Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
16 Julai 2026
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA),
S.L.P 944
Dar es Salaam.
Ndugu CPA, Dkt. Habibu J. Suluo
YAH: MAOMBI YA KUFUNGUA NA KUSAJILI NJIA MPYA YA DALADALA (MAKUMBUSHO – MAWASILIANO – UDSM – CHANGANYIKENI – GOBA NJIA NNE)
Tafadhali husika na kichwa cha habari hapo juu.
Sisi wakazi wa changanyikeni /UDSM tunaomba rasmi kibali cha kuweka na kusajili magari ya abiria katika njia tajwa hapo juu.
Njia hii inatajwa kuwa na uhitaji mkubwa kutokana na sababu zifuatazo:
Tunaomba mamlaka yenu ifanye tathmini ya njia hii ili kuruhusu usafiri kuanza na kupunguza changamoto za usafiri kwa wananchi.
Wasilisho rasmi la maombi haya linaweza kufanyika kupitia mfumo wa RRIMS au kwa kukutana na maafisa wenu kwa taratibu zaidi.
Wako mtiifu,
Mkaazi a Changanyikeni
Nakala : UWADAR
Bajaji za Njia Panda Chuo -Changanyikeni

- Kuongezeka kwa wanafunzi wa UDSM na wakazi wengi wanaohamia maeneo ya Changanyikeni na Goba.
- Urahisi kwa abiria kutoka maeneo ya Goba Njia Nne kwenda moja kwa moja mpaka Makumbusho kupitia Mawasiliano/Mlimani bila kulazimika kubadili magari mara kwa mara.
- Ughali wa Bajaji na kutokuwa salama hasa kwa watoto wa kike kwa matukio ya kubakwa na kuibiwa laptops.
- Appartments nyingi sasa zimejengwa na kuna wakazi wengi, kurahisisha usafiri na watu kuhamia huko