Latra yakataa mapendekezo viwango vipya vya nauli za daladala Dar es Salaam'

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (Latra CCC) limekata mapendekezo ya nauli yaliyotolewa na wadau wa usafiri wa masafa marefu na mafupi.

Uwamuzi huo umefikiwa leo Jumatano Aprili 13, 2022 baada ya Umoja wa Wasafirishaji Abiria Mkoa wa Dar es Salaam kupendekeza kiwango cha nauli kuwa mara mbili ya nauli inayotozwa sasa.

Akiwasilisha viwango hivyo Katibu wa umoja huo, Suleiman Kimwe amesema umependekeza viwango vya nauli kuwa mara mbili ya ilivyo sasa

"Kwa maoni yetu tunaomba ongezeko la nauli ya Sh400 kwa kila njia. Mfano kwa nauli ya Sh500 iwe Sh900 “amesema Kimwe.

Hata hivyo Kaimu Mtendaji wa Latra CCC, Leo Ngowi amesema kuwa safari za mjini ni fupi na abiria wengi wamekuwa wakipanda na kushuka njiani huku mabasi hayo kubeba abiria kupita kiasi.

Katika kuchambua viwango hivyo, Ngowi amesema wamebaini maombi ya nyongeza ni tofauti na bei ya mafuta iliyoongezeka.

"Tunapendekeza wasilisho hili lirudishwe kwa mtoa huduma, lakini kama wanazungumzia hasara pia tunashauri kutumia mfumo wa kuzuia mianya ya upotevu kwa kumtumia tiketi mtandao," amesema Ngowi.

Mwananchi
 
nauli ikiwa mia 9 itapendeza sana na itawakumbusha watu vijijibwalivyotoka
 
Kuna sehemu moja na nunuaga maembe,embe kabla ya huu mfumuko ilikuwa 1000 ila sasa hivi wanauza 1500.Hata kupanda ila sio kwa kiwango hiki.
 
Ni sawa tu, kwa nini wasile kwa kadrin ya urefu wa kamba yaooo
 
Dala dala ziwe phased out na mwendo kasi. Madereva wa dala dala ni manyoko sana.
 
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (Latra CCC) limekata mapendekezo ya nauli yaliyotolewa na wadau wa usafiri wa masafa marefu na mafupi.

Uwamuzi huo umefikiwa leo Jumatano Aprili 13, 2022 baada ya Umoja wa Wasafirishaji Abiria Mkoa wa Dar es Salaam kupendekeza kiwango cha nauli kuwa mara mbili ya nauli inayotozwa sasa.

Akiwasilisha viwango hivyo Katibu wa umoja huo, Suleiman Kimwe amesema umependekeza viwango vya nauli kuwa mara mbili ya ilivyo sasa

"Kwa maoni yetu tunaomba ongezeko la nauli ya Sh400 kwa kila njia. Mfano kwa nauli ya Sh500 iwe Sh900 “amesema Kimwe.

Hata hivyo Kaimu Mtendaji wa Latra CCC, Leo Ngowi amesema kuwa safari za mjini ni fupi na abiria wengi wamekuwa wakipanda na kushuka njiani huku mabasi hayo kubeba abiria kupita kiasi.

Katika kuchambua viwango hivyo, Ngowi amesema wamebaini maombi ya nyongeza ni tofauti na bei ya mafuta iliyoongezeka.

"Tunapendekeza wasilisho hili lirudishwe kwa mtoa huduma, lakini kama wanazungumzia hasara pia tunashauri kutumia mfumo wa kuzuia mianya ya upotevu kwa kumtumia tiketi mtandao," amesema Ngowi.

Mwananchi
Hii nchi ni kama gulio la katerero
 
Safi ngowi wasikubali hyo kitu toka mafuta yapande week sas hakna daladal yoyote imepaki au dereva wake kuacha Kaz kisa mafuta .daladal siko nyingi mtaani na nauli jni ile ile walau waongeze shiling Mia kutoka Mia nne
 
Back
Top Bottom