MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,580
- Thread starter
- #121
MJ1 Mapenzi hayana formulae... Infidelity ingekua kwamba inasukumwa na sababu moja tu!! Ingekua rahisi saana kupata jibu kua ni nani alaumiwe. Mara nyingi sie wanadamu tuko very quick at judging hasa issue kama hii ya kutembea na kaka/dada wa mwenza wako ikitokea. Naamini kua in different situations na circumstance lawama uhama toka kwa mtu wa kulaumiwa...
..........Hapo nakubaliana na wewe kabisa darling sana tu but hii haikupi sababu ya wewe/yeye kutembea na mdogo/dada/kaka yangu! wanawake/ume mbona wako wengi huko nje??
Thanx AshaDii for this very useful post. Hili pia nalikubali na ninakubaliana na wewe. Kategwa AKAKUBALI kutegeka. AKAKUBALI kutegeka. Still to me sidhani kama anaescape lawama kwa kuwa ametegwa na mazingira!! Ina maana akiishi na dada yake yeye, kisha dadake akawa anamhandle na kumtunza kama ulivyoelezea hapo, atapitiwa pia?Mfano wa pale unapokuta Mumeo kalala na dadako ukitaka umpate nani alumiwe yategemea...
- Je wee kama Mke umeacha kua dadako (awe mdogo ama mkubwa kwako) karibu mno na mumeo... Yaani zile za kutreat kila mmoja wenu kama wife mdogo and mkubwa, utani mwiiiingi... huyo dadako yupo huru mno kwa shemejie uko so relaxed waweza ondoka hata home yeye ndo apike, amfulie ampokee, ahandle nyumba, ahandle watoto... yaani ukiiangalia kwa ukaribu with a detached mind anakua kama mke mdogo/mkubwa vile - Hapo kwa mwanaume yeyote lijali lazima atapita hapo kwa dadako, hasa kama wako so free na wewe ni busy person.
Kwa mke ina maana naye akiwa anaishi na shemejiye ambaye amamcare, handle kuliko mumewe anavyomhandle kwa sababu tu mumeo yuko buzzy ndio umchojolee?? Au ndo mtaniambia kuwa hawa wanaokutwa na situation hii hujikuta tu wameshaanza kukiss na kufanya hayo mambo bila ya kutongozana? na hata ikitokea mara moja basi wananogewa na kuendeleza?? Bado utasema hawana lawama kwa kuwa mume/mke alijisahau wajibu wake??
kutembea ninakokuzungumzia mimi hapa ni kule kwa kumfanya nyumba ndogo/serengeti boy yaani sio ile ya one night stand ambayo inawezatokea hata kwa sababu ya ulevi n.k
Je unajua tabia ya dadako (maana hii ipo saana) kua yeye kutembea na mume wa mtu sio shida kwake, yeye ni mtu wa kujirusha, ndio huja once in a while nyumbani hasa kama ndio siku kachelewa kurudi hataki enda wagongea home but yupo comfy kwako... Yupo free saana tu kwako, aweza ingia chumbani upo na mumeo... kazoeana mno na mumeo, ndo kwanza asubuhi yake anapoondoka lift anapata ya shemeji kwenda kwake.
- Je unajua tabia ya mumeo ya ukicheche.... kwake skirt isipite machoni kwake ni shida kabisa. Mume wa namna hio hafai kuachiwa dadako ndani na akwa nae huru saana. Na lazima umpe warning dadako tabia ya shemijie (thou it is beyond me kwanini aendelee kukaa hapo.
- Hizi sababu ni za msingi sana ninazielewa but inapokuja kwenye AMEKUBALI kuhadaika na kujenga kibanda huwa wanawaza kuwa hawatakaa wagundulike au nini? Na wanapokuwa wanayafikiria haya hawahisi suala zima la lawama?
Ikumbukwe pia kua ndio mwaweza kua mlikutana na mumeo mkaoana... But in the long run tokana na sababu tu kua mapenzi hayana ADABU mumeo anarealise kua the Woman ambae anapenda zaidi kuliko alivowahi penda ni dadako.... na dadako pia aka fall kwa mumeo.... Hapo kweli kabisa na hivi mko karibu ana excuse ya kuja hapo home.... Possibility ya kutembea ni kubwa mno.
So unataka kusema its okay hata akifall kwa mamangu ambaye anahapen kuwa single au binti yangu mkubwa ambaye nilimpata enzi za ujanani?? Kuwa its okay mimi nikajikuta ninafall kwa Baba mkwe wangu au mtoto wa kiume wa mume wangu ?? AishaDii tafadhali usinichanganye zaidi ya hapa nitaokota makopo barabarani mwenzio.
Uwezo wa mwanaume pia yaweza changia hasa kama mwanamke umetoka familia ya kimasikini mno... na mwanaume anale familia yenu kwa kila kitu, yaani ukileta dadako hapo kwa wale ambao hawana ustaarabu kwa wazi kabisa atatembea nae kwa kujua huna la kufanya wala pa kukimbilia....
Hii Darling unanipa jibu la why wengine wanavumilia lakini si nani alaumiwe. Yeye kuwa na pesa zake sio kigezo cha kujivua utu wake na kutembea na dada zangu hata kama amewakuta wanauza Ohio! yaani kesho yake atatembea barabarani kifua mbele wakati tupu yake imeshaonywa na ukoo mzima??
Mimi kama mwanamke nikiwa na pesa zangu namtunza Baba chanja na ukoo wake wote ndo inanipa uhuru wa kuchagua among the bullies?
Hata hivo haya mambo yapo soo complicated na nimegusia hivo kwa mfano but kiukweli sidhani kama nimejibu ipasavo... Ukiangalia hizo baadhi ya sababu ama ambavo vyaweza pelekea... unakuta lawama ina hama from one person to another....
MJ1 Naamini kua wewe ni mzima wa Afya. Nakutakia usiku mwema dear...
Kama kuniweza leo umeniweza. Aksante Mpenzi ah uzima utoke wapi mamii?