Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Januari 2023 LATRA ilitangaza maombi ya leseni kwa wadau wenye vyombo vya usafiri kwa ajili ya kusogeza huduma ya usafiri kwa wananchi wanaotumia barabara ya Mbezi Chini inayojulikana kama Mwai Kibaki. Route hiyo ilikuwa inaanzia Bunju na Tegeta, inakuja kuingilia Afrikana Mbezi, na kwenda kuingilia Maringo na hatimaye kufika Kawe.
Njia ina umuhimu wake kwasababu itasaidia wakazi wa barabara hiyo ambao wamekuwa wakisumbuka kutokana na kutokuwa na usafiri wa uhakika kutokana na Bajaj wanazotumia kutokidhi mahitaji yao.
Pia wanafunzi wanalazimika kutembea umbali mrefu sana zaidi ya kilometa mbili ili kufikia shule ya umma iliyo eneo la kwa Zena kutokana na kutomudu gharama za bajaj.
Mamlaka inapaswa kutoa taarifa ya maendeleo ya maombi hayo ili kuleta matumaini kwa wananchi, kuendelea kukaa kimya ni dharau na kutowajibika kwa kushindwa kusogeza huduma hii muhimu kwa maendeleo ya uchumi.