Acheni lawama, mama alishasema mwisho wa umeme kukatika ni mwezi wa tatu...waacheni TANESCO watekeleze majukumu yao halali
Hata wapewe miaka 20 hawatakuja na Suluhu yoyote..
Kwani haya matatizo ya umeme yameanza juzi wakati wa Samia Suluhu Hassan?
Yameanza seriously wakati wa Jakaya Kikwete pale ambapo watumiaji umeme walipoongezeka sana huku vyanzo vya umeme vikiwa vilevile..
Watu wakatumia fursa ya matatizo haya kufanya ufisadi badala ya tatizo hilo liwafanye watumie akili zao kwa kasi na ubora zaidi ili kuleta suluhu ya kudumu..
Since then (almost 30 yrs now) sababu zinazotolewa ni zilezile na ahadi ni zilezile lakini tatizo liko palepale..
Mzee baba, Hayati John P. Magufuli alijitajidi kidogo lakini amekufa na kufa na reforms zake. Waliokuja wanaendeleza tatizo tu na story zilezile za wakati wa Mkapa na Jakaya Kikwete zimerudi tena..
In my opinion,
FaizaFoxy (mwana CCM huyu) ana hoja ya akili sana na inachohitaji ni kuongezewa nyama tu ktk kuiboresha. Na ofcoz hiyo ndiyo itakuwa suluhu ya kudumu Kwa ishu hii na zingine zote inazohusi maendeleo ya kijamii..
Kwa mfano, si tu Shirika hili livunjwe vunjwe na mamlaka ya usimamizi wa sekta ya nishati iwekwe kwenye mikoa na wilaya...
Hili la kuvunjwa vunjwa ni sawa kabisa.
Lakini kama mfumo wa utawala wa kuteua viongozi DSM au Dodoma na kuletwa na mtu mmoja aitwaye Rais kuja kutawala/kuongoza wananchi wa mikoa husika utaendelea, pendekezo la
FaizaFoxy linaweza lisilete tija inayotarajiwa..
Tunataka watawala wa mikoa na wilaya wachaguliwe na wananchi wa mikoa na wilaya husika na wawajibike kwao katika mambo yote ya usimamizi wa utawala na maendeleo ya jamii ya mikoa husika..
Sambamba na hilo☝️☝️, lazima pia mifumo ya mamlaka ya usimamizi wa kifedha kuanzia vyanzo vya mapato (kodi), bajeti na ajira za wafanyakazi wote ziwe mikononi mwa mamlaka ya mikoa na wilaya husika na sio kama ilivyo sasa kwamba, kodi zote, ajira zote ni mpaka DSM au Dodoma iamue ndo baadae Rais (kwa sasa Samia) ndo aamue mikoani na wilayani tupeleke ngapi na amlete nani na kwa wakati gani ili awatawale wenyeji..
Kwa mfumo huu uliopo sasa ni ngumu sana kutoboa kimaendeleo kwa haraka kwa sabb una - encourage impunity na kutowajibika kwa viongozi..!
Suluhu ni kuwepo na
mamlaka za serikali za mitaa zilizo huru na kamili kwelikweli na sio usanii huu uliopo sasa wa serikali za mitaa Kwa jina tu lakini maamuzi yote ya kiutawala na kifedha yanatoka DSM au Dodoma..