Lawama zote za umeme ziwaendee Kitila Mkumbo na Nehemiah Mchechu

Like seriously kwenye kichwa chako unaamini una hoja.

Embu tutajie source za umeme kile mkoa?

Wewe inaonekana uelewa wako ni mdogo sana. Unafoka ukiamini una uelewa, kumbe ni wale ambao wanajua kuhesabu tu, halafu wanaamini kuwa tayari wamekuwa mathematicians. Yaani kwa fikra zako ulivyoelewa hoja ya mleta mada ya kila mkoa kuwa na kampuni yake ya umeme inamaanisha kila mkoa uwe na chamzo chake?

Na vipi zile nchi ambazo hazina vyanzo vyake vya umeme ndani ya nchi, huwa hazina umeme?

Nchi nyingi Duniani zina makampuni ya umeme zaidi ya moja. Mathalani US, jimbo moja tu kama la Florida lina makampuni zaidi ya 20 ya umeme. Jimbo la Alabama lina makampuni zaidi ya qp ya umeme.


Ungekuwa na upeo ungeweza kulipinga wazo la mleta mada kwa hoja au ukayaboresha mawazo yake kwa kuzingatia practibility yake, na siyo kufoka ovyo kiasi cha wachangiaji kushindwa kuelewa ni nini unachokielewa au maarifa uliyo nayo kwenye sekta hii ya umeme.
 
Nisingekuwa na uhakika nisingesema!! Si nyie wenyewe kila siku mnalalama kuhusu umeme na TANESCO, DAWASA, AIR TANZANIA etc!!!!!
Another crappy defensive sentence
thank you

80% pale ndani hata ukiwapa manabii na nitume kuwasimamia wanashindwa because of th culture ya pale
 
Ukiondoa banking sekta, wapi penguins private sector imefanya vizuri ilipopewa ubia na serikali?
 
Una hoja but please don’t compare usa na Afrika
 
Nioneshe nchi moja duniani yenye shirika moja tu la umeme linalofanya production, transmission mpaka distribution lililofanikiwa.

Huwa sikisii.
Huyo Moyor hajui chochote. Mataifa yaliyoendelea yote, yana makampuni zaidi ya matano ya umeme.

UK ina kampuni 37 za umeme. US ina kampuni zaidi ya 100 za umeme. Halafu huyo Moyor anabwabwaja na kujifanya anajua sana.

The United Kingdom has one of the most competitive energy markets with over 37 active energy suppliers and at least 62 who have stopped trading. These suppliers buy energy in the wholesale market, then sell it on to their customers.
 
Boresha wazo la mleta mada kuliko kulalamika tu. Wazo la msingi, kwa kuwa Serikali imeshindwa kama ilivyoshindwa katika mambo mengine, sekta binafsi iingie. Ikiwezekana kila kampuni kupewa mkoa mmoja au mikoa kadhaa, siyo manispaa au miji kumiliki makampuni ya umeme.
 
Una hoja but please don’t compare usa na Afrika
Tukiruhusu kampuni binafsi zitoe huduma ya umeme, hayo hayo makampuni yaliyopo US, UK, na kwingineko, yatakuja kuwekeza huku kwetu alimradi Serikali isivuruge.

Tulishindwa kwenye simu, leo tuna makampuni ya simu, japo sisi si wamilikaji. Tulishindwa kwenye viwanda vya bia, leo wanywaji mpaka wanashindwa kuzimaliza, na sisi siyo wamiliki wakuu. Ndivyo inavyoweza kuwa kwenye sekta ya nishati.
 
Ndio haya yakujiandikia

Nchi ambayo aiwezi simamia shirika moja lake la umeme, litaweza simamia mashirika 25?

Unadhani hayo mashirika ya umeme huko kwa wenzetu yanaweza kata umeme kwa kujisikia tu? Unaelewa fines wanazopigwa umeme ukikatika na regulators wao wa umeme.

Uwezi kuta shirika la umeme huko halina risk report na mitigation strategy kuzuia madhara ya kukosa umeme, vinginevyo utajua rungu la regulator.

Halafu mashirika ya umeme sio sawa, ni complicated business kuliko kwenda kuokota link za wikipedia.

Kwanza kuna national security issue serikali ndio inajukumu la kuhakikisha kuna vyanzo vya kutosha vya kuzalisha umeme wa uhakika; kwenye mapungufu watawekeza wao hata kwa hasara.

Pili uwekezaji ni tofauti na business models za hayo mashirika ni tofauti. Wababe ni wenye vyanzo vya uzalishaji, kinachotokea maeneo mengine unakuta mzalishaji awezi fika anaacha wengine wawekeze miundombinu na kuwalipa kutumia, au unakuta mtu ana surplus ya uzalishaji, mwingine anaona hiyo ni fursa ya kununua huo umeme kwa bei rahisi na kuuza.

Ukitoa makampuni makubwa ambayo yanazalisha, sambaza na kuuza kwa wateja au other business; waliobaki ni very weak. Sera tu za greener investment ku limit carbon emission zikisababisha gharama za uzalishaji kupanda biashara nyingi zinazonunua na kuuza umeme chali, geopolitics za mafuta za muda mrefu kama Ukraine war zimeua kampuni kibao za umeme ambazo hazizalishi.

Ni hivi mnatabia ya kujiandikia mambo bila ya kufanya investigation za kina to how things work, regulated and the role of government kwenye kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana all the time.
 
Shida ya umeme mijambazi ya akina Hilary Clinton na na symbion yao yakatuharibu
 


Soma hizo rules and regulations za kupewa licence ya kufanya biashara ya umeme; breach sasa uone moto wake.

