Latino na harakati za kuzamia ughaibuni mpaka kutoswa baharini

Tuendeleee

Latino........ Yule jamaa Akamwambia mwenzake hapa akuna ushahidi kwayo kesi tunaikataa
ivyo wakiwa kwenye hukumu jama wakahojiwa walitoa maelezo Yale Yale ambayo walisha yapanga waongee wakiwa kwenye kesi .

Wale askari walikaza kamba kwamba hawa sisi tumewakuta na nyama sasa mkuu anauliza izo nyama zikwapi wale jamaa awaeleweki ivyo washkaji wakashtakiwa kwa kosa la kukatisha kwenye hifazi kifungo cha miezi mitatu kipind kile iliesabiwa usiku na mchana ivyo ikawa mwez mmoja na nusu.

Iyo ilikua ni story ya wale jamaa wawili baada ya kurudi nyumbani kutoka kwenye makasa wao.
Turudi sasa kwa upande wetu siku iyo tupo pale kambini kama kawaida ghafla walikuja washkaji wawili wapo uchi wa mnyama kila kitu waz waz wamechoka alafu wamechanika chanika mwilini na miiba , tukawauliza vipi imekuaje wakataja walipokuepo na pale walikua wamekimbia takriban masaa matano ivi wapo hoi iyo kambi waliokua ni mbali sana na pale wakasema wakati tupo kambini kule maji yalituishia sasa tuakenda kufata maji kwenye mto uliopo ndani ya hifazi mule tulivyofika pale tukachota maji kisha tukaona ngoja nasi tujimwagie maana mule maji ni hadimu shida kuyapata sasa tumevua nguo zetu tupo ndani ya maji tunaoga askari hawa hapa inabidi wajisalimishe jamaa wakaona hapa njia ni kusepa wana ondokaje wakazama ndani ya maji kupiga mbizi mbele kwa mbele wale askari wasivyo na huruma wakaanza kupiga risasi kwenye maji
mule kwenye maji mna majani majani baada ya ilo zoez awakua na uhakika kama wamewapata au vipi wakaona wamwage petrol kwenye maji
petrol ya kipindi icho sio kama ya sasa ivi wakamwaga juu ya maji wakapiga moto wale jamaa wamekwenda mbele. wakiibuka juu moto inabidi wazame chini Yale majani yana miba miba yana wachana akuna namna walifanikiwa kutoka mbele uko wakatembea mmoja alifika nywele zimeungua kidogo pia wako peku kuna mmoja alichomwa na mwiba wa mti wa mtarula mguuni majani yake hua anapenda sana kula twiga huu mti umezungukwa na miba sana nakumbuka kuna jamaa yetu mmoja alipanda huu mti baada ya kukimbizwa na nyati baada ya kumjeruhi na yule nyati alipiga San ule mti alichoka akaondoka jamaa kushuka tulitafuta miti ya zarula tukapanga ngazi ndio kushuka na hata alivyoshuka chini tulimtoa miba nyingi mpaka alizimia na miba zile zina sumu .

Wale jamaa tuliwapatia huduma tukawapa mavazi vipensi kisha chumvi kisu maji unga na mboga pia kiberit maana yake pale ilibidi waendelee na safari sababu awajatoka pale kwetu jamaa walitushukuru waka enda zao.

Sisi tukaendelea na mawindo yetu siku iyo kumekucha mapema mzee wangu alimuona ndege flani ivi ambae hua ana onesha ishara ndege uyu ana kawaida ukimfatilia hua ana kupeleka sehemu labda pana asali au kitu kingne ambach pia yeye ufaidika mfano asali akikupeleka apo ujue anatak utoe asali ila yeye apate njia kula watoto wa nyuki watu wa porini porini wana elewa sana hii.

Dingi alitoka na jamaa wawili waka enda kule kumfatilia yule ndege walikuta pango lina tundu katikati alafu kuna nyuki wapo wengi na asali ya kutosha wale nyuki walikunywa ile asali mpaka wali lewa wakawa wana ruka tu jama mmoja akafata vyombo aliporudi mmoja wao akaanza akatoa sega akatia kwenye chombo akatoa jingne chombo ki kajaaa full
Wakchukua chombo kingine tena kuingiza mkono kutoa mkono ukanasa ndani ya lile pango kwa vile walikua ni watu wa matambiko wakajua hapa kuna mzimu ndani ya pango ivyo auruhusu tena kuchukua ile asali waliochukua inatosha ivyo ikabid sasa waanze kuongea maneno ya kimila kutambika ili jamaa aachiwe ule mkono iliwauchukua karibu nusu saha ndipo jamaa mkono ukatoka na bahat nzuri ata askari awakupita mitaa ile apo wakaondoka kurudi kambini hapa yalikua ni mambo ya mizimu kwa wale wenye imani izo wana elewa kuhusu mizimu uko mapangoni.


