vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 2,474
- 4,726
Katika tembea tembea zangu, mkoa wa Morogoro ni moja ya sehemu ambayo mfumo wa nauli haujakaa sawa. Ukipanda daladala za Dar es salaam mfumo wa nauli umekaa vizuri sana na unaeleweka na inaonesha ni wazi kabisa mamlaka zinafatilia juu ya hilo. Mfano gari linatoka Tandika kwenda Mbezi nauli ipo wazi kuwa kutoka Tandika hadi point fulani ni 500 hadi sehemu fulani 600 hadi point fulani ni 700 na hadi Mbezi ni 850. Hata mtu akipandia njiani, atalipa kulingana na umbali anaosafiri.
Lakini daladala za Morogoro ni wazi LATRA pengine huwaacha wenye vyombo vya usafiri wajipangie ama pengine wana shindwa kuwa na meno ya kuweza kusimamia juu ya nauli.
Nitatoa mifano kadhaa juu ya hili.
1) kwa magari yanaenda Mlali, abiria akishuka mindu nauli ni elfu moja au akishuka Sanga Sanga nauli ni hiyo elfu moja, kitu ambacho sio sahihi. Umbali wa Sanga Sanga kutokea kituo cha soko la Kingalu sidhani kama kunastaili kulipwa nauli ya sh elfu moja (takribani 16km) hapo sijaizungumzia Mindu na Kasanga ambapo ndio umbali mfupi zaidi. Mfano tu kwa Dar, kutoka Tandika hadi mbezi kuna takribani km 29 ukipitia Kimara na takribani kuna km 37 kama utapitia Kinyerezi. Lakini huu umbali wa km 37 nauli yake ni 850 tu, sasa inakuaje kwa Morogoro?
2) Mfano wa pili ni daladala za Kihonda Azimio (Kilolo) hapa kuna mkanganyiko haswa, kuna magari nauli yao ni 500 na mengine ni 600.
Hawa wa 600 ndio wanashangaza zaidi kwasababu hawazingatii umbali mtu anaotumia, ukipanda Msamvu kisha ukashuka kwa Chambo utalipa hiyo hiyo 600, popote pale 600. Kuwa na nauli mbili kwa destination moja ni kama vile hakuna usimamizi kwenye swala la nauli.
Na hili swala halipo kwenye daladala pekee, hadi kwenye mabasi ya mikoani na kwenda wilayani huko. Mfano mwaka jana nauli ya kutoka Morogoro kwenda Ifakara wanatoza elfu 12. Kila gari ilikuwa inakatisha kiasi hiko na abiria wengi walijua ndio nauli nauli halali kumbe ilikuwa sio halali hadi pale LATRA walipokuwa wanastukiza kufanya msako wa tiketi za abiria barabarani ili kubaini kiasi cha nauli walizotozwa.
Kuna siku nilikuwa nasafiri kutoka Morogoro kwenda Handeni, tulivyofika Mkambalani konda anaamua kuwabadilishia tiketi abiria ambayo ina nauli tofauti na uelekeo tofauti badala ya Handeni ikawa ni Mbezi, na nauli abiria wakaandikiwa Moro- Mbezi 7,000/=
Naomba mamlaka kwa mkoa wa Morogoro, jitahidini kusimamia vyema hili swala la nauli.