macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Wapo. Tatizo ni kuwa wanachaguana kwa kujuana. Unamteua mtu kama huyu Mchechu unategemea kupata nini? Hawa ni ''wajanja wajanja'' wa mjini tu na hakuna la ziada. Sasa hawa wapo wengi kweli kweli kwenye teuzi za Samia. Au tukubali tumefeli tuajiri uongozi wa juu kutoka kwa mataifa yaliyoendelea. Nchi kama hizi za Scandinavia zina watu waadilifu kweli. Kwanza tuchukuwe kampuni ifanye upembuzi yakinifu kuhusu muundo bora wa shirika halafu zile nafasi muhimu zote tuwape wazungu. Rais akicheza karata vizuri anaweza kupata wataalam kwa kusaidiwa na serikali za nchi husika na hata malipo yakawa chini kabisa. Vinginevyo badala ya kukubali kupewa misaada ya fedha tuombe wataalam waje kutusaidia kuendesha shirika kwa muda fulani.Hata uongozi ushushwe na buibui hakuna Mtanzania mwenye ujanja wa kuendesha mashirika makubwa kwa sasa.
Niambie nani anaeweza kuongoza shirika kubwa bila ujinga?