Walivyorudi tukaenda sehemu moja ivi kuchota maji lakini maji ayo hua yanabadilika sometimes yanakua mekundu ivi yanabadirika badirika ni kibwawa flani inasemekana iyo sehemu kama ni mwanamke akiwa katika siku zake Basi aluhusiwi kuchota maji apo au akiwa mjamzito aluhusiwi ana potea akija apo.
Tukachota maji tukaondoka sasa katika mizunguko yetu siku iyo tulifika sehemu flani palikua na mafiga matatu ya kupikia kwenye Yale mafiga palikua na gogo moja kubwa ambalo ukiweka figa moja upande huu na jingne upande mwingne kisha na lile gogo yanakua matatu tukaweka kuni na kuanza kupika ugali na mboga baada ya kumaliza sasa tunakula.
Ghafla lile gogo kubwa likaanza kutikisika alafu linatoa ka utomvu sasa tukashangaa ina maana ili gogo ni bichi au vipi ghafla likaanza kuondoka kumbe ni kiumbe alikua ni chatu mmoja mkubwa sana kumbe ule moto ndio ulimfanya pale aondoke ulimzidi na pia watu hua wana kaa pale bila shida kumbe ni chatu mkubwa mrefu sana anakaribia mstimu inavyoonekana uku kwetu ndio kulikua mkiani kule mbele ndio kichwa kilipo ina maana pale alitega tu siku nyingi kama mnyama atapita kule kichwani ana mnasa na sio lahisi kugundua kama uyu ni nyoka jinsi alivyo na mwili wake ulizungukwa kama na udongo udongo ivi kwaiyo kule mbele alikoelekea na kutokomea msituni ndio kilipo kichwa bila shaka.

Lakini nyoka hawa wakubwa wanakua kama na ushetani ivi na huwa ni nyoka ambao wanaweza leta maafa makubwa mwisho wa awa nyoka unakuaga baharini uko
atujui ki ivyo kubaki kwao hapa ardhini huweza kuleta majanga kwa viumbe wadogo maana yanakua makubwa mno.

.
Wakuu ni mkasa wa Latino ayo ni maneno yake una Uhuru wa kuamini au kuto amini ni wewe.
.,....................

Itaendelea tunao fatilia Basi tuzidi kuepo........
Apo chini Latino akiwa kwenye moja ya interview akiadisia mkasa wake uyo mwenye mzula.
 
Dah Latino vp mbona epsod haziendeleiiii
 
Tawire
 
hapo kwenye chatu ndipo latino kaniacha na kalamu mdomoni[emoji52][emoji52][emoji52]
 
hapo kwenye chatu ndipo latino kaniacha na kalamu mdomoni[emoji52][emoji52][emoji52]
Katoa maelezo mengi sijaweka hapo nafikiri ndio kalamu ingeshka kabisa mdomo kuna ile ishu ya nyoka kuvutwa na minyororo baharini kuelekea angani hii mada humu ndani nishawai iyona kuna Uzi upo.
 
Katoa maelezo mengi sijaweka hapo nafikiri ndio kalamu ingeshka kabisa mdomo kuna ile ishu ya nyoka kuvutwa na minyororo baharini kuelekea angani hii mada humu ndani nishawai iyona kuna Uzi upo.
ishi ya nyoka kupaa,hii nayo nyingine wala sio nyoka.
 
Tuendelee
Latino...........
baada ya misuko suko iyo uko hifadhini tulirudi nyumbani na zile nyama tulizo toka nazo porini tuliuza baada ya kuwasili tu ivyo wana kijij walijua tusharudi ivyo walikuja kwa wingi kununua nyama pori na pia nyama pori upendwa sana zina utofauti mkubwa na hizi nyama za hawa wanaofugwa.

