Siku chache baada ya Mwananchi kutoa wito kwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kuhusu njia ya Makongo Juu kuwa na uhaba wa Daladala mamlaka hiyo imetoa mwongozo ukiwataka Wadau kujitokeza kuongeza huduma ya usafiri katika njia hiyo.
Taarifa ya LATRA imeeleza "Katika hatua ya kuboresha upatikanaji wa huduma ya usafiri wa abiria, inatangaza njia mpya (New Route) na zenye uhitaji wa kuongeza idadi ya magari..."