LATRA yawataka wenye mabasi ya abiria kuanza kutumia tiketi za mtandao, watakaoshindwa kufanya hivyo kufutiwa leseni

LATRA yawataka wenye mabasi ya abiria kuanza kutumia tiketi za mtandao, watakaoshindwa kufanya hivyo kufutiwa leseni

Mwanzo ticket mlikuwa mnapataje? Si utaingia ndani ya basi na konda atakukatia ticket kama kawaida kulingana na nauli ya unapoenda.
Kuna kitu kinaitwa Mobile POS, hio inaweza kua popote kwenye gari na njiani watu wakipanda, wanakatiwa tiketi popote pale. Sijui kama hii nayo itatatumika, lakini ndio ilivyo. Huu mfumo mzuri sana, ni watu tu kutoelewa.
 
ITATENGENEZA FURSA ZINGINE KWA WENYE SMART PHONE HUKO MIKOANI FUNGUA BANDA ANDIKA UNAKATISHA TIKETI KWA MTANDAO WE KUWA TU NA SMARTPHONE
Msemaji mmoja hapa kasema ukataji tiketi utaendelea kufanyika kwenye ofisi za makampuni ya mabasi kwa kutumia mashine kama zile za EFD. Kwa hiyo sio issue ya kutumia smartphone!
 
Bora tuanzie hapo maana biashara ilikuwa haiendi kabisa. Maana Kuna watu walikuwa wanajiendesha kienyeji tu. Hapa tutaondokana na biashara za kiubabaishaji maana Kuna makampuni yalikuwa mafia wa kukwepa kodi na kuifanya hii biashara isiwe ya kiushindani.
Tuna miaka karibia tisa toka nauli mpya zitolewe lakini mpaka leo hii Kuna njia hata zile nauli za kiwango Cha chini bado hawajafikia huku gharama zikiwa zinaongezeka kila wakati.
Mfano tu Bei elekezi kwa njia ya mwanza kwa semi luxury ni
Asilimia kubwa ya wachangiaji wa mada hii wamekurupuka kujibu bila hata kujua huo mfumo unafanyaje kazi

Lengo la technologia yoyote ni kufanya mambo yafanyike kwa speed, ufanisi na urahisi zaidi

Kwanza hapa nipende kuipongeza serekali maana abiria hua wanapigwa sana kwenye bei za tickets za vitabu ila kwa hizi za mashine itakua ngumu Kuweka udalali hivyo unalipia nauli halali iliyoandikwa kwenye ticket
Mpaka Sasa hivi hakuna kampuni ambayo ishafikia kutoza kiwango Cha chini Cha nauli za mabasi.
Mfano kutoka dar- mwanza nauli elekezi kwa semi luxury ilikuwa ni 67500 ila wanatoza 40000 ila kwa huu mfumo kutokana na kuondoa udalali tutegemea nauli kupanda na kufikia vile viwango vilivyopangwa na serikali.
Mfano kwa hiyo nauli wanayotoza Sasa hivi mfano mwanza Nina Imani hakuna anayelipa VAt maana Kama no 40000 vat si pungufu ya 7000.
Kwa mfumo huu lazima nauli zipande maana mfumo utajua mauzo yote na tajiri atalazimika kulipa vat apende asipende. Ila mapato kwa serikali na mmiliki lazima yaongezeke.
Hata hivyo tulichelewa Maana wamiliki na serikali walikuwa hawavuni kulingana na uwekezaji.
Mfano mdogo tu kwa Basi ya watu 50 kwenda mwanza. VAT kwa Basi so chini ya 360000 kwa nauli za Sasa ila Nina Imani serikali haizipati.
Kwa mabasi 1500 nchi nzima kwa kiwango Cha chini si chini ya 540mil zinakosekana kwa siku kwa mwezi serikali ingeweza pata hata 16bil kwenye mabasi tu.
 
Na pia basi likiharibika njiani, refund inaweza fanyika kwa watu wote kwenye simu zao au hio safari data zote zikaingizwa kwenye basi litalo kuja wabeba nakadhalika. Digitali uwezekano auna kikomo, ni jinsi tu zile program walivyo zi seti, kila kinacho itajika kinaweza fanyika au ongezwa kwenye mfumo kama akija fikiriwa kwa sasa na hai chukui mda mrefu ku-update system ikabili changamoto zitazo jitokeza
 
Wenye mabasi hameni nchi na mali zenu kuna jirani kibao zinahitaji huduma za usafiri Ruanda,Burundi Malawi yaani msing'ang'anie sehemu haina tija,mtandao wasi wasi unataka watu wakate tiketi,
 
Watakuwa wehu,yaaani hii itawasadia wao/wenye mabasi kunufaika San kwa kudhibiti nauli na mapato.... Hivi unajua juzi tu Xmas abiria walikuwa wanakatiwa tiketi da-mwza Hadi 65k Ila mwenye gar/basi anafungiwa hesabu ya 30/35.

Sawa Ni tulipe kwa kielekrotoniki [emoji3581], japo waanze na Safari za mbali au zile nauli Ni 15k+
Yaani hiyo ya mwanza ndo Bei elekezi sasa
 

Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini ( LATRA ) imetangaza kwamba hadi kufikia January 6 mwaka 2021 mabasi yote yawe yameanza kutumia tiketi za mtandao, vinginevyo watafungiwa kutoa huduma hiyo .

