LATRA mnafahamu kwamba mabasi ya Arusha- Moshi hayatoi tiketi kwa abiria?

Tony Laurent

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
5,606
Reaction score
7,032
Mimi nipo eneo hili la Ukanda huu wa Kaskazini- hasa mikoa hii ya Arusha na Kilimanjaro kwa muda fulani. Kwa muda mfupi ambao nimekuwa huku, nimesafiri kwa nyakati tofauti kwa mabasi madogo (maarufu kama Coaster kwa wenyeji wa huku) kati ya Moshi - Arusha na Arusha- Moshi lakini cha kushangaza sijawahi kuona makondakta wakitoa tiketi kwa abiria.

Na inaonekana wenyeji walisharidhika na hali hii, kwa kuwa hakuna anayehoji. Na mimi pia kutokana na ugeni nimeona niendelee kuangalia hali inavyokwenda kwanza, kabla ya kufanya lolote. Hivyo nimeamua kuanzia na hapa JF kabla ya kuchukua hatua nyingine zaidi.

Kwenu LATRA. Je, mnafahamu kuwa watoa huduma hawa hawatoi tiketi kwa abiria? Lakini inaonekana pia kuwa huwa hamfanyi ukaguzi.

Kama mngekuwa mnafanya ukaguzi mngegundua juu ya upungufu huu na kuufanyia kazi. Au kama mnafahamu, basi mmeamua kulifumbia macho kwa sababu mnazozijua wenyewe.
 
Pole mdau wa maendeleo.

Bahati mbaya wenye Mamlaka hawatumii huu usafiri (coaster). Pia hawatimizi wajibu wao mpaka wasukumwe na kukumbushwa.

Kwa kuepuka kugombana na makonda, huwa nawaomba tiketi kwamba naenda kuitumia kudai kurudishiwa nauli yangu.
#KAZI IENDELEE√
 
Aisee! Kwah hiyo hadi udai. LATRA nawaita tena, timizeni wajibu wenu. Na nyie wamiliki wa hivyo vyombo vya usafiri wahimizeni makondakta wenu kutoa tiketi kwa abiria.
 
Nimesafiri Sana Arusha - Moshi , Moshi -Arusha miaka ya 2012-2016 Nami sijawah kuona tiket
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…