LATRA Shusheni Nauli, Mafuta yameshuka mara mbili Mfulilizo!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
2-8-2026 mafuta ya Diesel na Pertol yameshuka zaidi, LATRA simameni na Mheshimiwa rais na wanyonge, shusheni nauli mfumukom wa bei uondoke.

Nauli zilipandishwa kwenye Marekebisho yalitangazwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kupitia Gazeti la Serikali mnamo Aprili 17, 2026, na kutoa muda wa siku 14 kabla ya kuanza kutumika.

BABAJI NA BODA BODA:
LATRA , kama mmetambua boda na daladala ni usafiri rasmi, tunaomba muweke nauli rasmi, hasa zile za kuchangia.

 
Mafuta yameshuka sana soko la Dunia yapo bei ya zamani kabla ya vita ila hao Ewura wanashusha kwa kuibia sana wanatamani vita iendelee ili wapandishe tena Tsh 1000 wakishusha ni Tsh 100 kwa lita moja.
 
Watakwambia subiri kidogo nao warudishe hela zao walizopata hasara baada ya kuwacheleweshea kupandisha bei...
 
ulishawahi kuona bei ya soda ikishuka baada ya kupanda? hii mifumo migumu, tutafute hela kumudu hizo gharama
Soda ilikuwaga 250 leo hii 600 pepsico 700 coke duh
 
Mafuta yameshuka kidogo san was hushed ata mia 500 ili naur zishuke pia
Mafuta dar mwaka 2023 ilikuwa 3400+ saivi 2026 ni 3800+

Nauli za mwaka 2023 zilikuwa ndogo sanaaa nauli kubwa sana ilikuwa 900 kwa usafiri wa walala hoi wa daresalama

Dar dom ilikuwa 25000 hadi 28000
Angalia leo hii uone maajabu
 
Mafuta yameshuka sana soko la Dunia yapo bei ya zamani kabla ya vita ila hao Ewura wanashusha kwa kuibia sana wanatamani vita iendelee ili wapandishe tena Tsh 1000 wakishusha ni Tsh 100 kwa lita moja.
LATRA wasimame na wananchi, mafuta ndio yanasababisha mfumuko wa bei.
Jana nimetoka car service kila kitu kimepanda wanasema mafuta.
 
Huwa zikiongezeka kushuka ni ngumu, mbaya zaidi pikipiki na bajaji nauli ni za juu kupitiliza ijapokuwa zinafanya Kazi kama daladala tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…