Latra yakataa mapendekezo viwango vipya vya nauli za daladala Dar es Salaam'

Latra yakataa mapendekezo viwango vipya vya nauli za daladala Dar es Salaam'

Kila kitu kitapanda bei,nauli zitapanda,kwa kifupi wamefanyia kazi maneno ya Mkuu wa nchi,KAZI IENDELEE,ngoja tukazindue Royal Tour kwanza tarehe 18,tutarudi!
 
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (Latra CCC) limekataa mapendekezo ya nauli yaliyotolewa na wadau wa usafiri wa masafa marefu na mafupi.

Uwamuzi huo umefikiwa leo Jumatano Aprili 13, 2022 baada ya Umoja wa Wasafirishaji Abiria Mkoa wa Dar es Salaam kupendekeza kiwango cha nauli kuwa mara mbili ya nauli inayotozwa sasa.

Akiwasilisha viwango hivyo Katibu wa umoja huo, Suleiman Kimwe amesema umependekeza viwango vya nauli kuwa mara mbili ya ilivyo sasa

"Kwa maoni yetu tunaomba ongezeko la nauli ya Sh400 kwa kila njia. Mfano kwa nauli ya Sh500 iwe Sh900 “amesema Kimwe.

Hata hivyo Kaimu Mtendaji wa Latra CCC, Leo Ngowi amesema kuwa safari za mjini ni fupi na abiria wengi wamekuwa wakipanda na kushuka njiani huku mabasi hayo kubeba abiria kupita kiasi.

"Tunapendekeza wasilisho hili lirudishwe kwa mtoa huduma, lakini kama wanazungumzia hasara pia tunashauri kutumia mfumo wa kuzuia mianya ya upotevu kwa kumtumia tiketi mtandao," amesema Ngowi.

Chanzo: Mwananchi
 
Ila binadamu ni wabinafsi yaani iongezeke mia we udouble nauli?ngoja ninyamaze
 
Napendekeza nauli ya kichwa iwe sawa na bei ya lita ya mafuta.uchumi ulisinyaa kwa sasa hela imerudi mtaani.
 
Kimwe simamieni hapohapo.

Huyo Ngowi naye aache ujinga,hajui gari likijaza kupita kiasi ndiyo linakula na wese zaidi?

Kama 900 ni kubwa nendeni "sheli" wenyewe mkanunue hilo wese la 500 mnywe na kukimbia kazini kwa miguu.😁.
 
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (Latra CCC) limekata mapendekezo ya nauli yaliyotolewa na wadau wa usafiri wa masafa marefu na mafupi.

Uwamuzi huo umefikiwa leo Jumatano Aprili 13, 2022 baada ya Umoja wa Wasafirishaji Abiria Mkoa wa Dar es Salaam kupendekeza kiwango cha nauli kuwa mara mbili ya nauli inayotozwa sasa.

Akiwasilisha viwango hivyo Katibu wa umoja huo, Suleiman Kimwe amesema umependekeza viwango vya nauli kuwa mara mbili ya ilivyo sasa

"Kwa maoni yetu tunaomba ongezeko la nauli ya Sh400 kwa kila njia. Mfano kwa nauli ya Sh500 iwe Sh900 “amesema Kimwe.

Hata hivyo Kaimu Mtendaji wa Latra CCC, Leo Ngowi amesema kuwa safari za mjini ni fupi na abiria wengi wamekuwa wakipanda na kushuka njiani huku mabasi hayo kubeba abiria kupita kiasi.

Katika kuchambua viwango hivyo, Ngowi amesema wamebaini maombi ya nyongeza ni tofauti na bei ya mafuta iliyoongezeka.

"Tunapendekeza wasilisho hili lirudishwe kwa mtoa huduma, lakini kama wanazungumzia hasara pia tunashauri kutumia mfumo wa kuzuia mianya ya upotevu kwa kumtumia tiketi mtandao," amesema Ngowi.

Mwananchi
...Yaani Ukitoka MigoMigo kwema TU Faya pale, iwe buku!
 
Awamu hii inaweza zusha taharuki nchini. heri mmeliona hilo mapema
 
Back
Top Bottom