Ligi za upinzani wa hoja nazipenda sana Tena sana kwa kuwa mpaka nashiriki nakuwa nimejipanga vya kutosha.
Sasa subiri nikuambie, wewe ni kuadi na umetumwa kufanya ukuadi na ni mtupu wa taratibu na Sheria za usafirishaji za LATRA.
LATRA hawawezi kufanya Kama Trafiki abadani kwa kuwa LATRA ni mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini na vyombo vinavyodhibitiwa na LATRA ni vyombo vilivyosajiliwa kama vya biashara.
Kwa Sheria za LATRA ,kuna makosa ya dereva na makosa ya mmiliki. Anayetakiwa kulipia na kuutunza mfumo wa VTS ni mmiliki ,dereva yeye kapewa gari tu.
Wanaopewa semina na mafunzo ya kuutunza mfumo wa VTS ni wamiliki ,hapo unaona ni sawa kwamba mfumo mzima anaujua mmiliki na ni jukumu la mmiliki kuhakikisha mfumo upo sawa kila siku, eti dereva ndio awajibike kwa makosa ya mfumo?