Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
Peleka mabasi upewe route. Acha kulia lia bila iuchukua hatua.16 Julai 2026
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA),
S.L.P 944
Dar es Salaam.
Ndugu CPA, Dkt. Habibu J. Suluo
YAH: MAOMBI YA KUFUNGUA NA KUSAJILI NJIA MPYA YA DALADALA (MAKUMBUSHO – MAWASILIANO – UDSM – CHANGANYIKENI – GOBA NJIA NNE)
Tafadhali husika na kichwa cha habari hapo juu.
Sisi wakazi wa changanyikeni /UDSM tunaomba rasmi kibali cha kuweka na kusajili magari ya abiria katika njia tajwa hapo juu.
Njia hii inatajwa kuwa na uhitaji mkubwa kutokana na sababu zifuatazo:
Njia tunayoomba ipitwe na magari yetu ni: Makumbusho → Mawasiliano → Mlimani (UDSM) → Changanyikeni → Goba Njia Nne.
- Kuongezeka kwa wanafunzi wa UDSM na wakazi wengi wanaohamia maeneo ya Changanyikeni na Goba.
- Urahisi kwa abiria kutoka maeneo ya Goba Njia Nne kwenda moja kwa moja mpaka Makumbusho kupitia Mawasiliano/Mlimani bila kulazimika kubadili magari mara kwa mara.
- Ughali wa Bajaji na kutokuwa salama hasa kwa watoto wa kike kwa matukio ya kubakwa na kuibiwa laptops.
- Appartments nyingi sasa zimejengwa na kuna wakazi wengi, kurahisisha usafiri.
Tunaomba mamlaka yenu ifanye tathmini ya njia hii ili kuruhusu usafiri kuanza na kupunguza changamoto za usafiri kwa wananchi.
Wasilisho rasmi la maombi haya linaweza kufanyika kupitia mfumo wa RRIMS au kwa kukutana na maafisa wenu kwa taratibu zaidi.
Wako mtiifu,
Mkaazi a Changanyikeni
Nakala : UWADAR
Bajaji za Njia Panda Chuo
LATRA hutangaza rote na kutoa idadi ya magari , sijalia ila nimeongea kwa niaba ya wana changanyikeni.Peleka mabasi upewe route. Acha kulia lia bila iuchukua hatua.
Hakika, ni njia mojawapo ya kuwasilisha kero.LATRA hutangaza rote na kutoa idadi ya magari , sijalia ila nimeongea kwa niaba ya wana changanyikeni.
+255 262 323 930 hii namba tunapiga haipokelewi.
chache, kule si mbsgala na kuna masharti ,angalia hatabajaj na boda za kule ni tofauti kabisa.Daladala zikiwa nyingi chuoni UDSM itakuwa vurugu.
Umekuja lini Dar? Kabla ya bajaj Kulikuaga na daladala za kutosha Ubungo-Changanyikeni, Ubunho-Mwenge (kupitia chuoni)Daladala zikiwa nyingi chuoni UDSM itakuwa vurugu.
ASANTE , SAUTI YAKO HAKIKA ITAFIKA KWENYE MAMLAKA.Ni sahihi kabisa wakazi wa Changanyikeni mnastahili daladala watu ni wengi mno na usafiri ni bodaboda na Bajaj tu from Ubungo njia panda
Changanyikeni Mara ya mwisho nilikuja 2015 kwenye msiba wa Nova. Hivi ile bar Junction bado Ina trend huko Changanyikeni?ASANTE , SAUTI YAKO HAKIKA ITAFIKA KWENYE MAMLAKA.
Ipo, tena imeboreshwa zaidi.Changanyikeni Mara ya mwisho nilikuja 2015 kwenye msiba wa Nova. Hivi ile bar Junction bado Ina trend huko Changanyikeni?
Ntakuja kula gambe siku moja hapo mkuu . Na pale kwa Ndama bar bado ipo?Ipo, tena imeboreshwa zaidi.
Nova mwana sana yuleChanganyikeni Mara ya mwisho nilikuja 2015 kwenye msiba wa Nova. Hivi ile bar Junction bado Ina trend huko Changanyikeni?
ndama mtoto wa ng'ombeNtakuja kula gambe siku moja hapo mkuu . Na pale kwa Ndama bar bado ipo?