Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 5,606
- 7,032
Mimi nipo eneo hili la Ukanda huu wa Kaskazini- hasa mikoa hii ya Arusha na Kilimanjaro kwa muda fulani. Kwa muda mfupi ambao nimekuwa huku, nimesafiri kwa nyakati tofauti kwa mabasi madogo (maarufu kama Coaster kwa wenyeji wa huku) kati ya Moshi - Arusha na Arusha- Moshi lakini cha kushangaza sijawahi kuona makondakta wakitoa tiketi kwa abiria.
Na inaonekana wenyeji walisharidhika na hali hii, kwa kuwa hakuna anayehoji. Na mimi pia kutokana na ugeni nimeona niendelee kuangalia hali inavyokwenda kwanza, kabla ya kufanya lolote. Hivyo nimeamua kuanzia na hapa JF kabla ya kuchukua hatua nyingine zaidi.
Kwenu LATRA. Je, mnafahamu kuwa watoa huduma hawa hawatoi tiketi kwa abiria? Lakini inaonekana pia kuwa huwa hamfanyi ukaguzi.
Kama mngekuwa mnafanya ukaguzi mngegundua juu ya upungufu huu na kuufanyia kazi. Au kama mnafahamu, basi mmeamua kulifumbia macho kwa sababu mnazozijua wenyewe.