaa anamikasa flan ya kweli lakin ndani yake ina uongo mwingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…