KERO: EWURA mmetangaza kuwa bei ya Mafuta ya petroli na dizeli imeshuka, JE LATRA nao mbona hawatutangazii bei mpya za nauli?

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
4,994
Reaction score
9,625
Moja kwa moja kwenye kero yangu:

Nimeona tangazo la EWURA kutangaza kuwa bei ya mafuta ya petroli na dizeli imeshuka kwa sh 96 and 151 kwa mafuta yanayoshushiwa katika bandari ya Dar-es-salaam .

Bei mpya
  • Petroli: Sh 3,990 kwa lita
  • Dizeli: Sh 4,182 kwa lita
mpaka sasa sijaelewa kwanini mafuta ndani ya muda mfupi yalipanda kwa zaidi ya sh 1500 ila kwenye kushushwa tunapunguziwa sh 96-151.

Wataalamu mje kufafanua.

Naongea kkwa mwananchi mwenye kipato cha chini kabisa na Kero yangu naielekeza kwa LATRA (mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini) ,vp mbona mpo kimya wakuu hamtutangazii kuhusu kushuka kwa bei mpya za nauli za mabasi ya mikoani, mwendokasi pamoja na daladala?

Kama wamiliki wa vyombo vya usafiri wa ardhini walilalamika kuhusu kupanda kwa gharama za mafuta na kupelekea nyinyi LATRA kututangazia bei mpya za nauli, Vivyo hivyo sisi watumiaji wa vyombo hivi vya usafiri tunahoji ni lini mtatutangazia bei mpya za nauli?

Wananchi tunaoishi kwa kipato cha chini ya dola moja tunaumia kutokana na ongezeko la nauli kwasababu kipato chetu bado ni cha chini.

Iwafikie

LATRA
 
CCM MTANDAO WANATUIBIA WATANGANYIKA.

MAFUTA NI GHALI TANGANYIKA KULIKO ZAMBIA.
 
Nauli zinajua njia Moja tuu YA KUPANDA,KUSHUKA HAPANA!!!
Hata mafuta yafike 2000 Nauli itabaki palepale,hii ni TANGANYIKA mkuu😥
 
Sababu za kupanda bei za nauli ilikuwa ni kupanda kwa bei ya mafuta, ila kushusha watakataa watakuja na sababu za kupanda gharama za uendeshaji. Kwani nani anajali?
 
Songea petrol lita 4190 sa sijui yameshuka au yameongezeka?
 
Kwahiyo Wamiliki wa vyomba vya usafiri wao wapunguze kiasi gani?, hebu tuanze kuchambua hizo asilimia...
 
Moja kwa moja kwenye kero yangu:

Nimeona tangazo la EWURA kutangaza kuwa bei ya mafuta ya petroli na dizeli imeshuka kwa sh 96 and 151 kwa mafuta yanayoshushiwa katika bandari ya Dar-es-salaam .

Bei mpya
  • Petroli: Sh 3,990 kwa lita
  • Dizeli: Sh 4,182 kwa lita
mpaka sasa sijaelewa kwanini mafuta ndani ya muda mfupi yalipanda kwa zaidi ya sh 1500 ila kwenye kushushwa tunapunguziwa sh 96-151.

Wataalamu mje kufafanua.

Naongea kkwa mwananchi mwenye kipato cha chini kabisa na Kero yangu naielekeza kwa LATRA (mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini) ,vp mbona mpo kimya wakuu hamtutangazii kuhusu kushuka kwa bei mpya za nauli za mabasi ya mikoani, mwendokasi pamoja na daladala?

Kama wamiliki wa vyombo vya usafiri wa ardhini walilalamika kuhusu kupanda kwa gharama za mafuta na kupelekea nyinyi LATRA kututangazia bei mpya za nauli, Vivyo hivyo sisi watumiaji wa vyombo hivi vya usafiri tunahoji ni lini mtatutangazia bei mpya za nauli?

Wananchi tunaoishi kwa kipato cha chini ya dola moja tunaumia kutokana na ongezeko la nauli kwasababu kipato chetu bado ni cha chini.

Iwafikie

LATRA
Mbona vituo vya mafuta hawajaanza kutumia hiyo bei mpya?
 
Back
Top Bottom