Halafu hayo mashirika yaki fail serikali inayachukua na ina wataalamu wake wa kuyaendesha mpaka watakapotokea watu wengine wa kuyanunua usione wapo kimya ukadhani hayo makampuni binafsi yapo yapo tu; kuna invisible hand ya serikali weka nchi kwenye risk ya umeme uone watakavyokushukia.

Sasa shirika moja lina kushinda kusimamia utawezaje 25.
 
Mengi uliyoyasema ni sahihi. Tunapotofautiana, ni nini kifanyike. Serikali imeshindwa kuendesha na kuisimamia TANESCO.

Tukiwa na kampuni binafsi, angalao tunaweza kupata suluhisho la tatizo la uwezo duni wa Serikali kuendesha shirika la umeme. Tutabakia na uwezo mdogo wa Serikali kusimamia/ku-regulate. Kuliko ilivyo sasa ambapo Serikali iliyo failure kwa kila kitu halafu inalazimika kufanya kila kitu kwenye sekta ya umeme.
 

Hiyo biashara sio rahisi kama unavyofikiria wewe. Ni very capital intensive uwekezaji wake.

Halafu inabidi uzingatie uwepo wa soko la mitaji au investors wa kuwekeza pamoja na government policies zilizopo huko kusaidia wawekezaji. Kwa sasa kuna incentives kwenye green sources so watu wanachukua risks aina maana wana sustainable businesses.

Kingine ni mitaji hakuna nchi duniani inaweza shindana na US kwenye capital market and number of potential investors.

Sasa basi ukienda nchi kama U.K. uliotolea mfano ushindani wa umeme ni oligopoly kuna makampuni kama matano tu ndiyo yenye impact. Hao wengine ni ghasia tu hasa wanaonunua umemea unaozalishwa na wenzao ni very high risk business ndio maana zinakufa haraka. Wengine hao wa kwenye green technologies wanazalisha sijui umeme wa mawimbi, hydrogen and other sources pretty much ni experiments tu at this infancy stages and as far as the government is concerned sio watu ambao kwa sasa wapo katika vichwa vyao kama sehemu ya energy security lakini wanahesabika kama biashara za umeme.

Ni hivi the matter is more complicated ukilipekuwa kwa undani kushinda unavyodhani, halafu rules zake za kuendesha hayo mashirika ukiweka vigezo hivyo kwa Tanzania upati mwekezaji.

Wawekezaji watanzania wanataka kuja kujenga vyanzo hasa vya green, energy (mainly solar and wind), kuuzia serikali huo umeme. Wakitoka hapo hiyo investment inawaruhusu kuchafua kwao wanatumia kama carbon trade initiatives (moja ya rules ni kuwekeza third world umeme safi, na wewe unaruhusiwa kuchafua equal amount huko kwao).

Ni hivi kuendesha reli kupitia line ya serikali au umeme hasa kwa makampuni makubwa rules zake huko kwa wenzetu sio ndogo huko kwa wenzetu na kuchezea fines za £5m kwa makosa madogo tu washazoea, kwenye reli fines zinavuka hundred million easily.

Hiyo niliyoweka hapo juu wote hao ambao biashara zao chali ni wale wanaonunua tu; lakini sio big players.

Shida ya Tanzania ni usimamizi wa serikali kwa TANESCO kabla ya kufikiria kingine chochote; hilo kwanza lirekebishwe.
 
Tukikubaliana kuwa sekta binafsi haiwezi kuendesha sekta ya nishati ya umeme. Na Serikali hii, miaka yote imeshindwa, japo kuna vipindi vichache kulikuwana unafuu; kwa hiyo tuseme hakuna soluhisho, na haya yataendelea kuwa ndiyo maisha yetu?

Kila mmoja anajua kabisa kuwa tupo hapa kutokana na aina ya Serikali ambazo tumekuwa nazo, lakini siyo kweli hatuwezi kuwa na umeme wenye uhakika. Na wala siyo kweli kuwa hakuna watanzania ambao wangeweza kuiendesha TANESCO kwa ufanisi kama kusingekuwa na kuingiliwa na watu wa Serikali wenye madaraka na maamuzi makubwa lakini wenye uelewa duni kabisa. Lakini kuna mwanga wowote unaotuelekeza katika kuondoka kwenye kadhia hii?
 


TANESCO ina assets za 19.5 trillion kwa mujibu wa financial statement na government equity yenye thamani trillion 4 kwa sasa.

Sasa kama unataka kuliuza shirika lote hilo si chini ya tsh trillion 7 walau upate faida. But then hata serikali ikisema iliweke sokoni nani unamjua wewe ana hela ya kununua.

Pili serikali lazima iweke conditions ukishindwa kuendesha wanalichukua, maana TANESCO ina asset nyingi zenye thamani mtu anaweza kununua shirika kwa lengo la asset striping akaanza kuuza majengo ya ofisi, nyumba za wafanyakazi, na asset zingine kwa madai streamlining business (anaanza kuvuna kabla ya hata biashara kurudisha through operation).

Ndio maana kuna post nikakueleza bila ya TANESCO mwekezaji gani unaemjua wewe yupo tayari kuja hata kujenga gas plant ya $1 billion moja, aendeshe mwenyewe, ajenge infrastructure network yake, ofisi zake za kuhudumia wateja na kuuza umeme, magari yake ya kuangalia miundombinu.

Huyo mwekezaji unaemjua wewe yupo wapi, embu ajitokeze tuone kama atakataliwa.

Listen TANESCO ni very complicated umeme wenyewe huko vijijini wanauza bei che kuliko gharama za kuzalisha, unadhani mwekezaji atakuwa tayari kufanya hivyo.

Haya mambo sio rahisi vile kama tunavyojadili humu, unless unshauri shirika litolewe sandakalawe.
 
Suluhisho lipo ni kuikatakata Tanesco kimikoa, ijitegemee kila mkoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…