Kwani hivyo vifaa hakuna mamlaka halali zinazotambulika zinazoviuza? kama wameacha watu waviuze kiholela, bila kuwepo mamlaka ya kuvikagua vitokapo na viuzwapo, basi LATRA wakubali uzembe na wasiwaonee hao watumiaji wa vifaa husika.
Nchi imejaa uswahili uswahili tu.
1. Vifaa vyovyote (tv, radio, simu, nk) huharibika kwa sababu nyingi zikiwamo zisizojulikana.
2. Kifaa kuharibika (malfunctioning) hakutabiriki na hakuwezi kuwa kwa aina moja.
3. Zinaharibika ndege angani ije kuwa kifaa cha ki electronic kisichojulikana kwa jina, mtengenezaji au hata ubora wake?
4. Nani anafuatilia kuona vifaa hivi vinafanya kazi inavyotakiwa muda wote?
5. Nani anawajibika kwa utendaji mbovu wa vifaa hivi?
Yako mengi ya kujiuliza kuhusu vifaa hivi ambavyo labda wala havijaidhinishwa na TBS.
Kwa barua ya LATRA wamiliki wale wameadhibiwa kwa malfunctioning ya vifaa hivi.
It is inconceivable!
LATRA anapaswa kuthibitisha mahakamani pasi na shaka kuwa malfunctioning hiyo imeletwa na mtu kwa kudharimia.
Enyi wahanga wa dhwalimu kama hizi unyonge wenu hadi lini?
Mahakamani dhidi ya awaye yote ndiko kunakoweza kuwapo haki.