Lavalava amka, hatukuoni ukitusua nje ya WCB

Lavalava anaweza mimi nazipenda nyimbo zake ingawa sijui anakwama wapi maana simuoni akisogea, sijajua kama watanzania ndio wagumu kumuelewa ama muziki wake ndio mgumu kueleweka. Siku akitoka WCB pengine watu ndo watajua uzuri wa nyimbo zake japo ndio atakuwa amepotea
 
Je umeshawahi kununua mziki wake kwenye platform yoyote au kulipa pesa na kuingia kwenye show yake?
 
Nyimbo siwezi kuzinunua wakati wanaziachia bure kwa kina Dj Mwanga, ila namchangia ninapoingia U-Tube na ninaposikiliza kupitia Audiomack/Boomplay. Kuhusu show sijawahi kusikia show yake yoyote kwa huku ninapoishi sasa, labda nimewahi kumuona kupitia show ya Wasafi
 
At least wewe unamchangia kwenye audiomack, boomplay na youtube.

Hawa wasanii mara nyingine wanaangushwa na mashabiki mandazi, wanajifanya wanampenda wakati wanafanya piracy kwenye kazi zake.
 
Kabisa, wengine wanasubiria atoke WCB ndo utasikia wakisema 'Lavalava alikuwa mkali sana, WCB walikuwa hawampi sapoti ya kutosha', kumbe wao ndo wanamuangusha. Huwa najaribu kupitia account yake ya U-Tube huwa naona haisogei, subscribers wanaongezeka kwa mwendo wa kinyonga compared na wanalebo wenzake, hata viewers wa video zake ni wakusuasua na sio kwamba nyimbo zake sio nzuri, nikiingia Boomplay wasanii wenzake wote wa lebo (ukiondoa Queen Darlin) ngoma zao huwa zinatrend, ila yeye ni mara chache, yaani kiutaniutani hata Zuchu atampita. Mashabiki wampe sapoti, ni msanii mzuri au hadi atengeneze kiki?
 
At least wewe unamchangia kwenye audiomack, boomplay na youtube.

Hawa wasanii mara nyingine wanaangushwa na mashabiki mandazi, wanajifanya wanampenda wakati wanafanya piracy kwenye kazi zake.

Bwashee unataka mashabiki tufanyeje, tumchangie pesa akiwa amelala studio.?

Kazi tunazipata kwa njia inayowezekana, ni jukumu lake kuhakikisha anazipata hela zetu.... teknolojia inaturahishia mambo nasi hatuwezi kuwa na huruma yenye gharama.
 
Tuacheni kushauri watu vibaya,lavalava akitoka WCB mziki wake utakuwa mgumu sana maana hana fan base kubwa,kwenye mziki kuna watu wanabebwa na lebo na kuna watu wanaibeba lebo,lavalava anabebwa na lebo nje ya hapo mtamtia njaa tu
 
Bwashee unataka mashabiki tufanyeje, tumchangie pesa akiwa amelala studio.?

Kazi tunazipata kwa njia inayowezekana, ni jukumu lake kuhakikisha anazipata hela zetu.... teknolojia inaturahishia mambo nasi hatuwezi kuwa na huruma yenye gharama.
Wewe ndiyo shabiki mandazi niliyemzungumzia?
 
Back
Top Bottom