Alafu pia ilikua ni mboga ya msimu ambayo mpaka watu waingie chaka waende huko ndipo warudi na nyama baada ya kukaa kwa kipindi kirefu .
Baada ya kufika nyumbani na kukaa tukisubiri safari nyingne pale nyumbani mi hua sikai bure sababu tulikua karibu na msitu ambao una vinyama vidogo basi mi hua natega mitego kuwanasa.

Lakini Pia hufanyika Yale maandalizi yakuandaa safari wale wa mama huandaa unga na mzee hua ana Fanya maandaliz yake hapa mzee huandaaga pombe moja ivi inaitwa konyagi mwitu dingi alikua anatengeneza mwenyewe hii alikua mtaalaamu sana konyagi mwitu maarufu kama gongo tena ile grade one ambayo kama ukiiwasha moto inawaka inakua na alcohol kali sana na hata ikikaa sana kwenye jua inaweza lipuka hii kunywa lazima ufanye michanganyo mingne ili kupata grad 2 kupunguza makali maana ile number one hua zinachoma mahini sababu alcohol yake kwanza aieleweki ni ngapi usikute 100 na kuendelea maanadalizi ya gongo ilikua unachukua mapapai yaliyoiva unakata kata unatia kwenye pipa kisha sukari alafu amila unachemsha kwa siku kazaa kila inapofika asubuhi unaenda ikologa kwa muda maalumu mpaka ikamilike kunakua na mtambo maalumu ambao ule mvuke ndio upita uko na kuja kwenye chombo inaanguka tone moja moja mpaka inajaa iyo grade one ata Bomu la asili unatengeneza Yale ya chupa unaweka utambi alafu unarusha umekiwasha.

Hii ilikua inaleta stimu na kujiamini unapokua porini kule na vitu hatarishi kama wanyama n.k
Basi sikai kinyonge nyumbani hapa natega mitego kunasa kina ndezi, ndimba, minawara , kanga kware na wengne, siku iyo nilitega mitego ya kware ambao upendelea kupita kwenye njia za nguruwe mwitu (pori) nilitega mitego ulipofika muda nikaona ngoja nikaangalie mitego yangu ila njia zile za ngurue zinakua juu kuna nyasi kama unapita mtu basi unatambaa nilifika mtego wa kwanza nikakuta kanasa nyoka,
nyoka flani ivi wanakua na miba hapa kichwani wanaitwa mbaru sikutaka kukaribia sana nikachukua manati nilikua nayo Yale manati ya mabomba ya hospital yanyotumika kwenye mkojo kwa waliowai tumia wana elewa habari yake yanavutika sana nikampiga kichwani nikampasua kichwa kisha nikaachana nae.

Nikaendelea mbele nikiwa natambaa kufata ile mitego mingne ghafla mbele nikamuona ngurue pori yupo kwenye nyumba yake shimo alafu ana watoto nikafanya mahesabu ya haraka niludi lakini yule ngurue akaanza kutoka na kuanza kunfukuza ikabidi nigeuke kujiokoa nikatanua nyasi maana zilikua zimefunika juu niakachomoka nae akaja akapita pale akaanza kunifukuza mi mbele ye nyuma bahat nzuri mbele kulikua na mti wa mbungo una matunda yanaitwa bungo nikarukia ule mti ye akapita chini awa ngurue mgongon au kichwan wana manyoya flani ivi makali ka kisu ya mesimama hapa juu nilivyorukia pale nikashtuka kwenye pensi yangu niliivaa uku chini kuna pitisha hewa kumbe alivyonipitia kwa chini alichana nilivyoshuka nikaangalia sehemu zangu zipo sikujiamini wale ngurue sio.

