Lavalava amka, hatukuoni ukitusua nje ya WCB

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Ada ya mja hunena, muungwana ni vitendo!

Sikia hii, labda kama umezaliwa kuishi na kufa (kimziki) ndani ya WCB. Pengine unalijua hili, na huna cha kufanya kwa maana uwezo wako ndo umeishia hapo.

Madogo wanakuja, madogo wanakua na wanaondoka. Huoneshi kujitanua, ulisikika vema ulipoingia lakini sasa hali ni mbaya.

Usije kusema hujaambiwa, kama kuna wanaokusifia kuwa bado ni mkali basi ujue wanakulamba kisogo. Labda kama una ‘ukali’ mwingine unaokutetea na kukuongezea mbeleko.

Niliwahi kuwa shabiki yako, nyimbo zako kadhaa ziliwahi kunirahisishia ‘kazi’ mahali fulani. Nalazimika kuendelea kukukubali kama sehemu ya fadhila, ila usipoamka utaona vumbi tu.

Siku ukifurushwa hapo ndo akili zitakukaa sawa, kama ni uwezo umegota bora ukimbie kwa visingizio kama yule mwingine kabla ya fedheha ambayo hutoweza kujitetea.

Ukibebwa, jishikie!
 
Brand name zina siri mkuu.
Ukitoboa Kama Mrs fulani usijiinue, jina limekubeba tulia hapo.(cc Flora Mbasha,Upendo Kilahiro nk)
Ukitoboa kwa kuuza matunda mpaka kupewa jina na Jenni matunda,au Asha mchicha usijiinue,kamatia hapo ,unaweza kufanya mengineyo ila usisahau ulikotoka.
Wale waliomshangilia Yesu kwa mitende na kutandika nguo apite kabla ya wiki walisema asulubiwe.
 
Mavoco alishauriwa hivyohivyo leo hasikiki tena,na yule alikuwa mkubwa kuliko lavalava leo hii huyo mnaemshauri ajitoe wcb wakati hana fanbase kubwa sijui mnamtakia nini,dogo ana aina yake ya muziki ambao una mashabiki wake muacheni
 
Hajashauriwa ajitoe, bali aamke ili ajijenge kuna leo na kesho... tazama Mboso kamkuta na ameshajitanua yeye kagota!

Apige kazi, hao hao mashabiki zake basi wanahitaji kumsikia na sio kumhurumia.
 
Ada ya mja hunena, muungwana ni vitendo!

Sikia hii, labda kama umezaliwa kuishi na kufa (kimziki) ndani ya WCB. Pengine unalijua hili, na huna cha kufanya kwa maana uwezo wako ndo umeishia hapo.

Madogo wanakuja, madogo wanakua na wanaondoka. Huoneshi kujitanua, ulisikika vema ulipoingia lakini sasa hali ni mbaya.

Usije kusema hujaambiwa, kama kuna wanaokusifia kuwa bado ni mkali basi ujue wanakulamba kisogo. Labda kama una ‘ukali’ mwingine unaokutetea na kukuongezea mbeleko.

Niliwahi kuwa shabiki yako, nyimbo zako kadhaa ziliwahi kunirahisishia ‘kazi’ mahali fulani. Nalazimika kuendelea kukukubali kama sehemu ya fadhila, ila usipoamka utaona vumbi tu.

Siku ukifurushwa hapo ndo akili zitakukaa sawa, kama ni uwezo umegota bora ukimbie kwa visingizio kama yule mwingine kabla ya fedheha ambayo hutoweza kujitetea.

Ukibebwa, jishikie!
Aende kingmusic alale sebuleni
 
Mavoco alishauriwa hivyohivyo leo hasikiki tena,na yule alikuwa mkubwa kuliko lavalava leo hii huyo mnaemshauri ajitoe wcb wakati hana fanbase kubwa sijui mnamtakia nini,dogo ana aina yake ya muziki ambao una mashabiki wake muacheni
Umenena.
Zaidi angetumia jina alilonalo kufanya biashara nyingine pasipo kuondoka wcb.

Wanaosema atoke wcb watuambie aende wapi ili apate mafanikio zaidi ya hayo kimziki.

Siamini katika kujaza nafasi za watu wengine.
 
Back
Top Bottom