Bado haijajulikana sababu hasa za wenye mabasi ya abiria kulazimishwa kufuata utaratibu huu mpya huku wakitozwa kodi lukuki ambayo wanailipa bila mizengwe yoyote

Tahadhari: kama una safari ya muhimu ni bora ukafanya hivyo kabla ya tarehe hiyo, maana lolote la kukukwamisha laweza kutokea .

Nakulilia Tanzania

===============

View attachment 1668365
Welcome to the digital world. Hii ina maana kuwa sasakila mtu analazimika kulipa kodi
 
Jinsi uneployment inavyokuwa kwa kasi tatizo..

Watu lukuki watakosa ajira...
Hiyo ipo worldwide. Teknolojia inachukua baadhi ya kazi za watu.
Binafsi naona ni sahihi itapunguza usumbufu wa wapiga debe, mapato ya serikali kukusanywa kwa umakini zaidi pia kupanda kwa nauli bila mpangilio. Lazima tukubali mabadiliko wakatafute kazi nyingine.
 
Fursa hiyo kafungue ofisi unakuwa unawakatia tiketi kwa mtandao , unakuwa unalipwa buku au buku 2 kwa tiketi.


Mbona ndege Zina madalali au hujui ?


Kila Kitu Ni fursa
Nilishafikiria hilo,jambo,wapiga debe wajiupgrade kichwani
 
Wenye mabasi hameni nchi na mali zenu kuna jirani kibao zinahitaji huduma za usafiri Ruanda,Burundi Malawi yaani msing'ang'anie sehemu haina tija,mtandao wasi wasi unataka watu wakate tiketi,
Kukata tiketi kwa mtandao ni faida kwa mwenye basi hasara kwa wapiga.Sasa mwenye basi ahame kwa sababu gani?
 
Sasa mtu wa buchosa ndani ndani akitaka ticket na kwenye mambo ya kutumia mtandao yuko chini inakuwaje hapo

Ova
Ukisoma hilo Tangazo unaona wanaanzia route ya Dar to Mikoani. Maana yake Stand za Dsm ndio zinahusika na zoezi hili kwa sasa (ambayo ni Pilot area kwa lugha nyingine). Na nadhani watu wanachanganya. Kinachoagizwa hapo ni Ticketi za kielektroniki (kama ilivyobadilika madukani), na sio kulipia ticketi kwa njia ya mtandao(kama vile unapolipia luku).
 
Mleta Habari hii sidhani kama umeelewa hiyo Tangazo la Latra. Naona umepoliticize habari.

Kinachobadilishwa hapa ni kutoka risiti za mkono kwenda risiti za mtandao (kwa lugha rahisi risiti za EFD). Hii ni njia ya kisasa ya taarifa. Sasa sijui wewe hapo unatatizo gani na mfumo huo.
 
Nilishafikiria hilo,jambo,wapiga debe wajiupgrade kichwani
Kama tiketi hizi zitakatwa mtandaoni hapo wapiga debe hawatakuwa na kazi , lakini kama bado zitakatwa ofisini wapiga debe wataendelea kuula tu
 
Kwa hii mada ndio uone watu wengi hawana ubongo, mwingine mara anakuambia sijui simu vijijini hakuna mtandao. Mwingine sijui sio wote wenye smartphone.
Hawaelewi hata huo mfumo ni kama ule wa efd.
Kuna mabus wanatumia huu mfumo muda mrefu sana
Upendo ya Dar- Iringa nayo ilianza muda tu.
 
Kivipi? Wenzetu sijui hata kama mna vichwa.
Mawakala watakuwepo kama kawaida na wao ndio watakuwa wanakata hizo ticket, wapiga debe wao kazi yao ni kukupeleka kwa wakala
wewe kichwa unacho?umeelewa nnachomaanisha au just unapost tu utumbo???mimi nnaongelea wale mateja pale Ubungo na Mikoani kama Msamvu Morogoro....Ustarabu upo Dodoma new Bus stand akuna mateja pale ndo nnachomaanisha,pia Ubungo akuna mawakala wale ni vishoka tu
 
Ukisoma hilo Tangazo unaona wanaanzia route ya Dar to Mikoani. Maana yake Stand za Dsm ndio zinahusika na zoezi hili kwa sasa (ambayo ni Pilot area kwa lugha nyingine). Na nadhani watu wanachanganya. Kinachoagizwa hapo ni Ticketi za kielektroniki (kama ilivyobadilika madukani), na sio kulipia ticketi kwa njia ya mtandao(kama vile unapolipia luku).
Okk nmekupata

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Ukisoma hilo Tangazo unaona wanaanzia route ya Dar to Mikoani. Maana yake Stand za Dsm ndio zinahusika na zoezi hili kwa sasa (ambayo ni Pilot area kwa lugha nyingine). Na nadhani watu wanachanganya. Kinachoagizwa hapo ni Ticketi za kielektroniki (kama ilivyobadilika madukani), na sio kulipia ticketi kwa njia ya mtandao(kama vile unapolipia luku).
Acha bana hii inatumika hata kwa stand za mikoani kwa baadhi ya mabasi ambayo yaliashaanza kukatisha hizi tickets
 
Tena naishauri serikali kusiwe na kuandika majina iingizwe TIN ya mteja jina litokee, mtoto atatumia TIN yamzazi au mlezi.
Baada ya miaka mitatu ukitaka kusafiri Kodi unayodaiwa ikatwe kidogo kidogo 10% ya nauli.....haijalishi unadaiwa bilioni.
Ukilipa school fee 10% ikapunguze Deni lako TRA, mabenki yaunganishe TIN namba na Tra
 
Back
Top Bottom