Nikarudi nyumbani,
nikiwa na mzee siku iyo tulienda shamban kwenye mpunga kulinda nguruwe huwaga wanakuja kula mpunga kati kati ya shamba palikua na kibanda alafu unapada juu unalala uko palikua na bati flani tulitega na kamba ukivuta linajipiga linapiga kelele kama kuna ngurue wanakimbia chin ya banda tuliwasha moto mkubw si tukawa juu usiku mi nimesinzia walikuja simba walikua pemben ya shamba mzee alivuta ile kamba bati likajipiga wale simba wakakimbia lengo la mzee kupiga lile bati aliwona wale simba na ilikua pana mbala mwezi.
Mzee akajua wamekwenda
wale simba walirudi tena kuja kuchungulia kilicho wakimbiza muda huu nilwaona sababu lilie bati lilinishtua walikua wawili jike na dume mzee alipopiga awakuondoka waka uzunguka ule moto mzee akapiga tena lile bati wale simba awakua na habari tena na ile kelele wakajua juu kuna kitu wakawa pale pale wasi was wetu isije kibanda kuanguka na tayri kilikua na muda yawezekana nguzo zimeoza au vipi pia tuliomba isje moto ukazima sasa ndio itakua tawala yao ule moto ukaanza fifia sababu akuna wa kuchochea ukazima wale simba walikaa pale muda mrefu wakijua juu hapa kuna kitoweo moto umezima jicho la simba ndio linawaka ka tochi vibaya muda mwngne mbala mwezi ikawa inawaka baaadae inazima sasa kuna watu walikua wa kijiji cha pili ndio wanapita barbarani karibu na shambani pale mzee akawita kwa kuomba msaada waje pale kumsaidia anasumbuliwa na tumbo wale walipokuja pale wale simba wakatoka pale wakaingia tena porini lengo la mzee ilikua waje pale Ili sisi tutoke.
na simba akiwepo mahali ukipita kwa kujiamin lazma atoke lakini atajipanga atocheza mbali na hapo japo kulikua na mawili Liwe tukio kuvamiws au simba waondoke kwa muda kweli walikuja tukatoka haraka pale na wale watu walimfahamu mzee ivyo walimfikisha mpaka nyumbani wakijua anaumwa kumbe aikua ivyo.

Siku Izo zote tupo nyumbani ilikua kwenye maaandaliz yakusubir safar nyingne ya porini siku iliwadia tukaingia seluu uko kumburu siku iyo tulimpiga nyati alipigwa risai nyingi ambazo zingemfanya abaki cha ajabu akawa anaondoka ana elekea msitu flani tuli uita msitu wa kijani ni kijani tupu ila hua una mauza uza ule msitu na sio laisi kuingia kutokana na mauza uza,

kwa risasi zile aikua laisi kuondoka yule nyati.
Aliondoka tukaanza mfatilia tukakuta ameingia kwenye kale ka msitu ikabidi tuingie kwa kumfata yule nyati ile kuingia ulikuja upepo mkali alafu ikawa baridi kali sana ni mchana wa jua huo tukazidi kwenda tukakuta popo wakubwa alafu kuna mbega wale kama ngedere wasafi hivi mbeleni tukakuta kundi la nyati wapo wametulia tu alafu tukakuta nyoka wengi wapo mitini mikia ipo mitini vichwa vina Elea chini ivi atukujua nyoka wa aina gani wale jamii tofaut kabisa mzee mmoja muongozaji akasema tutoke hapa haraka ili eneo sio la kawaida tulitoka na tulivyofika nje hali ikarudi ile ile na baridi ile aikuepo tena.
Yule nyati atukumuona na sisi tu karudi katika eneo letu lile,
lakini pia katika ule msafara yule muongoza kundi anakua ni mtu ambae anshughulika sana na ushirikina ni mwanga uyu muda wowote anakupoteza mkiwa uko porini inakuaje mfano baba yangu Mimi alikua ni mtu wa maono ana mazindiko ivyo uyu muongoza kundi ana kawaida moja ya kuuliza labda mkilala mkiamka kuna yeyote alieota labda kitu flani kitatokea mzee huo uwezo alikua nao wa kuota laikin alikua asemi ukisema linaweza kukuta ili jambo la kuuliwa mnaweza mkaenda mahali pia mpo na uyo muongoza kundi kama pana wanyama anaweza akafanya namna kishirikina tu akawalaza usngiz kisha akapiga wale wanyama mkshtuka ye kashapiga.
Ana waambia mkusanye tu nyama lakini tukio ulioni sasa ikitokea kawalaza kimazngara we ujalala anaweza kukupiga risasi sababu umeona kinacho endelea ivyo anajua wewe una maono anakuua kisha anakata kichwa mwili anafukia icho kichwa mkiwa mnarudi yeye huja usiku kishirikina kubeba anaweka sehemu kadri mnavyorudi mnapo lala njiani ye anaenda anakibeba ivyo ivyo mpaka nyumbani anaenda kufanyia dawa kinakua kinamuonesha vitu vinavyokuja tokea mbeleni.

Yule mtu kitakachokua ni kwamba alikuepo wakati napiga wanyama ila alitoka sijui kaenda wapi ata tafutwa atopatikana itabaki tu kapotea au kaliwa na kule porini mawili kurudi au kubaki uko uko kufa akuna la zaidi ndugu matanga habari imeisha hatari mzee.

