Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Trafiki hawawezi kulifungia gari kwa kosa la kutowasha taa usiku, watamuadhibu dereva. Mabasi mliyoyafungia hayana hitilafu yoyote tatizo ni madereva walizima ving'amuzi, hivyo madereva wangeadhibiwa.
LATRA hayo mabasi yapo barabarani kwa mikopo benki na wamiliki wanatakiwa wailipe hiyo mikopo na kuilipa hiyo mikopo basi linatakiwa liwe barabarani liingize fedha, sasa nyie mmeyafungia hao wamiliki watapata wapi pesa ya kurejesha mikopo!
Latra hayo mabasi ndiyo yanayowaweka ofisini hivyo hamtakiwi kuyaonesha ubabe, wenzenu trafiki hutoa adhabu kwa mhusika, kama gari ni bovu watalizuia kuwepo barabarani na kama gari ni zima watamuadhibu dereva kwa kosa alilolifanya na hawatalihusisha gari.
Nawashauri mbadili adhabu yenu iende kwa mhusika.