Siku iyo katika kuwinda jamaa yetu mdunguaji alimuweka nyati taget akampiga yule nyati akaanza kuja jamaa anapiga nyati aanguki kushtuka uyu hapa alimpiga kichwa bunduki ikaanguka akampiga pembe ya mbavu kisha amkarusha juu akatua chini akaja akamshindilia na kwatu kifuani maeneo ya moyo jamaa alifariki pale pale na nyati nae alikufa hapo hapo.
Tulimzika uko kikawaida aturudi na mahiti njiani utaibeba siku ngapi habari yake ikaisha hapo.

Tulirudi nyumbani toka msituni ila njiani wakati tunarudui tukakutana na mbwa mwitu tulikimbilia juu ya miti wale mbwa walikaa pale karibia masaa matano mpaka kuondoka si tukashuka na kuendea na safari yetu kadri tulivyokua tunakaribia kwetu tukawa tunapungua sababu watu ndio walikua wanafika kwao ivyo mpaka tukabaki wale tunao elekea sehemu moja.
Tulifika kijiji kimoja ivi kutokana na usiku kua mwingi mzee anajulikana kwenye nyumba flani ivi tukaogonga odi tukakaribishwa pale tukaomba moto tukapewa chemsha maji kukanda miguu maana ilikua imevimba tukapika uji tukanywa baba akafanya ujanja wa kuaga kwamba tunaomba tuondoke ilikua ni janja ya kwamba wale wahusika watukatalie kwamba hapana jamani laleni usiku mwingi cha ajabu wakakubali sawa safari njema awakusema tulale kama tulivyo taraji du .

Sasa ikabidi tuondoke wahusika awakurizia tulale pale kilichofanya tutake kulala pale mbele maili kazaa kuna msitu mkubwa ambao eneo hilo wanakaa simba wengi ivyo tuliofia itakuaje eneo lile tukaondoka atujafika mbali akaja kijana wa ile nyumba tuliotoka alitumwa na mzee wake kawaite waludi kulala hapa.
waondoke asubuhi Dingi akagoma akasema tunashukuru sie tunaendelea na safari yetu.
Mungu saidia lile eneo tukapta vizuri atukukutana na simba hata mmoja mpaka sa 11 alafjiri tuakingia kijiji flani tukapumzika mahali kuvizia magari lakini ni Yale ya usiku tu mana safari zetu ilikua usiku kwa usiku sababu sisi ni majangiri ivyo kuna kijij tulipumzika kwa mzee mmoja ivi tulimpa na nyama ya asante lakini nae alitupa pesa japo aikua ivyo .

Lakini pale tulipo kwa mbele kidogo kuna kilabu cha pombe wale magemu wanakwendaga kunywa pombe lakini kuna machawa wao pale kama wakimpata mtu ana nyama pori basi wana washtua mzee alienda fata pombe akakuta watu wanamuulizia kama ana nyama pori sababu alikua mgeni kumbe ilikua janaja tu sababu wenyej watu ndio walituambia mzee angejichanganya ilikua kwaheri.
Tuliondoka salama usiku wake safar ikaanza tena pori kwa pori kijikij kwa kijiji tulifika sehemu flani ivi palikua na makaburi mzee aliisi kitu tukasimama ghafla alipita bonge la paka mbele yetu yuko spidi kali .
Mzee baadae alikuja kutuambia kwamba pale ulikua msafara wa wachawi kiongozi wa msafara alikua albino yupo na usinga yeye aliwaona yule paka ni kama alikua mwangalizi wa njia tu.
Tulifika nyumbani salama na majirani walishajua ivyo asubuhi tu wakaja kununua nyama.....................
Tutarejea......

tuendelee kuepo stor ipo nusu sasa
Load to south
 
Latino ni msimuliaji mzuri sana Kati ya wote waliopita Davistar mata.
Mikasa na matukio akumbanayo mwanadamu ndo elimu yenyewe na sio hii ya english medium.
Nasubiria episode ya 14 itoke
 
Mapenzi ya kiganster na mtoto wa kisomali muharamia hakuna kuvua nguo.
 
Jamaa ni sniper mzuri sana.Watu kama hawa unawapa ajira jeshini au askari game.Au kampuni za uwindaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…